2 Wafalme 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 10 (Swahili) 2nd Kings 10 (English)

Basi Ahabu alikuwa na wana sabini katika Samaria. Yehu akaandika barua, akazipeleka Samaria kwa wakuu wa Yezreeli, yaani, wazee na hao walezi wa wana wa Ahabu, kusema, 2 Wafalme 10:1

Now Ahab had seventy sons in Samaria. Jehu wrote letters, and sent to Samaria, to the rulers of Jezreel, even the elders, and to those who brought up [the sons of] Ahab, saying,

Barua hii mara ikiwawasilia, kwa kuwa mna wana wa bwana wenu pamoja nanyi, tena kwenu kuna magari na farasi, na mji wenye boma, na silaha; 2 Wafalme 10:2

Now as soon as this letter comes to you, seeing your master's sons are with you, and there are with you chariots and horses, a fortified city also, and armor;

basi mtazameni yeye aliye mwema na hodari miongoni mwa wana wa bwana wenu, mkamweke kitini mwa babaye, mkaipiganie nyumba ya bwana wenu. 2 Wafalme 10:3

look you out the best and meet of your master's sons, and set him on his father's throne, and fight for your master's house.

Lakini wao wakaogopa mno, wakasema, Tazama, wafalme wawili hawakusimama mbele yake; tupateje sisi kusimama? 2 Wafalme 10:4

But they were exceedingly afraid, and said, Behold, the two kings didn't stand before him: how then shall we stand?

Kisha yeye aliyekuwa juu ya nyumba, na yeye aliyekuwa juu ya mji, na wazee, na walezi, wakatuma ujumbe kwa Yehu, wakisema, Sisi tu watumwa wako, kila neno utakalotuambia, tutalifanya; hatutamfanya mtu awaye yote kuwa mfalme; ufanye yaliyo mema machoni pako. 2 Wafalme 10:5

He who was over the household, and he who was over the city, the elders also, and those who brought up [the children], sent to Jehu, saying, We are your servants, and will do all that you shall bid us; we will not make any man king: you do that which is good in your eyes.

Ndipo akawaandikia barua ya pili, kusema, Mkiwa upande wangu, na sauti yangu mkiisikia, vitwaeni vichwa vyao hao watu, wana wa bwana wenu, mkanijie kama wakati huu kesho hapa Yezreeli. Na hao wana wa mfalme, watu sabini, walikuwako kwa wakuu wa mji waliowalea. 2 Wafalme 10:6

Then he wrote a letter the second time to them, saying, If you be on my side, and if you will listen to my voice, take the heads of the men your master's sons, and come to me to Jezreel by tomorrow this time. Now the king's sons, being seventy persons, were with the great men of the city, who brought them up.

Ikawa, barua ilipowawasilia, waliwatwaa hao wana wa mfalme, wakawaua, watu sabini, wakatia vichwa vyao katika makapu, wakampelekea huko Yezreeli. 2 Wafalme 10:7

It happened, when the letter came to them, that they took the king's sons, and killed them, even seventy persons, and put their heads in baskets, and sent them to him to Jezreel.

Akaja mjumbe, akamwambia, akasema, Wamevileta vile vichwa vya wana wa mfalme. Akasema, Viwekeni chungu mbili penye maingilio ya lango hata asubuhi. 2 Wafalme 10:8

There came a messenger, and told him, saying, They have brought the heads of the king's sons. He said, Lay you them in two heaps at the entrance of the gate until the morning.

Ikawa asubuhi, akatoka, akasimama, akawaambia watu wote, Ninyi ni wenye haki; tazameni, mimi nalifanya fitina juu ya bwana wangu, nikamwua; ila ni nani aliyewapiga hawa wote? 2 Wafalme 10:9

It happened in the morning, that he went out, and stood, and said to all the people, You are righteous: behold, I conspired against my master, and killed him; but who struck all these?

Jueni basi ya kwamba halianguki chini lo lote la neno la Bwana, alilolinena Bwana juu ya nyumba ya Ahabu; kwa maana Bwana ameyafanya hayo aliyoyanena kwa kinywa cha mtumishi wake Eliya. 2 Wafalme 10:10

Know now that there shall fall to the earth nothing of the word of Yahweh, which Yahweh spoke concerning the house of Ahab: for Yahweh has done that which he spoke by his servant Elijah.

Hivyo Yehu akawapiga wote waliosalia wa nyumba ya Ahabu katika Yezreeli, na hao wakuu wake wote, na rafiki zake, na makuhani wake, hata hakumwachia aliyesalia hata mmoja. 2 Wafalme 10:11

So Jehu struck all that remained of the house of Ahab in Jezreel, and all his great men, and his familiar friends, and his priests, until he left him none remaining.

Akaondoka, akashika njia akaenda Samaria. Hata njiani karibu na nyumba ya kukatia manyoya kondoo, ya wachungaji. 2 Wafalme 10:12

He arose and departed, and went to Samaria. As he was at the shearing-house of the shepherds in the way,

Yehu akakutana na ndugu za Ahazia mfalme wa Yuda, akawauliza, Ni nani ninyi? Wakamjibu, Sisi tu ndugu zake Ahazia; tunashuka kuwasalimu wana wa mfalme na wana wa malkia. 2 Wafalme 10:13

Jehu met with the brothers of Ahaziah king of Judah, and said, Who are you? They answered, We are the brothers of Ahaziah: and we go down to Greet the children of the king and the children of the queen.

Akasema, Wakamateni wa hai. Wakawakamata wa hai, wakawaua penye birika ya nyumba ya kukatia manyoya kondoo, watu arobaini na wawili; wala hakumsaza mtu wao awaye yote. 2 Wafalme 10:14

He said, Take them alive. They took them alive, and killed them at the pit of the shearing-house, even two and forty men; neither left he any of them.

Alipotoka huko akamkuta Yehonadabu mwana wa Rekabu akija kumlaki; akamsalimu akamwambia, Je! Moyo wako umenyoka, kama moyo wangu ulivyo pamoja na moyo wako? Akajibu Yehonadabu, Ndio. Yehu akamwambia, Kama ndio, nipe mkono wako. Akampa mkono, akamkalisha pamoja naye garini. 2 Wafalme 10:15

When he was departed there, he lighted on Jehonadab the son of Rechab coming to meet him; and he greeted him, and said to him, Is your heart right, as my heart is with your heart? Jehonadab answered, It is. If it be, give me your hand. He gave him his hand; and he took him up to him into the chariot.

Akasema, Fuatana nami, ukaone wivu wangu kwa Bwana. Wakampandisha garini mwake. 2 Wafalme 10:16

He said, Come with me, and see my zeal for Yahweh. So they made him ride in his chariot.

Naye alipofika Samaria, aliwapiga wote waliomsalia Ahabu katika Samaria, hata akamwangamiza, sawasawa na neno la Bwana alilomwambia Eliya. 2 Wafalme 10:17

When he came to Samaria, he struck all who remained to Ahab in Samaria, until he had destroyed him, according to the word of Yahweh, which he spoke to Elijah.

Yehu akawakusanya watu wote, akawaambia, Ahabu alimtumikia Baali kidogo; bali Yehu atamtumikia sana. 2 Wafalme 10:18

Jehu gathered all the people together, and said to them, Ahab served Baal a little; but Jehu will serve him much.

Basi niitieni manabii wote wa Baali, wote wamwabuduo, na makuhani wake wote; mtu asikose kuwapo hata mmoja. Maana ninayo dhabihu kubwa ya kumtolea Baali; ye yote atakayekosa kuwapo hataishi. Lakini Yehu alifanya hayo kwa hila, ili awaharibu waliomwabudu Baali. 2 Wafalme 10:19

Now therefore call to me all the prophets of Baal, all his worshippers, and all his priests; let none be wanting: for I have a great sacrifice [to do] to Baal; whoever shall be wanting, he shall not live. But Jehu did it in subtlety, to the intent that he might destroy the worshippers of Baal.

Yehu akasema, Takaseni kusanyiko la dini kwa Baali. Wakalitangaza. 2 Wafalme 10:20

Jehu said, Sanctify a solemn assembly for Baal. They proclaimed it.

Yehu akatuma wajumbe katika Israeli yote, nao wote waliomwabudu Baali wakaja, wala hakusalia mtu ye yote asiyekuja. Wakaingia nyumbani mwa Baali; ikajaa nyumba ya Baali tangu mlango hata mlango. 2 Wafalme 10:21

Jehu sent through all Israel: and all the worshippers of Baal came, so that there was not a man left that didn't come. They came into the house of Baal; and the house of Baal was filled from one end to another.

Akamwambia yule aliyekuwa juu ya hazina ya mavazi, Uwatolee mavazi wote wanaomwabudu Baali. Akawatolea mavazi. 2 Wafalme 10:22

He said to him who was over the vestry, Bring forth vestments for all the worshippers of Baal. He brought them forth vestments.

Akaingia Yehu na Yehonadabu mwana wa Rekabu nyumbani mwa Baali, akawaambia waliomwabudu Baali, Tafuteni mkaangalie, asiwepo hapa pamoja nanyi mtu amtumikiaye Bwana, ila wamwabuduo Baali peke yao. 2 Wafalme 10:23

Jehu went, and Jehonadab the son of Rechab, into the house of Baal; and he said to the worshippers of Baal, Search, and look that there be here with you none of the servants of Yahweh, but the worshippers of Baal only.

Wakaingia ili watoe dhabihu na sadaka za kuteketezwa. Basi Yehu alikuwa amejiwekea nje watu themanini, akasema, Mtu mmoja akiokoka wa watu niliowatia mikononi mwenu, amwachaye huyo, roho yake itakuwa badala ya roho yake. 2 Wafalme 10:24

They went in to offer sacrifices and burnt offerings. Now Jehu had appointed him eighty men outside, and said, If any of the men whom I bring into your hands escape, [he who lets him go], his life shall be for the life of him.

Ikawa mara alipokwisha kutoa sadaka ya kuteketezwa, Yehu akawaambia walinzi na maakida, Ingieni mwapige; mtu awaye yote asitoke. Basi wakawapiga kwa makali ya upanga; walinzi na maakida wakawatupa nje, wakaenda mpaka mji wa nyumba ya Baali. 2 Wafalme 10:25

It happened, as soon as he had made an end of offering the burnt offering, that Jehu said to the guard and to the captains, Go in, and kill them; let none come forth. They struck them with the edge of the sword; and the guard and the captains cast them out, and went to the city of the house of Baal.

Wakazitoa nguzo zilizokuwamo nyumbani mwa Baali, wakaziteketeza. 2 Wafalme 10:26

They brought forth the pillars that were in the house of Baal, and burned them.

Wakaibomoa nguzo ya Baali, na kuiangusha nyumba ya Baali, wakaifanya choo hata leo. 2 Wafalme 10:27

They broke down the pillar of Baal, and broke down the house of Baal, and made it a latrine, to this day.

Ndivyo Yehu alivyomharibu Baali katika Israeli. 2 Wafalme 10:28

Thus Jehu destroyed Baal out of Israel.

Walakini katika makosa yake Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli, Yehu hakutoka katika kuyafuata, yaani, ndama za dhahabu zilizokuwako katika Betheli na Dani. 2 Wafalme 10:29

However from the sins of Jeroboam the son of Nebat, with which he made Israel to sin, Jehu didn't depart from after them, [to wit], the golden calves that were in Bethel, and that were in Dan.

Bwana akamwambia Yehu, Kwa kuwa umetenda vema kwa kufanya vilivyo haki machoni pangu, kuitendea nyumba ya Ahabu sawasawa na yote yaliyomo moyoni mwangu, wana wako wa kizazi cha nne watakaa kitini mwa Israeli. 2 Wafalme 10:30

Yahweh said to Jehu, Because you have done well in executing that which is right in my eyes, [and] have done to the house of Ahab according to all that was in my heart, your sons of the fourth generation shall sit on the throne of Israel.

Lakini Yehu hakuangalia, aende katika sheria ya Bwana, Mungu wa Israeli, kwa moyo wake wote; hakutoka katika makosa ya Yeroboamu, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli. 2 Wafalme 10:31

But Jehu took no heed to walk in the law of Yahweh, the God of Israel, with all his heart: he didn't depart from the sins of Jeroboam, with which he made Israel to sin.

Siku zile Bwana akaanza kupunguza Israeli. Hazaeli akawapiga mipakani mwote mwa Israeli; 2 Wafalme 10:32

In those days Yahweh began to cut off from Israel: and Hazael struck them in all the borders of Israel;

kutoka Yordani upande wa mashariki, nchi yote ya Gileadi, na ya Wagadi, na Wareubeni, na Wamanase, kutoka Aroeri iliopo karibu na bonde la Arnoni, yaani, Gileadi, na Bashani. 2 Wafalme 10:33

from the Jordan eastward, all the land of Gilead, the Gadites, and the Reubenites, and the Manassites, from Aroer, which is by the valley of the Arnon, even Gilead and Bashan.

Basi mambo yote ya Yehu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na ushujaa wake, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli? 2 Wafalme 10:34

Now the rest of the acts of Jehu, and all that he did, and all his might, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Israel?

Yehu akalala na babaze; wakamzika katika Samaria. Na Yehoahazi mwanawe akatawala mahali pake. 2 Wafalme 10:35

Jehu slept with his fathers; and they buried him in Samaria. Jehoahaz his son reigned in his place.

Na muda Yehu aliotawala juu ya Israeli katika Samaria ulikuwa miaka ishirini na minane. 2 Wafalme 10:36

The time that Jehu reigned over Israel in Samaria was twenty-eight years.