2 Wafalme 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 21 (Swahili) 2nd Kings 21 (English)

Manase alikuwa na umri wa miaka kumi na miwili alipoanza kutawala; akatawala miaka hamsini na mitano katika Yerusalemu, na jina la mamaye aliitwa Hefziba. 2 Wafalme 21:1

Manasseh was twelve years old when he began to reign; and he reigned fifty-five years in Jerusalem: and his mother's name was Hephzibah.

Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na machukizo ya mataifa, aliowafukuza Bwana mbele ya wana wa Israeli. 2 Wafalme 21:2

He did that which was evil in the sight of Yahweh, after the abominations of the nations whom Yahweh cast out before the children of Israel.

Kwa maana akapajenga tena mahali pa juu alipopaharibu Hezekia baba yake; akamjengea Baali madhabahu, akafanya Ashera kama alivyofanya Ahabu mfalme wa Israeli. Akajiinama mbele ya jeshi lote la mbinguni na kulitumikia. 2 Wafalme 21:3

For he built again the high places which Hezekiah his father had destroyed; and he reared up altars for Baal, and made an Asherah, as did Ahab king of Israel, and worshiped all the host of the sky, and served them.

Akazijenga madhabahu ndani ya nyumba ya Bwana, napo ndipo alipopanena Bwana, Katika Yerusalemu nitaliweka jina langu. 2 Wafalme 21:4

He built altars in the house of Yahweh, of which Yahweh said, In Jerusalem will I put my name.

Akajenga madhabahu kwa ajili ya jeshi lote la mbinguni katika behewa mbili za nyumba ya Bwana. 2 Wafalme 21:5

He built altars for all the host of the sky in the two courts of the house of Yahweh.

Akampitisha mwanawe motoni, akatazama bao, akafanya uganga, akajishughulisha na hao wenye pepo wa utambuzi, na wachawi; akafanya mabaya mengi machoni pa Bwana, hata kumkasirisha. 2 Wafalme 21:6

He made his son to pass through the fire, and practiced sorcery, and used enchantments, and dealt with those who had familiar spirits, and with wizards: he worked much evil in the sight of Yahweh, to provoke him to anger.

Akaiweka sanamu ya kuchongwa ya Ashera aliyoifanya ndani ya nyumba, ambayo Bwana alimwambia Daudi, na Sulemani mwanawe, Katika nyumba hii, na katika Yerusalemu, niliouchagua miongoni mwa kabila zote za Israeli, nitaliweka jina langu milele; 2 Wafalme 21:7

He set the engraved image of Asherah, that he had made, in the house of which Yahweh said to David and to Solomon his son, In this house, and in Jerusalem, which I have chosen out of all the tribes of Israel, will I put my name forever;

wala sitawapotosha Israeli miguu watoke katika nchi niliyowapa baba zao; wakiangalia tu na kufanya sawasawa na yote niliyowaamuru, na kwa kuishika torati yote aliyowaamuru mtumishi wangu Musa. 2 Wafalme 21:8

neither will I cause the feet of Israel to wander any more out of the land which I gave their fathers, if only they will observe to do according to all that I have commanded them, and according to all the law that my servant Moses commanded them.

Walakini hawakusikia; naye Manase akawakosesha wafanye mabaya, kuliko mataifa Bwana aliowaharibu mbele za wana wa Israeli. 2 Wafalme 21:9

But they didn't listen: and Manasseh seduced them to do that which is evil more than did the nations whom Yahweh destroyed before the children of Israel.

Bwana akanena kwa watumishi wake manabii, akisema, 2 Wafalme 21:10

Yahweh spoke by his servants the prophets, saying,

Kwa sababu Manase mfalme wa Yuda amefanya machukizo haya, na kutenda vibaya kuliko yote waliyoyatenda Waamori, waliokuwa kabla yake, naye akawakosesha Yuda kwa sanamu zake; 2 Wafalme 21:11

Because Manasseh king of Judah has done these abominations, and has done wickedly above all that the Amorites did, who were before him, and has made Judah also to sin with his idols;

kwa sababu hiyo Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Angalia, naleta mabaya juu ya Yerusalemu na juu ya Yuda, hata kila mtu asikiaye, masikio yake yatawasha yote mawili. 2 Wafalme 21:12

therefore thus says Yahweh, the God of Israel, Behold, I bring such evil on Jerusalem and Judah, that whoever hears of it, both his ears shall tingle.

Nami nitanyosha juu ya Yerusalemu kamba ya Samaria, na timazi ya nyumba ya Ahabu; nami nitaifuta Yerusalemu, kama mtu afutavyo sahani, kuifuta na kuifudikiza. 2 Wafalme 21:13

I will stretch over Jerusalem the line of Samaria, and the plummet of the house of Ahab; and I will wipe Jerusalem as a man wipes a dish, wiping it and turning it upside down.

Nami nitawatupa mabaki ya urithi wangu, na kuwatia mikononi mwa adui zao; nao watakuwa nyara na mateka kwa adui zao wote; 2 Wafalme 21:14

I will cast off the remnant of my inheritance, and deliver them into the hand of their enemies; and they shall become a prey and a spoil to all their enemies;

kwa sababu wametenda yaliyo mabaya machoni pangu, na kunikasirisha, tangu siku ile walipotoka baba zao katika Misri, hata leo hivi. 2 Wafalme 21:15

because they have done that which is evil in my sight, and have provoked me to anger, since the day their fathers came forth out of Egypt, even to this day.

Na Manase akazimwaga damu zisizo na hatia, nyingi sana, hata alipokuwa ameijaza Yerusalemu tangu upande huu hata upande huu; zaidi ya kosa lake alilowakosesha Yuda, kutenda yaliyo mabaya machoni pa Bwana. 2 Wafalme 21:16

Moreover Manasseh shed innocent blood very much, until he had filled Jerusalem from one end to another; besides his sin with which he made Judah to sin, in doing that which was evil in the sight of Yahweh.

Basi mambo yote ya Manase yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, na kosa lake alilolikosa, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? 2 Wafalme 21:17

Now the rest of the acts of Manasseh, and all that he did, and his sin that he sinned, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Judah?

Manase akalala na babaze, akazikwa katika bustani ya nyumba yake mwenyewe, yaani, bustani ya Uza. Na Amoni mwanawe akatawala mahali pake. 2 Wafalme 21:18

Manasseh slept with his fathers, and was buried in the garden of his own house, in the garden of Uzza: and Amon his son reigned in his place.

Amoni alikuwa na umri wa miaka ishirini na miwili alipoanza kutawala; akatawala miaka miwili huko Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Meshulemethi, binti Haruzi wa Yotba. 2 Wafalme 21:19

Amon was twenty-two years old when he began to reign; and he reigned two years in Jerusalem: and his mother's name was Meshullemeth the daughter of Haruz of Jotbah.

Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana, kama Manase babaye alivyofanya. 2 Wafalme 21:20

He did that which was evil in the sight of Yahweh, as did Manasseh his father.

Akaiendea njia yote aliyoiendea baba yake, akazitumikia sanamu alizozitumikia baba yake, akaziabudu. 2 Wafalme 21:21

He walked in all the way that his father walked in, and served the idols that his father served, and worshiped them:

Akamwacha Bwana, Mungu wa babaze, wala hakuiendea njia ya Bwana. 2 Wafalme 21:22

and he forsook Yahweh, the God of his fathers, and didn't walk in the way of Yahweh.

Nao watumishi wa Amoni wakafanya fitina juu yake, wakamwua mfalme ndani ya nyumba yake mwenyewe. 2 Wafalme 21:23

The servants of Amon conspired against him, and put the king to death in his own house.

Lakini watu wa nchi wakawaua wote waliofanya fitina juu yake mfalme Amoni, watu wa nchi wakamfanya Yosia mwanawe awe mfalme mahali pake. 2 Wafalme 21:24

But the people of the land killed all those who had conspired against king Amon; and the people of the land made Josiah his son king in his place.

Basi mambo yote ya Amoni yaliyosalia, aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? 2 Wafalme 21:25

Now the rest of the acts of Amon which he did, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Judah?

Akazikwa kaburini mwake katika bustani ya Uza. Na Yosia mwanawe akatawala mahali pake. 2 Wafalme 21:26

He was buried in his tomb in the garden of Uzza: and Josiah his son reigned in his place.