2 Wafalme 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 1 (Swahili) 2nd Kings 1 (English)

Ikawa, baada ya kufa kwake Ahabu, Moabu wakawaasi Israeli. 2 Wafalme 1:1

Moab rebelled against Israel after the death of Ahab.

Na Ahazia akaanguka katika dirisha la chumba chake orofani, katika Samaria, akaugua; akatuma wajumbe, akawaambia, Enendeni mkaulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, kwamba nitapona ugonjwa huu. 2 Wafalme 1:2

Ahaziah fell down through the lattice in his upper chamber that was in Samaria, and was sick: and he sent messengers, and said to them, Go, inquire of Baal Zebub, the god of Ekron, whether I shall recover of this sickness.

Lakini malaika wa Bwana akamwambia Eliya Mtishbi, Ondoka, uende ukaonane na wale wajumbe wa mfalme wa Samaria, ukawaambie, Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? 2 Wafalme 1:3

But the angel of Yahweh said to Elijah the Tishbite, Arise, go up to meet the messengers of the king of Samaria, and tell them, Is it because there is no God in Israel, that you go to inquire of Baal Zebub, the god of Ekron?

Basi sasa, Bwana asema hivi, Hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa. Eliya akaondoka. 2 Wafalme 1:4

Now therefore thus says Yahweh, You shall not come down from the bed where you are gone up, but shall surely die. Elijah departed.

Wale wajumbe wakarudi, na mfalme akawaambia, Mbona mmerudi? 2 Wafalme 1:5

The messengers returned to him, and he said to them, Why is it that you have returned?

Wakamwambia, Mtu alitokea, akaonana nasi, akatuambia, Enendeni, rudini kwa mfalme yule aliyewatuma, mkamwambie, Bwana asema hivi Je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni? Basi kwa ajili ya hayo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa. 2 Wafalme 1:6

They said to him, There came up a man to meet us, and said to us, Go, turn again to the king who sent you, and tell him, Thus says Yahweh, Is it because there is no God in Israel, that you send to inquire of Baal Zebub, the god of Ekron? therefore you shall not come down from the bed where you are gone up, but shall surely die.

Akawaambia, Je! Mtu yule aliyetokea, akaonana nanyi, akawaambia maneno hayo, alikuwa mtu wa namna gani? 2 Wafalme 1:7

He said to them, What manner of man was he who came up to meet you, and told you these words?

Wakamwambia, Alikuwa amevaa vazi la manyoya, tena amejifunga shuka ya ngozi kiunoni mwake. Naye akasema, Ndiye yule Eliya Mtishbi. 2 Wafalme 1:8

They answered him, He was a hairy man, and girt with a belt of leather about his loins. He said, It is Elijah the Tishbite.

Ndipo mfalme akatuma akida wa askari hamsini pamoja na hamsini wake, wamwendee Eliya. Akamwendea, na tazama, ameketi juu ya kilima. Akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka. 2 Wafalme 1:9

Then [the king] sent to him a captain of fifty with his fifty. He went up to him: and, behold, he was sitting on the top of the hill. He spoke to him, man of God, the king has said, Come down.

Eliya akajibu, akamwambia yule akida wa hamsini, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto ukashuka, ukamteketeza, yeye na hamsini wake. 2 Wafalme 1:10

Elijah answered to the captain of fifty, If I be a man of God, let fire come down from the sky, and consume you and your fifty. Fire came down from the sky, and consumed him and his fifty.

Akatuma tena akida wa hamsini mwingine pamoja na hamsini wake, wamwendee. Akajibu, akamwambia, Ewe mtu wa Mungu, mfalme asema, Shuka upesi. 2 Wafalme 1:11

Again he sent to him another captain of fifty and his fifty. He answered him, man of God, thus has the king said, Come down quickly.

Eliya akajibu, akamwambia, Ikiwa mimi ni mtu wa Mungu, na ushuke moto kutoka mbinguni, ukuteketeze wewe na hamsini wako. Moto wa Mungu ukashuka kutoka mbinguni, ukamteketeza, yeye na hamsini wake. 2 Wafalme 1:12

Elijah answered them, If I be a man of God, let fire come down from the sky, and consume you and your fifty. The fire of God came down from the sky, and consumed him and his fifty.

Tena akatuma akida wa hamsini wa tatu, pamoja na hamsini wake. Yule akida wa hamsini wa tatu akapanda, akaenda akapiga magoti mbele ya Eliya, akamsihi sana, akamwambia, Ee mtu wa Mungu, nakusihi, roho yangu, na roho za watumishi wako hawa hamsini, ziwe na thamani machoni pako. 2 Wafalme 1:13

Again he sent the captain of a third fifty with his fifty. The third captain of fifty went up, and came and fell on his knees before Elijah, and begged him, and said to him, man of God, please let my life, and the life of these fifty your servants, be precious in your sight.

Tazama, moto ulishuka kutoka mbinguni, ukawateketeza wale akida wa hamsini wawili wa kwanza pamoja na hamsini wao; laiti sasa roho yangu na iwe na thamani machoni pako. 2 Wafalme 1:14

Behold, fire came down from the sky, and consumed the two former captains of fifty with their fifties; but now let my life be precious in your sight.

Malaika wa Bwana akamwambia Eliya, Shuka pamoja naye; usimwogope. Akaondoka, akashuka pamoja naye hata kwa mfalme. 2 Wafalme 1:15

The angel of Yahweh said to Elijah, Go down with him: don't be afraid of him. He arose, and went down with him to the king.

Akamwambia, Bwana asema hivi, Kwa kuwa umetuma wajumbe waulize kwa Baal-zebubu, mungu wa Ekroni, je! Ni kwa sababu hapana Mungu katika Israeli, uulize neno lake? Kwa hiyo hutashuka katika kile kitanda ulichokipanda, bali hakika utakufa. 2 Wafalme 1:16

He said to him, Thus says Yahweh, Because you have sent messengers to inquire of Baal Zebub, the god of Ekron, is it because there is no God in Israel to inquire of his word? therefore you shall not come down from the bed where you are gone up, but shall surely die.

Basi akafa, sawasawa na neno la Bwana alilolinena Eliya. Na Yoramu alianza kutawala mahali pake katika mwaka wa pili wa Yehoramu mwana wa Yehoshafati mfalme wa Yuda; kwa kuwa yeye hakuwa na mwana. 2 Wafalme 1:17

So he died according to the word of Yahweh which Elijah had spoken. Jehoram began to reign in his place in the second year of Jehoram the son of Jehoshaphat king of Judah; because he had no son.

Na mambo yote yaliyosalia aliyoyafanya Ahazia, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli? 2 Wafalme 1:18

Now the rest of the acts of Ahaziah which he did, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Israel?