2 Wafalme 15 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 15 (Swahili) 2nd Kings 15 (English)

Katika mwaka wa ishirini na saba wa Yeroboamu mfalme wa Israeli Uzia mwana wa Amazia mfalme wa Yuda alianza kutawala. 2 Wafalme 15:1

In the twenty-seventh year of Jeroboam king of Israel began Azariah son of Amaziah king of Judah to reign.

Alikuwa na umri wa miaka kumi na sita alipoanza kutawala; akatawala miaka hamsini na miwili huko Yerusalemu. Na jina la mamaye aliitwa Yekolia wa Yerusalemu. 2 Wafalme 15:2

Sixteen years old was he when he began to reign; and he reigned fifty-two years in Jerusalem: and his mother's name was Jecoliah of Jerusalem.

Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana, kama yote aliyoyafanya babaye Amazia. 2 Wafalme 15:3

He did that which was right in the eyes of Yahweh, according to all that his father Amaziah had done.

Ila mahali pa juu hapakuondolewa, nao watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu. 2 Wafalme 15:4

However the high places were not taken away: the people still sacrificed and burnt incense in the high places.

Bwana akampiga mfalme, akawa na ukoma hata siku ya kufa kwake, akakaa katika nyumba ya pekee. Na Yothamu mwana wa mfalme alikuwa juu ya nyumba, akiwahukumu watu wa nchi. 2 Wafalme 15:5

Yahweh struck the king, so that he was a leper to the day of his death, and lived in a separate house. Jotham the king's son was over the household, judging the people of the land.

Basi mambo yote ya Uzia yaliyosalia, nayo yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? 2 Wafalme 15:6

Now the rest of the acts of Azariah, and all that he did, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Judah?

Uzia akalala na babaze; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi; na Yothamu mwanawe akatawala mahali pake. 2 Wafalme 15:7

Azariah slept with his fathers; and they buried him with his fathers in the city of David: and Jotham his son reigned in his place.

Katika mwaka wa thelathini na nane wa Uzia mfalme wa Yuda Zekaria mwana wa Yeroboamu akatawala juu ya Israeli katika Samaria miezi sita. 2 Wafalme 15:8

In the thirty-eighth year of Azariah king of Judah did Zechariah the son of Jeroboam reign over Israel in Samaria six months.

Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana kama walivyofanya babaze; hakuyaacha makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli. 2 Wafalme 15:9

He did that which was evil in the sight of Yahweh, as his fathers had done: he didn't depart from the sins of Jeroboam the son of Nebat, with which he made Israel to sin.

Na Shalumu mwana wa Yabeshi akafanya fitina juu yake, akampiga mbele ya watu, akamwua, akatawala mahali pake. 2 Wafalme 15:10

Shallum the son of Jabesh conspired against him, and struck him before the people, and killed him, and reigned in his place.

Basi mambo yote ya Zekaria yaliyosalia, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli. 2 Wafalme 15:11

Now the rest of the acts of Zechariah, behold, they are written in the book of the chronicles of the kings of Israel.

Hilo ndilo neno la Bwana alilomwambia Yehu, akisema, Wana wako watakaa kitini mwa Israeli hata kizazi cha nne. Ikawa vivyo hivyo. 2 Wafalme 15:12

This was the word of Yahweh which he spoke to Jehu, saying, Your sons to the fourth generation shall sit on the throne of Israel. So it came to pass.

Huyo Shalumu mwana wa Yabeshi alianza kutawala katika mwaka wa thelathini na kenda wa Uzia mfalme wa Yuda; akatawala muda wa mwezi mmoja katika Samaria. 2 Wafalme 15:13

Shallum the son of Jabesh began to reign in the nine and thirtieth year of Uzziah king of Judah; and he reigned the space of a month in Samaria.

Menahemu mwana wa Gadi akapanda kutoka Tirza, akaja Samaria, akampiga Shalumu mwana wa Yabeshi huko Samaria, akamwua, akatawala mahali pake. 2 Wafalme 15:14

Menahem the son of Gadi went up from Tirzah, and came to Samaria, and struck Shallum the son of Jabesh in Samaria, and killed him, and reigned in his place.

Basi mambo yote ya Shalumu yaliyosalia, na fitina aliyoifanya, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli. 2 Wafalme 15:15

Now the rest of the acts of Shallum, and his conspiracy which he made, behold, they are written in the book of the chronicles of the kings of Israel.

Ndipo Menahemu akapiga Tifsa, na wote waliokuwamo, na mipaka yake, toka Tirza; kwa sababu hawakumfungulia, kwa hiyo akaupiga; nao wanawake wote waliokuwamo wenye mimba akawapasua. 2 Wafalme 15:16

Then Menahem struck Tiphsah, and all who were therein, and the borders of it, from Tirzah: because they didn't open to him, therefore he struck it; and all the women therein who were with child he ripped up.

Katika mwaka wa thelathini na kenda wa Uzia mfalme wa Yuda Menahemu mwana wa Gadi alianza kutawala juu ya Israeli, akatawala miaka kumi katika Samaria. 2 Wafalme 15:17

In the nine and thirtieth year of Azariah king of Judah began Menahem the son of Gadi to reign over Israel, [and reigned] ten years in Samaria.

Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana; hakuyaacha siku zake zote makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli. 2 Wafalme 15:18

He did that which was evil in the sight of Yahweh: he didn't depart all his days from the sins of Jeroboam the son of Nebat, with which he made Israel to sin.

Akaja Pulu mfalme wa Ashuru juu ya nchi; naye Menahemu akampa Pulu talanta elfu za fedha, ili kwamba mkono wake uwe pamoja naye, na ufalme uwe imara mkononi mwake. 2 Wafalme 15:19

There came against the land Pul the king of Assyria; and Menahem gave Pul one thousand talents of silver, that his hand might be with him to confirm the kingdom in his hand.

Na Menahemu akawatoza Israeli fedha hiyo, yaani, wakuu wote wenye mali, kila mtu shekeli hamsini za fedha, ili ampe huyo mfalme wa Ashuru. Basi mfalme wa Ashuru akarejea, wala hakukaa huko katika nchi. 2 Wafalme 15:20

Menahem exacted the money of Israel, even of all the mighty men of wealth, of each man fifty shekels of silver, to give to the king of Assyria. So the king of Assyria turned back, and didn't stay there in the land.

Basi mambo yote ya Menahemu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli? 2 Wafalme 15:21

Now the rest of the acts of Menahem, and all that he did, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Israel?

Menahemu akalala na babaze; na Pekahia mwanawe akatawala mahali pake. 2 Wafalme 15:22

Menahem slept with his fathers; and Pekahiah his son reigned in his place.

Katika mwaka wa hamsini wa Uzia mfalme wa Yuda Pekahia mwana wa Menahemu alianza kutawala juu ya Israeli hatika Samaria; akatawala miaka miwili. 2 Wafalme 15:23

In the fiftieth year of Azariah king of Judah Pekahiah the son of Menahem began to reign over Israel in Samaria, [and reigned] two years.

Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana; hakuyaacha makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli. 2 Wafalme 15:24

He did that which was evil in the sight of Yahweh: he didn't depart from the sins of Jeroboam the son of Nebat, with which he made Israel to sin.

Na Peka mwana wa Remalia, jemadari wake, akamfanyia fitina, akampiga huko Samaria, katika ngome ya nyumba ya mfalme, pamoja na Argobu na Arie; na pamoja naye walikuwako watu hamsini wa Wagileadi. Akamwua, akatawala mahali pake. 2 Wafalme 15:25

Pekah the son of Remaliah, his captain, conspired against him, and struck him in Samaria, in the castle of the king's house, with Argob and Arieh; and with him were fifty men of the Gileadites: and he killed him, and reigned in his place.

Basi mambo yote ya Pekahia yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli. 2 Wafalme 15:26

Now the rest of the acts of Pekahiah, and all that he did, behold, they are written in the book of the chronicles of the kings of Israel.

Katika mwaka wa hamsini na mbili wa Uzia mfalme wa Yuda Peka mwana wa Remalia alianza kutawala juu ya Israeli katika Samaria; akatawala miaka ishirini. 2 Wafalme 15:27

In the two and fiftieth year of Azariah king of Judah Pekah the son of Remaliah began to reign over Israel in Samaria, [and reigned] twenty years.

Akafanya yaliyo maovu machoni pa Bwana; hakuyaacha makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli. 2 Wafalme 15:28

He did that which was evil in the sight of Yahweh: he didn't depart from the sins of Jeroboam the son of Nebat, with which he made Israel to sin.

Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru. 2 Wafalme 15:29

In the days of Pekah king of Israel came Tiglath Pileser king of Assyria, and took Ijon, and Abel Beth Maacah, and Janoah, and Kedesh, and Hazor, and Gilead, and Galilee, all the land of Naphtali; and he carried them captive to Assyria.

Na Hoshea mwana wa Ela akafanya fitina juu ya Peka mwana wa Remalia, akampiga, akamwua, akatawala mahali pake, katika mwaka wa ishirini wa Yothamu mwana wa Uzia. 2 Wafalme 15:30

Hoshea the son of Elah made a conspiracy against Pekah the son of Remaliah, and struck him, and killed him, and reigned in his place, in the twentieth year of Jotham the son of Uzziah.

Basi mambo yote ya Peka yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, tazama, yameandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Israeli. 2 Wafalme 15:31

Now the rest of the acts of Pekah, and all that he did, behold, they are written in the book of the chronicles of the kings of Israel.

Katika mwaka wa pili wa Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli Yothamu mwana wa Uzia mfalme wa Yuda alianza kutawala. 2 Wafalme 15:32

In the second year of Pekah the son of Remaliah king of Israel began Jotham the son of Uzziah king of Judah to reign.

Alikuwa na umri wa miaka ishirini na mitano alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Yerusha binti Sadoki. 2 Wafalme 15:33

He was twenty-five years old when he began to reign; and he reigned sixteen years in Jerusalem: and his mother's name was Jerusha the daughter of Zadok.

Akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana; akafanya kama yote aliyoyafanya Uzia baba yake. 2 Wafalme 15:34

He did that which was right in the eyes of Yahweh; he did according to all that his father Uzziah had done.

Ila mahali pa juu hapakuondolewa; watu walikuwa wakitoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu. Ndiye aliyelijenga lango la juu la nyumba ya Bwana. 2 Wafalme 15:35

However the high places were not taken away: the people still sacrificed and burned incense in the high places. He built the upper gate of the house of Yahweh.

Basi mambo yote ya Yothamu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? 2 Wafalme 15:36

Now the rest of the acts of Jotham, and all that he did, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Judah?

Zamani hizo akaanza Bwana kumtuma juu ya Yuda Resini mfalme wa Shamu, na Peka mwana wa Remalia. 2 Wafalme 15:37

In those days Yahweh began to send against Judah Rezin the king of Syria, and Pekah the son of Remaliah.

Yothamu akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi baba yake. Na Ahazi mwanawe akatawala mahali pake. 2 Wafalme 15:38

Jotham slept with his fathers, and was buried with his fathers in the city of David his father: and Ahaz his son reigned in his place.