2 Wafalme 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 16 (Swahili) 2nd Kings 16 (English)

Katika mwaka wa kumi na saba wa Peka mwana wa Remalia Ahazi mwana wa Yothamu mfalme wa Yuda alianza kutawala. 2 Wafalme 16:1

In the seventeenth year of Pekah the son of Remaliah Ahaz the son of Jotham king of Judah began to reign.

Alikuwa na umri wa miaka ishirini alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na sita katika Yerusalemu; wala hakufanya mema machoni pa Bwana Mungu wake, kama Daudi babaye. 2 Wafalme 16:2

Twenty years old was Ahaz when he began to reign; and he reigned sixteen years in Jerusalem: and he didn't do that which was right in the eyes of Yahweh his God, like David his father.

Lakini aliiendea njia ya wafalme wa Israeli, hata akampitisha mwanawe motoni, sawasawa na machukizo ya mataifa Bwana aliowafukuza mbele ya wana wa Israeli. 2 Wafalme 16:3

But he walked in the way of the kings of Israel, yes, and made his son to pass through the fire, according to the abominations of the nations, whom Yahweh cast out from before the children of Israel.

Kisha akatoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu, na juu ya vilima, na chini ya kila mti mbichi. 2 Wafalme 16:4

He sacrificed and burnt incense in the high places, and on the hills, and under every green tree.

Hapo ndipo akakwea Resini mfalme wa Shamu pamoja na Peka mwana wa Remalia mfalme wa Israeli juu ya Yerusalemu ili wapigane; wakamhusuru Ahazi, ila hawakuweza kumshinda. 2 Wafalme 16:5

Then Rezin king of Syria and Pekah son of Remaliah king of Israel came up to Jerusalem to war: and they besieged Ahaz, but could not overcome him.

Wakati huo Resini mfalme wa Shamu akawarudishia Washami Elathi, akawafukuza Wayahudi kutoka Elathi; nao Washami wakaja Elathi, wakakaa humo hata leo. 2 Wafalme 16:6

At that time Rezin king of Syria recovered Elath to Syria, and drove the Jews from Elath; and the Syrians came to Elath, and lived there, to this day.

Basi Ahazi akatuma wajumbe kwa Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akasema, Mimi ni mtumishi, tena mwana wako; kwea, ukaniokoe mkononi mwa mfalme wa Shamu, na mkononi mwa mfalme wa Israeli, walioniinukia. 2 Wafalme 16:7

So Ahaz sent messengers to Tiglath Pileser king of Assyria, saying, I am your servant and your son: come up, and save me out of the hand of the king of Syria, and out of the hand of the king of Israel, who rise up against me.

Ahazi akatwaa fedha na dhahabu iliyoonekana katika nyumba ya Bwana, na katika hazina za nyumba ya mfalme, akazipeleka kwa mfalme wa Ashuru kuwa zawadi. 2 Wafalme 16:8

Ahaz took the silver and gold that was found in the house of Yahweh, and in the treasures of the king's house, and sent it for a present to the king of Assyria.

Na huyo mfalme wa Ashuru akamsikia; mfalme wa Ashuru akapanda juu ya Dameski, akautwaa, akawahamisha watu wake mateka mpaka Kiri, akamwua Resini. 2 Wafalme 16:9

The king of Assyria listened to him; and the king of Assyria went up against Damascus, and took it, and carried [the people of] it captive to Kir, and killed Rezin.

Naye mfalme Ahazi akaenda Dameski ili aonane na Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akaiona ile madhabahu iliyokuwako Dameski. Mfalme Ahazi akamletea Uria kuhani namna yake ile madhabahu, na cheo chake, kama ilivyokuwa kazi yake yote. 2 Wafalme 16:10

King Ahaz went to Damascus to meet Tiglath Pileser king of Assyria, and saw the altar that was at Damascus; and king Ahaz sent to Urijah the priest the fashion of the altar, and the pattern of it, according to all the workmanship of it.

Naye Uria kuhani akajenga madhabahu; sawasawa na yote aliyomletea mfalme Ahazi kutoka Dameski; ndivyo alivyoifanya Uria kuhani iwe tayari atakaporudi mfalme Ahazi kutoka Dameski. 2 Wafalme 16:11

Urijah the priest built an altar: according to all that king Ahaz had sent from Damascus, so did Urijah the priest make it against the coming of king Ahaz from Damascus.

Na mfalme aliporudi kutoka Dameski, mfalme akaiona ile madhabahu; mfalme akakaribia madhabahuni, na kutoa sadaka juu yake. 2 Wafalme 16:12

When the king was come from Damascus, the king saw the altar: and the king drew near to the altar, and offered thereon.

Akaiteketeza sadaka yake ya kuteketezwa, na sadaka yake ya unga, akamimina sadaka yake ya kinywaji, akanyunyiza damu ya sadaka zake za amani, juu ya madhabahu. 2 Wafalme 16:13

He burnt his burnt offering and his meal-offering, and poured his drink-offering, and sprinkled the blood of his peace-offerings, on the altar.

Na ile madhabahu ya shaba iliyokuwako mbele za Bwana, akaileta kutoka mbele ya nyumba, kutoka kati ya madhabahu yake mwenyewe na nyumba ya Bwana, akaiweka upande wa kaskazini wa madhabahu yake. 2 Wafalme 16:14

The brazen altar, which was before Yahweh, he brought from the forefront of the house, from between his altar and the house of Yahweh, and put it on the north side of his altar.

Mfalme Ahazi akamwamuru Uria kuhani, akisema, Juu ya madhabahu hiyo kubwa uiteketeze sadaka ya kuteketezwa ya asubuhi, na sadaka ya unga ya jioni, na sadaka ya mfalme ya kuteketezwa, na sadaka yake ya unga, pamoja na sadaka ya kuteketezwa ya watu wote wa nchi, na sadaka yao ya unga, na sadaka zao za kinywaji; ukanyunyize juu yake damu yote ya sadaka ya kuteketezwa, na damu yote ya dhabihu; bali madhabahu ya shaba itakuwa kwangu mimi ili niiulizie. 2 Wafalme 16:15

King Ahaz commanded Urijah the priest, saying, On the great altar burn the morning burnt offering, and the evening meal-offering, and the king's burnt offering, and his meal-offering, with the burnt offering of all the people of the land, and their meal-offering, and their drink-offerings; and sprinkle on it all the blood of the burnt offering, and all the blood of the sacrifice: but the brazen altar shall be for me to inquire by.

Akafanya hivyo Uria kuhani, sawasawa na yote aliyoyaamuru mfalme Ahazi. 2 Wafalme 16:16

Thus did Urijah the priest, according to all that king Ahaz commanded.

Mfalme Ahazi akakata papi za matako, akaliondoa lile birika juu yake; akaitelemsha ile bahari itoke juu ya ng'ombe za shaba zilizokuwa chini yake, akaiweka juu ya sakafu ya mawe. 2 Wafalme 16:17

King Ahaz cut off the panels of the bases, and removed the basin from off them, and took down the sea from off the brazen oxen that were under it, and put it on a pavement of stone.

Na ukumbi wa sabato walioujenga katika hiyo nyumba, na mahali pa kuingia pake mfalme palipokuwapo nje, akavigeuza kuikabili nyumba ya Bwana, kwa sababu ya mfalme wa Ashuru. 2 Wafalme 16:18

The covered way for the Sabbath that they had built in the house, and the king's entry outside, turned he to the house of Yahweh, because of the king of Assyria.

Basi mambo yote ya Ahazi yaliyosalia, aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? 2 Wafalme 16:19

Now the rest of the acts of Ahaz which he did, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Judah?

Ahazi akalala na babaze, akazikwa pamoja na babaze katika mji wa Daudi; na Hezekia mwanawe akatawala mahali pake.

2 Wafalme 16:20

Ahaz slept with his fathers, and was buried with his fathers in the city of David: and Hezekiah his son reigned in his place.