2 Wafalme 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 12 (Swahili) 2nd Kings 12 (English)

Katika mwaka wa saba wa Yehu, Yoashi alianza kutawala; akatawala miaka arobaini huko Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Sibia wa Beer-sheba. 2 Wafalme 12:1

In the seventh year of Jehu began Jehoash to reign; and he reigned forty years in Jerusalem: and his mother's name was Zibiah of Beersheba.

Yoashi akafanya yaliyo mema machoni pa Bwana siku zake zote Yehoyada kuhani alizomfundisha. 2 Wafalme 12:2

Jehoash did that which was right in the eyes of Yahweh all his days in which Jehoiada the priest instructed him.

Ila mahali pa juu hapakuondolewa; watu wakaendelea kutoa sadaka na kufukiza uvumba katika mahali pa juu. 2 Wafalme 12:3

However the high places were not taken away; the people still sacrificed and burnt incense in the high places.

Yoashi akawaambia makuhani, Fedha yote ya vitu vitakatifu iliyoletwa nyumbani mwa Bwana, fedha ya matumizi, fedha ya watu kadiri alivyoandikiwa kila mtu, na fedha yote iliyoletwa kama mtu ye yote aonavyo moyoni mwake kuileta nyumbani mwa Bwana, 2 Wafalme 12:4

Jehoash said to the priests, All the money of the holy things that is brought into the house of Yahweh, in current money, the money of the persons for whom each man is rated, and all the money that it comes into any man's heart to bring into the house of Yahweh,

makuhani na waitwae, kila mtu kwa hao awajuao; nao watatengeneza palipobomoka nyumbani, kila mahali palipoonekana pamebomoka. 2 Wafalme 12:5

let the priests take it to them, every man from his acquaintance; and they shall repair the breaches of the house, wherever any breach shall be found.

Lakini ikawa, mwaka wa ishirini na tatu wa mfalme Yoashi, makuhani walikuwa hawajatengeneza mabomoko ya nyumba. 2 Wafalme 12:6

But it was so, that in the three and twentieth year of king Jehoash the priests had not repaired the breaches of the house.

Ndipo mfalme Yoashi akamwita Yehoyada kuhani, na makuhani wengine, akawauliza, Mbona hamtengenezi mabomoko ya nyumba? Basi sasa msipokee tena fedha kwa hao mwajuao, lakini itoeni kwa ajili ya mabomoko ya nyumba. 2 Wafalme 12:7

Then king Jehoash called for Jehoiada the priest, and for the [other] priests, and said to them, Why don't you repair the breaches of the house? now therefore take no [more] money from your acquaintance, but deliver it for the breaches of the house.

Nao makuhani wakakubali kwamba wasipokee fedha kwa watu, wala wasitengeneze mabomoko ya nyumba. 2 Wafalme 12:8

The priests consented that they should take no [more] money from the people, neither repair the breaches of the house.

Lakini Yehoyada kuhani akatwaa kasha, akatoboa tundu katika kifuniko chake, akaliweka karibu na madhabahu, upande wa kuume mtu aingiapo nyumbani mwa Bwana; na makuhani, waliolinda mlangoni, wakatia ndani yake fedha yote iliyoletwa nyumbani mwa Bwana. 2 Wafalme 12:9

But Jehoiada the priest took a chest, and bored a hole in the lid of it, and set it beside the altar, on the right side as one comes into the house of Yahweh: and the priests who kept the threshold put therein all the money that was brought into the house of Yahweh.

Ikawa, walipoona ya kuwa fedha nyingi imo kashani, karani wa mfalme akapanda na kuhani mkuu, wakaifunga mifukoni, wakaihesabu fedha iliyoonekana nyumbani mwa Bwana. 2 Wafalme 12:10

It was so, when they saw that there was much money in the chest, that the king's scribe and the high priest came up, and they put up in bags and counted the money that was found in the house of Yahweh.

Na fedha iliyopimwa wakawapa mikononi wale waliofanya kazi, walioisimamia nyumba ya Bwana; na hao wakawatolea maseremala na wajenzi walioifanya kazi katika nyumba ya Bwana, 2 Wafalme 12:11

They gave the money that was weighed out into the hands of those who did the work, who had the oversight of the house of Yahweh: and they paid it out to the carpenters and the builders, who worked on the house of Yahweh,

na hao waashi, na wakata mawe, tena kununua miti na mawe ya kuchongwa, ili kuyatengeneza mabomoko ya nyumba ya Bwana, tena kwa gharama zote za kuitengeneza nyumba. 2 Wafalme 12:12

and to the masons and the stone cutters, and for buying timber and hewn stone to repair the breaches of the house of Yahweh, and for all that was laid out for the house to repair it.

Lakini havikufanywa kwa nyumba ya Bwana vikombe vya fedha, wala makasi, wala mabakuli, wala panda, wala vyombo vyo vyote vya dhahabu, wala vyombo vya fedha, kwa hiyo fedha iliyoletwa nyumbani mwa Bwana; 2 Wafalme 12:13

But there were not made for the house of Yahweh cups of silver, snuffers, basins, trumpets, any vessels of gold, or vessels of silver, of the money that was brought into the house of Yahweh;

kwa sababu hiyo fedha waliwapa watenda kazi, wakaitengeneza kwayo nyumba ya Bwana. 2 Wafalme 12:14

for they gave that to those who did the work, and repaired therewith the house of Yahweh.

Walakini hawakufanya hesabu na hao watu, waliokabidhiwa fedha hiyo ili wawape watenda kazi; kwa kuwa walitenda kwa uaminifu. 2 Wafalme 12:15

Moreover they didn't demand an accounting from the men into whose hand they delivered the money to give to those who did the work; for they dealt faithfully.

Lakini fedha ya matoleo ya kosa, na fedha ya matoleo ya dhambi, haikuletwa nyumbani mwa Bwana; hiyo ilikuwa ya makuhani wenyewe. 2 Wafalme 12:16

The money for the trespass-offerings, and the money for the sin-offerings, was not brought into the house of Yahweh: it was the priests'.

Ndipo akakwea Hazaeli mfalme wa Shamu akapigana na Gathi, akautwaa; Hazaeli akaelekeza uso ili akwee kwenda Yerusalemu. 2 Wafalme 12:17

Then Hazael king of Syria went up, and fought against Gath, and took it; and Hazael set his face to go up to Jerusalem.

Yoashi mfalme wa Yuda akavitwaa vyote alivyoviweka wakfu Yehoshafati, na Yehoramu, na Ahazia, baba zake, wafalme wa Yuda, navyo vyote alivyoweka wakfu mwenyewe, na dhahabu yote iliyoonekana katika hazina za nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme, akamletea Hazaeli mfalme wa Shamu; basi akaenda zake kutoka Yerusalemu. 2 Wafalme 12:18

Jehoash king of Judah took all the holy things that Jehoshaphat and Jehoram and Ahaziah, his fathers, kings of Judah, had dedicated, and his own holy things, and all the gold that was found in the treasures of the house of Yahweh, and of the king's house, and sent it to Hazael king of Syria: and he went away from Jerusalem.

Basi mambo yote ya Yoashi yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda? 2 Wafalme 12:19

Now the rest of the acts of Joash, and all that he did, aren't they written in the book of the chronicles of the kings of Judah?

Nao watumishi wake wakaondoka, wakafanya fitina, wakamwua Yoashi katika nyumba ya Milo, hapo panaposhukia Sila. 2 Wafalme 12:20

His servants arose, and made a conspiracy, and struck Joash at the house of Millo, [on the way] that goes down to Silla.

Kwa maana Yozakari mwana wa Shimeathi, na Yehozabadi mwana wa Shomeri, watumishi wake, wakampiga, naye akafa; wakamzika pamoja na babaze mjini mwa Daudi. Na Amazia mwanawe akatawala mahali pake. 2 Wafalme 12:21

For Jozacar the son of Shimeath, and Jehozabad the son of Shomer, his servants, struck him, and he died; and they buried him with his fathers in the city of David: and Amaziah his son reigned in his place.