2 Wafalme 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wafalme 3 (Swahili) 2nd Kings 3 (English)

Basi Yoramu mwana wa Ahabu alianza kutawala juu ya Israeli huko Samaria katika mwaka wa kumi na nane wa Yehoshafati mfalme wa Yuda ,akatawala miaka kumi na miwili. 2 Wafalme 3:1

Now Jehoram the son of Ahab began to reign over Israel in Samaria in the eighteenth year of Jehoshaphat king of Judah, and reigned twelve years.

Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana; ila si kama baba yake na kama mama yake; maana akaiondoa ile nguzo ya Baali aliyoifanya baba yake. 2 Wafalme 3:2

He did that which was evil in the sight of Yahweh, but not like his father, and like his mother; for he put away the pillar of Baal that his father had made.

Pamoja na hayo alishikamana na dhambi za Yeroboamu mwana wa Nebati, ambazo kwa hizo aliwakosesha Israeli; wala hakuziacha. 2 Wafalme 3:3

Nevertheless he cleaved to the sins of Jeroboam the son of Nebat, with which he made Israel to sin; he didn't depart from it.

Basi Mesha, mfalme wa Moabu, alikuwa mfuga kondoo; naye alikuwa akimlipa mfalme wa Israeli sufu ya wana-kondoo elfu mia, na ya kondoo waume elfu mia. 2 Wafalme 3:4

Now Mesha king of Moab was a sheep-master; and he rendered to the king of Israel the wool of one hundred thousand lambs, and of one hundred thousand rams.

Lakini ikawa, Ahabu alipokufa, mfalme wa Moabu akamwasi mfalme wa Israeli. 2 Wafalme 3:5

But it happened, when Ahab was dead, that the king of Moab rebelled against the king of Israel.

Akatoka wakati ule ule mfalme Yoramu katika Samaria, akawahesabu Israeli wote. 2 Wafalme 3:6

King Jehoram went out of Samaria at that time, and mustered all Israel.

Akaenda akatuma kwa Yehoshafati mfalme wa Yuda, akasema, Mfalme wa Moabu ameniasi; je! Utakwenda pamoja nami tupigane na Moabu? Akasema, Nitakwenda; mimi ni kama wewe, watu wangu ni kama watu wako, farasi zangu ni kama farasi zako. 2 Wafalme 3:7

He went and sent to Jehoshaphat the king of Judah, saying, The king of Moab has rebelled against me: will you go with me against Moab to battle? He said, I will go up: I am as you are, my people as your people, my horses as your horses.

Akauliza, Njia ipi tuiendee? Akajibu, Njia ya jangwa la Edomu. 2 Wafalme 3:8

He said, Which way shall we go up? He answered, The way of the wilderness of Edom.

Basi mfalme wa Israeli akaenda, na mfalme wa Yuda, na mfalme wa Edomu; wakazunguka mwendo wa siku saba; wala hapakuwa na maji kwa jeshi, wala kwa wanyama waliowafuata. 2 Wafalme 3:9

So the king of Israel went, and the king of Judah, and the king of Edom; and they made a circuit of seven days' journey: and there was no water for the host, nor for the animals that followed them.

Mfalme wa Israeli akasema, Ole wetu! Kwani Bwana amewakutanisha hawa wafalme watatu, awaue mkononi mwa Moabu. 2 Wafalme 3:10

The king of Israel said, Alas! for Yahweh has called these three kings together to deliver them into the hand of Moab.

Lakini Yehoshafati akasema, Je! Hapana hapa nabii wa Bwana, ili tumwulize Bwana kwa yeye? Akajibu mtumishi mmoja wa mfalme wa Israeli, akasema, Yupo hapa Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akimimina maji juu ya mikono yake Eliya. 2 Wafalme 3:11

But Jehoshaphat said, Isn't there here a prophet of Yahweh, that we may inquire of Yahweh by him? One of the king of Israel's servants answered, Elisha the son of Shaphat is here, who poured water on the hands of Elijah.

Yehoshafati akasema, Neno la Bwana analo huyu. Basi mfalme wa Israeli, na Yehoshafati, na mfalme wa Edomu, wakamshukia. 2 Wafalme 3:12

Jehoshaphat said, The word of Yahweh is with him. So the king of Israel and Jehoshaphat and the king of Edom went down to him.

Elisha akamwambia mfalme wa Israeli, Nina nini mimi nawe? Uende kwa manabii wa babayo, na manabii wa mamayo. Mfalme wa Israeli akamwambia, La, sivyo; kwa kuwa Bwana amewakutanisha hawa wafalme watatu, awaue mkononi mwa Moabu. 2 Wafalme 3:13

Elisha said to the king of Israel, What have I to do with you? get you to the prophets of your father, and to the prophets of your mother. The king of Israel said to him, No; for Yahweh has called these three kings together to deliver them into the hand of Moab.

Elisha akasema, Kama Bwana wa majeshi aishivyo, ambaye nimesimama mbele zake, kama singemwangalia uso wake Yehoshafati mfalme wa Yuda, singekutazama, wala kuonana nawe. 2 Wafalme 3:14

Elisha said, As Yahweh of Hosts lives, before whom I stand, surely, were it not that I regard the presence of Jehoshaphat the king of Judah, I would not look toward you, nor see you.

Ila sasa niletee mpiga kinanda. Ikawa, mpiga kinanda alipokipiga, mkono wa Bwana ukamjia juu yake. 2 Wafalme 3:15

But now bring me a minstrel. It happened, when the minstrel played, that the hand of Yahweh came on him.

Akasema, Bwana asema hivi, Fanyeni bonde hili lijae mahandaki. 2 Wafalme 3:16

He said, Thus says Yahweh, Make this valley full of trenches.

Kwa kuwa Bwana asema hivi, Hamutauona upepo, wala hamtaiona mvua, ila bonde hilo litajaa maji; nanyi mtakunywa, ninyi, na ng'ombe zenu, na wanyama wenu. 2 Wafalme 3:17

For thus says Yahweh, You shall not see wind, neither shall you see rain; yet that valley shall be filled with water, and you shall drink, both you and your cattle and your animals.

Na jambo hili ni jepesi machoni pa Bwana; pia atawatia Wamoabi mikononi mwenu. 2 Wafalme 3:18

This is but a light thing in the sight of Yahweh: he will also deliver the Moabites into your hand.

Nanyi mtapiga kila mji wenye boma, na kila mji ulio mzuri, na kila mti mwema mtaukata, na chemchemi zote za maji mtaziziba, na kila mahali palipo pema mtapaharibu kwa mawe. 2 Wafalme 3:19

You shall strike every fortified city, and every choice city, and shall fell every good tree, and stop all springs of water, and mar every good piece of land with stones.

Ikawa asubuhi, wakati wa kutoa sadaka ya unga, tazama, maji yakaja kwa njia ya Edomu, hata nchi ikajaa maji. 2 Wafalme 3:20

It happened in the morning, about the time of offering the offering, that behold, there came water by the way of Edom, and the country was filled with water.

Basi Wamoabi wote waliposikia ya kuwa wafalme hao wamekwea ili kupigana nao, walijikusanya pamoja, wote wawezao kuvaa silaha, na wenye umri zaidi, wakasimama mpakani. 2 Wafalme 3:21

Now when all the Moabites heard that the kings had come up to fight against them, they gathered themselves together, all who were able to put on armor, and upward, and stood on the border.

Wakaamka asubuhi na mapema, na hilo jua likameta-meta juu ya maji, na Wamoabi wakayaona yale maji yaliyowaelekea kuwa ni mekundu kama damu. 2 Wafalme 3:22

They rose up early in the morning, and the sun shone on the water, and the Moabites saw the water over against them as red as blood:

Wakasema, Ndiyo damu hii; bila shaka hao wafalme wameharibika, wamepigana kila mtu na mwenziwe; basi sasa, enyi Wamoabi, nyara hizo! 2 Wafalme 3:23

and they said, This is blood; the kings are surely destroyed, and they have struck each man his fellow: now therefore, Moab, to the spoil.

Hata walipokuja matuoni kwa Israeli, Waisraeli wakainuka wakawapiga Wamoabi, hata wakakimbia mbele yao; wakaendelea wakiwapiga-piga Wamoabi hata kwao. 2 Wafalme 3:24

When they came to the camp of Israel, the Israelites rose up and struck the Moabites, so that they fled before them; and they went forward into the land smiting the Moabites.

Wakaibomoa ile miji; wakatupa katika kila mahali palipo pema kila mtu jiwe lake, wakapajaza; wakaziziba chemchemi zote za maji, wakaikata miti yote iliyo mizuri; mpaka katika Kir-haresethi tu wakayasaza mawe yake; ila wenye kombeo wakauzunguka wakaupiga. 2 Wafalme 3:25

They beat down the cities; and on every good piece of land they cast every man his stone, and filled it; and they stopped all the springs of water, and felled all the good trees, until in Kir Hareseth [only] they left the stones of it; however the men armed with slings went about it, and struck it.

Naye mfalme wa Moabu alipoona ya kwamba ameshindwa vitani, alitwaa pamoja naye watu mia saba wenye kufuta panga ili wapenye hata kwa mfalme wa Edomu; wala hawakudiriki. 2 Wafalme 3:26

When the king of Moab saw that the battle was too severe for him, he took with him seven hundred men who drew sword, to break through to the king of Edom; but they could not.

Ndipo akamtwaa mwanawe wa kwanza, yeye ambaye angetawala mahali pake, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa juu ya ukuta. Kukawa hasira kuu juu ya Israeli; basi wakatoka kwake, wakarudi kwenda nchi yao wenyewe. 2 Wafalme 3:27

Then he took his eldest son who would have reigned in his place, and offered him for a burnt offering on the wall. There was great wrath against Israel: and they departed from him, and returned to their own land.