Sifa Lyrics

Unabaki Kuitwa Mungu by Upendo Nkone cover art

Upendo Nkone - Unabaki Kuitwa Mungu Lyrics

Artist:
Upendo Nkone

Lyrics

Unabaki kuitwa Mungu
Hata kama ulinihuzunisha
Unabaki kuitwa Mungu
Hata kama haujajibu maswali


Unabaki kuitwa Mungu
Hata kama pito langu ni nzito
Unabaki kuitwa Mungu
Maana wewe ni Mungu mkuu


Umesema nikutafute sana baba
Ndipo nitakapo kuona bwana wangu
Nimefanya hivyo kwa miaka mingi sana
Lakini bado uko kimya


Ona watu wameanza kunicheka sana
Aibu hii nijifiche wapi Yesu wangu
Na umesema hautaniaibisha  wee
Nitendee Yesu nisiaibike


Unabaki kuitwa Mungu
Hata kama ulinihuzunisha
Unabaki kuitwa Mungu
Hata kama haujajibu maswali


Unabaki kuitwa Mungu
Hata kama pito langu ni nzito
Unabaki kuitwa Mungu
Maana wewe ni Mungu mkuu


Safari ya wokovu sio mchezo
Tunakutana na mambo mazito sana
Ambayo mtu kuyategemea
Na tena yanaumiza moyo


Lakini Mungu yeye ni mwaminifu sana
Anafanya mlango wa kutokea
Jitie moyo katika bwana
Maana faraja ya kweli yatoka kwake


Unabaki kuitwa Mungu
Hata kama ulinihuzunisha
Unabaki kuitwa Mungu
Hata kama haujajibu maswali


Unabaki kuitwa Mungu
Hata kama pito langu ni nzito
Unabaki kuitwa Mungu
Maana wewe ni Mungu mkuu


Video