Sifa Lyrics

Napenda Niwe Karibu Na Wewe by Emmanuel Mgogo cover art

Emmanuel Mgogo - Napenda Niwe Karibu Na Wewe Lyrics

Artist:
Emmanuel Mgogo

Lyrics

Mimi napenda niwe karibu na wewe
Bwana niwe na wewe
Univute niwe karibu na wewe
Bwana mimi napendaga


Mimi napenda niwe karibu na wewe
Bwana niwe na wewe
Univute niwe karibu na wewe
Bwana mimi napendaga 


Maana hapa nilipo
Nipo moyoni na kiu zaidi
Nina kiu na wewe, kuwa karibu na wewe
Napenda ooh, ninapendaga


Maana hapa nilipo
Sijaridhika nina kiu zaidi
Nina kiu na wewe, kuwa karibu na wewe
Oooh ninapendaga


Nina haja na wewe bwana
Natamani ukae nami
Sioni mwingine bwana
Sijapata mwingine


Ila ni wewe wa kunifaa mimi
Wa kunitunza ila ni wewe
Tabibu wa karibu bwana
 
Usinipite pembeni bwana
Sina mwingine wa kunihurumia
Pale ninapo jeruhiwa
Na wanyang'anyi uwe karibu


We ni msamaria mwema utanihudumia
Utanifunga majeraha na kunifariji
Unionyeshe pendo lako
Maana wanipenda


Unionyeshe pendo lako
Maana wanipenda


Sioni la kunifurahisha
Nikiwa mbali na uwepo wako
Kama mti unang'olewa udongoni
Nitasinya na kudhoofika


Ninaomba univute niwe karibu nawe
Kama mti uliopandwa kando kando ya maji
Uzao wa matunda mazuri
Wala majani yake hayanyauki


Kila nitendalo nifanikiwe
Bwana naomba


Wewe ni maji ya uzima
Wewe ni maji yaliyo hai
Kisima cha uzima
Na upendo


Kama hayana na porini
Ayatamanivyo maji
Ndivyo nafsi yangu yakutamani wewe
Fanya hima usichelewe


Univute karibu nawe
Niwe na wewe


Mimi napenda niwe karibu na wewe
Bwana niwe na wewe
Univute niwe karibu na wewe
Bwana mimi napendaga


Mimi napenda niwe karibu na wewe
Bwana niwe na wewe
Univute niwe karibu na wewe
Bwana mimi napendaga 


Maana hapa nilipo
Nipo moyoni na kiu zaidi
Nina kiu na wewe, kuwa karibu na wewe
Napenda ooh, ninapendaga


Maana hapa nilipo
Sijaridhika nina kiu zaidi
Nina kiu na wewe, kuwa karibu na wewe
Oooh ninapendaga


Kukaa na wewe 
Ni shauku pekee 
Ya moyo wangu bwana aah
Hapa nilipo sijaridhika


Natamani nipandishwe juu
Univute karibu na wewe
Karibu zaidi ya jana
Uwe nuru uniangazie


Pendo lako kama maji
Nizame kwenye kisima 
Cha uwepo wako 


Nimesoma katika neno lako Zaburi
Umesema ooh
Aketiye mahali pake pa siri
Palipo juu 


Huyo atakaa katika uvuli wake mwenyezi
Ataokolewa na mitego ya adui
Silaha zote na mishale
Haitofanikiwa


Silaha zote na mishale
Haitofanikiwa


Nichue uniweke hapo bwana
Hili ni ombi la moyo wangu
Niketishe kwenye uwepo wako
Tuketishe kwenye uwepo wako


Usiniache gizani bwana
Peke yangu siwezi
Kaa nami, karibu nami
Ndani yangu nami ndani yako


Univute karibu nawe
Mikononi mwako niwe salama
Univute karibu nawe
Niwe na wewe bwana


Mimi napenda niwe karibu na wewe
Bwana niwe na wewe
Univute niwe karibu na wewe
Bwana mimi napendaga


Mimi napenda niwe karibu na wewe
Bwana niwe na wewe
Univute niwe karibu na wewe
Bwana mimi napendaga 


Maana hapa nilipo
Nipo moyoni na kiu zaidi
Nina kiu na wewe, kuwa karibu na wewe
Napenda ooh, ninapendaga


Maana hapa nilipo
Sijaridhika nina kiu zaidi
Nina kiu na wewe, kuwa karibu na wewe
Oooh ninapendaga


Video