Uso Wangu

Uso Wangu Lyrics

Uso wangu utakwenda nawewe na wewe 
Na mimi nitakupa raha raha 
Uso wangu utakwenda nawewe na wewe 
Na mimi nitakupa raha raha ah  .

Mwenyewe siwezi siwezi bila wewe 
Mwenyewe siwezi siwezi bila wewe 
Siwezi siwezi bila wewe siwezi  .

Kuna mahali natamani 
Moyo wangu watamani nikae hapo 
Niwe hapo daima   .

Mahali hapo kuna raha 
Furaha na utoshelevu 
salama amani vinatawala  .

Tena nasikia sauti ikiniambia mwanangu 
Mahali hapo ni nyumbani ulipoumbwa ukae  .

Mahali hapo ni pale penye uwepo wa Mungu 
Penye uso wa Mungu Baba  .

Mwanadamu Bila Mungu huwezi lolote 
Hatuwezi lolote bila Mungu ni hasara  .

Musa kamwambia Mungu usituchukue toka hapa 
Uso usipoenda nasi ee Mungu 
Maana ni nini kitakachotutofautisha 
Na watu wengine 
Ni nini kitakachotufanya tushinde Bwana  .

Nena nasi Mungu, nena nasi Bwana 
Usitutenge na uso wako nena nasi 
Bwana twakuomba aah  .

Uso wangu utakwenda nawewe na wewe 
Na mimi nitakupa raha raha 
Uso wangu utakwenda nawewe na wewe 
Na mimi nitakupa raha raha ah  .

Mwenyewe siwezi siwezi bila wewe 
Mwenyewe siwezi siwezi bila wewe 
Siwezi siwezi bila wewe siwezi  .

Siku moja bila Mungu bila uwepo wa Mungu 
Ni sawa na miaka elfu jangwani 
Siku moja bila Mungu bila uwepo wa Mungu 
Ni sawa na miaka mingi jangwani  .

Hatua nyingi bila Mungu 
Maendelea bila Mungu 
Mwisho ni aibu ni bure eeh 
Usianze wala kuenda bila Mungu 
Hutafika mbali wewe mwite  
Maana huwezi mwenyewe 
Uso wa Mungu ukiwa nawe 
Utakufanikisha wewe utakushindia 
Utakuwa juu  .

Whatever comes in your way 
You will overcome it 
because the presence of the Lord is with you hey
Amesema kila anipataye mimi 
Amepata uzima huyo 
Na kibali kwa Bwana oh 
Utapata zaidi ya hekima 
Na elimu za dunia 
Uso wa Mungu ukiwa nawewe utakuwa nuru  .

Tafuta sana kuwa na Mungu 
Tunza sana uwepo wa Mungu 
Maana huo ni ufungu wa Maisha  .

Ameahidi atakupatia ukimuomba lolote 
Omba sana uwepo wa Mungu maishani mwako 


Top Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Uso Wangu:

0 Comments/Reviews