Sifa Lyrics

Utukufu ni Wako by Sifaeli Mwabuka cover art

Sifaeli Mwabuka - Utukufu ni Wako Lyrics

Artist:
Sifaeli Mwabuka

Lyrics

Acha mimi nikushukuru wewe Mungu
Uliyenitunza toka utoto wangu
Ukanichagua tumboni mwa mama
Umeniweka kwenye kusudi lako nisimame

Acha mimi nikushukuru wewe Mungu
Uliyenitunza toka utoto wangu
Ukanichagua tumboni mwa mama
Umeniweka kwenye kusudi lako nisimame

Mimi ni nani kwa yote uliyonitendea?
Nimekulipa nini kwa uhai huu nilio nao
Mimi ni nani kwa yote uliyonitendea?
Nimekulipa nini kwa uhai huu nilio nao

Niseme ni akili zangu baba sio kweli
Niseme ni elimu yangu baba sio kweli
Niseme ni uzuri wangu baba sio kweli
Niseme ni utajiri wangu baba sio kweli

Acha mimi niseme, utukufu nakurudishia wewe
Nasema ni asante Mungu wangu, utukufu nakurudishia wewe
Mimi ni nani hata naishi leo, utukufu nakurudishia wewe
Niliomba mke ukanipa kutoka kwako, utukufu nakurudishia wewe
Maombi yangu ukajibu Mungu wangu, utukufu nakurudishia wewe
Niliomba kazi ukanipa kazi nzuri, utukufu nakurudishia wewe
Ooh Mungu, ee Mungu wangu

Niende kwa nani nikuache wewe Mungu
Hatua zangu zaongozwa na wewe
Maisha yangu yako mikononi mwako
Hata nipitie magumu najua Mungu yuko

Niende kwa nani nikuache wewe Mungu
Hatua zangu zaongozwa na wewe
Maisha yangu yako mikononi mwako
Hata nipitie magumu najua Mungu yuko

Jeuri yangu kwa sababu Mungu unanipenda
Ujasiri wangu kwa sababu Mungu unanilinda 
Jeuri yangu kwa sababu Mungu unanipenda
Ujasiri wangu kwa sababu Mungu unanilinda 

Niende kwa nani kama si wewe
Nimwite nani kama si wewe
Yote umefanya baba acha niseme baba asante

Utukufu nakurudishia wewe

Video