Joyce Omondi - Uinuliwe Lyrics

Album: Spirit vs Soul
Released: 10 Nov 2017
iTunes Amazon Music

Lyrics

Hallelujah pokea sifa wewe ni Bwana uinuliwe Hakuna Mungu kama wewe eh Yahweh ni wewe wewe pekee Wewe peke yako Ni we wa kuabudu na wa kutamani juu mbinguni na duniani Na duniani Mwaminifu we nitaeleza sifa zako eh Bwana umetukuka Wote wajue Ukuu wako wadumu milele na milele Hallelujah pokea sifa wewe ni Bwana uinuliwe Hallelujah pokea sifa wewe ni Bwana uinuliwe

Hakuna wa kufananishwa nawe Yesu wanitosha wanitosha Kwa moyo wangu wote nasema ni asante nashukuru Baba nakupenda Na wote na malaika maserafi na makerubi napaza Sauti nikisema mtakatifu ni wewe we Mwenyezi Mungu Hallelujah pokea sifa wewe ni Bwana uinuliwe Wastahili Wastahili sifa zote Sifa zote ni zako Wastahili Wastahili utukufu wote Baba Utukufu wote ni wako Wastahili Wastahili uwezo wote Uwezo wote ni wako Wastahili Wastahili Wastahili upendo wote Upendo wote ni wako Hallelujah pokea sifa wewe ni Bwana uinuliwe Hallelujah

Video

Joyce Omondi - Uinuliwe (Official HD Video) SMS SKIZA 7381085 to 811

Thumbnail for Uinuliwe video
Loading...
In Queue
View Lyrics