Sifa Lyrics

Peke Yako by Derick Marton cover art

Derick Marton - Peke Yako Lyrics

Artist:
Derick Marton

Lyrics

Nanyoosha mikono yangu juu!
Nanyoosha mikono yangu juu!


Nanyoosha mikono yangu juu
Kukusifu na kukuabudu
Nanyoosha mikono yangu juu
Kukusifu Mungu wa miungu


Uwezo wako, matendo yako 
Ni dhahiri juu ya ukuu wako 
Neema yako, rehema zako 
Ninajua ni sababu ya pendo lako 


Wewe ni Mungu wa wote wenye mwili 
Kanuni zako hakuna wa kubadili 
Unafanya mchana,usiku, alfajiri 
Jina lako ni Niko ambaye Niko 


Wewe ni Mkuu wa kusifiwa 
Kuabudiwa ni wewe 
Wewe Uko juu umeinuliwa 
Wa kushangiliwa ni wewe


Wewe ni Mkuu wa kusifiwa 
Kuabudiwa ni wewe 
Wewe Uko juu umeinuliwa 
Wa kushangiliwa ni wewe


Haulinganishwi haufanishwi 
Na chochote “ehhe eeh”  
Jehova Nissi 
Mimi bila wewe si lolote 


Haulinganishwi haufanishwi 
Na chochote “ehhe eeh”  
Jehova Nissi 
Mimi bila wewe si lolote 


Watawala milele watawala milele 
Watawala milele peke yako oh
Unadumu milele unadumu milele 
Unadumu milele peke yako oh


Wa kusifiwa wa kuabudiwa ni wewe 
Wewe uko juu umeinuliwa wa kushangiliwa ni wewe 
Wewe ni mkuu wa kusifiwa wa kuabudiwa ni wewe 
Wewe uko juu umeinuliwa wa kushangiliwa ni wewe


Wa kusifiwa wa kuabudiwa ni wewe 
Wewe uko juu umeinuliwa wa kushangiliwa ni wewe 
Wewe ni mkuu wa kusifiwa wa kuabudiwa ni wewe 
Wewe uko juu umeinuliwa wa kushangiliwa ni wewe


Nani kama wewe eeh 
Nani kama wewe baba nani kama wewe
Nani kama wewe eeh 
Nani kama wewe baba nani kama wewe


Wewe ni Mkuu wa kusifiwa 
Kuabudiwa ni wewe 
Wewe Uko juu umeinuliwa 
Wa kushangiliwa ni wewe


Wewe ni Mkuu wa kusifiwa 
Kuabudiwa ni wewe 
Wewe Uko juu umeinuliwa 
Wa kushangiliwa ni wewe


Watawala milele 
Watawala milele peke yako oh
Unadumu milele, unadumu milele
Unadumu milele peke yako oh


Video