Joyce Omondi - Lihimidi Jina Lake Lyrics
Lyrics
Mashariki na magharibi haziwezi kutana Hivyo ndivyo uliweka dhambi zangu mbali nami Kwa kukomboa uhai wangu wanisamehe Tena wanivisha taji ya upendo wako Ooh Nisemeje? Nikupe nini?
Eeeh nafsi yangu mhimidi bwana Usisahau fadhili zake zote Eeeh nafsi yangu mhimidi bwana Usisahau fadhili zake zote Lihimidi Jina lake Jina lake Jina lake Takatifu Lihimidi jina lake, Jina lake, jina lake Takatifu
Kweli Baba wewe ni mwema, uinuliwe Kwa ajili ya neema na fadhili zako Jina lako litukuzwe leo na milele Maana haulinganiswi na yeyote Baba Nisemeje nikupe nini ila sifa
Upendo wako umenizunguka Neema yako imenipandisha Halleluya, jina lako ni kuu Amani na furaha umenipa Halleluya, jina lako ni kuu
Astahili sifa, astahili utukufu Takatifu uu Baba
Video
Joyce Omondi - Lihimidi Jina Lake (Official Video) SMS SKIZA 7381082 to 811