Umesikia Kilio Changu Yesu Lyrics - Lavender Obuya

Lavender Obuya swahili

Buy/Download Audio

Umesikia Kilio Changu Yesu Lyrics

Kwa muda mengi nimeteseka aah,
Nikuugua magonjwa sugu, yaliyoshinda madakitari
Yaliyoshinda wenyi hekima wa dunia
Nilizunguka dunia kote eeh,
Nikitafuta uponyaji wangu sikupata
Wewe Mungu umeniponya bure Baba
Umeniponya bila malipo Yesu, umeniponya kwa damu yako
Kama sio wewe nitamwabudu nani,
Kama sio wewe nitamwabudu nani,
Umesikia Baba …

Umesikia kilio changu, ukanitoa shimoni Yesu
Ukanifanya kiumbe kipya, kama sio wewe nitamwabudu nani
Kama sio wewe nitamwabudu nani?

Umeniondolea aibu Yesu, nilikataliwa ulinikubali Baba
Ulinikubali jinsi nilivyo, ukaniokoa kwa damu yako Jehovah
Ukanikomboa kwa damu yako, ukanijaza kwa damu yako
Kama sio wewe nitamwabudu nani,
Kama sio wewe nitamwabudu nani? Kama si wewe …

Umesikia kilio changu, ukanitoa shimoni Yesu
Ukanifanya kiumbe kipya, kama sio wewe nitamwabudu nani
Kama sio wewe nitamwabudu nani?

Wewe ni kinga kwa wanyonge wote Baba
Wewe ni kinga kwa wasiojiweza
Wakikumbilia hakuna aibu
Wewe ni Mungu usiyebagua aah
Wewe ni Mungu haulinganishwi
Unapenda wote Mungu muumba aah
Nimekuchagua kati ya miungu Yesu
Kwa damu yako nimekombolewa, umeyavuta laana yangu
Umebadilisha historia Bwana
Kama sio wewe nitamwabudu nani? Kama si wewe …

Umesikia kilio changu, ukanitoa shimoni Yesu
Ukanifanya kiumbe kipya, kama sio wewe nitamwabudu nani
Kama sio wewe nitamwabudu nani?

Umesikia Kilio Changu Yesu Video