Sifa Lyrics

Dhahabu by Beatrice Mwaipaja cover art

Beatrice Mwaipaja - Dhahabu Lyrics

Artist:
Beatrice Mwaipaja

Lyrics

Nilipokuwa nipo chini mavumbini
Nilipokuwa nipo chini mavumbini
Walinikataa waliniona ni mavumbi tu
Walinikataa nilikuwa sina dhamani kwao


Walijua jana yangu, hawakujua leo yangu
Waliniona ni masikini, waliniona sina dhamani kwao
Waliniona sina lolote, ila walichokosea hao hao 
Walijua jana yangu wao, hawakujua leo yangu wanadamu


Leo nang'ara kama dhahabu 
Acha ning'are mi ni dhahabu
Leo nang'ara kama dhahabu 
Acha ning'are mi ni dhahabu


Mimi mimi ni dhahabu, mimi ni dhahabu
Mimi mimi ni dhahabu, mimi ni dhahabu
Mimi mimi ni dhahabu, mimi ni dhahabu
Mimi mimi ni dhahabu, mimi ni dhahabu


Usiidharau leo ya mtu
Usiidharau leo ya mtu
Maana haujui kesho yake
Maana haujui hatima yake
Hatima ya mtu i mikonono mwa Mungu
Hatima ya mtu i mikonono mwa Mungu


Aliye masikini leo, kesho huyo ndo tajiri
Unayemwona chini leo leo, kesho atainuliwa na Mungu
Hatima ya mtu i mikonono mwa Mungu
Kesho ya mtu i mikonono mwake Baba


Daudi alikuwa mchunga kondoo porini
Daudi alikuwa mchunga kondoo Daudi
Nani alijua Daudi ni mfalme
Nani alijua Daudi ni mtu mkubwa


Kumbe unaweza pitia leo, kwa utukufu wa kesho
Kumbe unaweza pitia leo, hiyo ni heshima kwa Mungu
Watakapo kuja kuinua watashanga aah
Usije idharau leo ya mtu'


Sasa nang'ara kama dhahabu
Amenitengeneza Mungu leo nang'ara
Kama dhahabu


Mimi mimi ni dhahabu, mimi ni dhahabu
Mimi mimi ni dhahabu, mimi ni dhahabu
Mimi mimi ni dhahabu, mimi ni dhahabu
Mimi mimi ni dhahabu, mimi ni dhahabu


Nilipokuwa masikini nilivumilia
Waliponikataa na kunibeza nilivumilia 


Leo nang'ara kama dhahabu
Acha ning'are Mungu amenitoa mbali
Acha ning'are Mungu amenikumbuka
Na sifa kuu ya dhahabu
Na sifa kuu ya dhahabu, dhahabu 


Ni lazima ipite kwenye moto
Ikipita kwenye moto dhahabu itang'ara tu


Na sifa kuu ya Mungu wetu huyu
Hutuinua kutoka chini, chini chini sana
Na kutupandisha mpaka juu
Na kutuketisha na wakuu


Usijeidharau leo ya mtu
Hatima ya mtu i mikonono mwa Mungu


Leo nang'ara kama dhahabu 
Acha ning'are mi ni dhahabu
Leo nang'ara kama dhahabu 
Acha ning'are mi ni dhahabu


Video