Sifa Lyrics

Ahadi by Paul Clement cover art

Paul Clement - Ahadi Lyrics

Artist:
Paul Clement
Album:
Uzima Tele
Official Release:
12 Dec 2025

Lyrics

Ahadi ya Mungu sio deni
Ahadi ya Mungu sio deni


Mungu hawezi kuahidi
Asichoweza timiza
Mungu hawezi kuahidi
Kama hana uhakika


Mungu hawezi kuahidi kitu chochote
Kama ana mashaka
Vyote alivyoahidi anaweza kutimiza
Kila alichoahidi kiko ndani ya uwezo wake
Mungu hasemi uongo wala hadanganyi
Alichoahidi hawezi kusahau


Ahadi za Mungu sio deni
Ahadi za Mungu ni kweli
Ahadi za Mungu subiri
Atazitimiza, atazitimiza


Mungu amesema tuombe lolote kwake
Tuombe lolote kwa jina lake
Ameahidi atatupa vyote
Na hatopoteza chochote


Alivyoahidi haanzi kutafuta
Alivyoahidi anavyokavitunza
Alivyoahidi amevitunza
Ameviweka kwenye ghala ya baraka


Anasubiri muda mwafaka
Aweze kutupatia
Hata kama inachelewa ingoje
Ahadi ya Mungu ingoje


Mungu hasemi uongo wala hadanganyi
Alichoahidi hawezi kusahau
Mungu hasemi uongo wala hadanganyi
Alichoahidi hawezi kusahau


Ahadi za Mungu sio deni
Ahadi za Mungu ni kweli
Ahadi za Mungu subiri
Atazitimiza, atazitimiza


Ahadi za Mungu sio deni
Ahadi za Mungu ni kweli
Ahadi za Mungu subiri
Atazitimiza, atazitimiza


Ni kweli, ni kweli
Ahadi zake, upendo wake, neno lake
Ni kweli, ni kweli
Ni kweli, ni kweli


 


Video