Giza totoro yanizingira
Miale haijanifikia
Ilhali kumekucha pambazuka
Imani yashuka didimia
Amani nayo yafifia
Eloi Lamasabaktani
Yuko Mungu anayeweza
Yuko Mungu anayetenda
Mwamini Yeye
Mwamini Yeye hutohaibika
Giza likiwa nisito Bwana atawasha
Sababu Mungu u mwenye hamasha
Atarejesha amani, atarejesha furaha
Ulivyovipoteza kwa muda mrefu
Atarejesha Bwana
Yuko Mungu anayeweza
Yuko Mungu anayetenda
Mwamini Yeye
Mwamini Yeye hutohaibika
Pale ninaposhindwa nani wa kuniwezesha
Yeye ndiye awezaye
Nikiwa vitani nani wa kunishindia
Ni yeye ndiye awezaye
Ninapotia shaka nani wa kuniongoza
Ni yeye Mungu yuko
Yuko Mungu anayeweza
Yuko Mungu anayetenda
Mwamini Yeye
Mwamini Yeye hutohaibika
Yuko Mungu anayeweza
Yuko Mungu anayetenda
Mwamini Yeye
Mwamini Yeye hutohaibika