Alice Kimanzi - Dua Lyrics

Dua Lyrics

VERSE 1:
Hali hii yangu
Isiwe nafasi ya kuto msifu Mungu
Mahali nilofika pasi ninungúnishe moyo
Daima nimshukuru
Nafsi yangu ’sisahau
Yale yote ametenda
Kwa upendo wake mwema
Kanizingira kwa neema
Moyo wangu vuta heri kwa subira

CHORUS:
Atajibu dua langu
Kwa njia Yake na wakati Wake (x2)
Moyo tulia

VERSE 2:
Najua njia hii si rahisi
Natambua mlima huu umezidi
Uwezo wangu
Egemeo ni Yesu tu
Na hata giza likija na mashaka pia
Yazibe macho yangu
Bado nitazidi kwani Ye aliahidi
Nasadiki Neno Lake kweli

BRIDGE:
Kwani Yeye anakuona
Tena Yeye anakujali (moyo tulia)
Anahisi uchungu wako
Tulia, tulia


Dua Video

Dua Lyrics -  Alice Kimanzi

Alice Kimanzi Songs

Related Songs