Sifa Lyrics

Nikumbuke by Joel Lwaga cover art

Joel Lwaga - Nikumbuke Lyrics

Artist:
Joel Lwaga

Lyrics

"Nikumbuke" by **Joel Lwaga ft. Diamond


[Verse 1 - Diamond Platnumz]

Eee Baba...

Sio kwamba nateseka

Ama nina wivu na baraka za wengine

Hapana, niko sawa


Eee Baba...

Sio kwamba nakukumbusha

Kwamba labda umenisahau

Hapana

Najua unanijua kwa jina

Unaona nayopitia


[Pre-Chorus]

Ila kama mwanadamu kuna muda

Moyo unauma, nazidiwa

Sa ntamweleza nani kama si wewe?

Yani kama mtu kuna muda mambo

Yananizidia, nazidiwa

Sa ntamwambia nani kama si wewe?


[Chorus]

Unapowabariki wengine

Usiniache na mimi

Usiniache na mimi

Baba nakungoja


Unapowapa riziki wengine

Unikumbuke na mimi

Unikumbuke na mimi

Baba nakungoja


Unapowabariki wengine

Usiniache na mimi

Usiniache na mimi

Baba nakungoja...


[Verse 2 - Joel Lwaga]

Mmmh

Riziki mafungu saba

Pengine la kwangu la sita

Ila wewe pekee ndo unayeweza ibadili hata ikawa kumi

Sifikiri Mungu Baba

Kwamba mi ndo mwema kabisa

Ila naomba ipokee ikipendeza dua yangu, nifute niduni


Baba mi nikila na kulala

Kupata shiba tu naridhika, wa...

Wape magari, nipe ndala

Walau miba kusitirika

Ukinipa nyumba pia eeh walah ah

Siwezi danganya ntafarijika

Pengine Baba biashara

Wateja waje kutiririka


[Pre-Chorus]

Maana kama mwanadamu kuna muda

Mambo yananizidi, nazidiwa Baba

Sa ntamweleza nani kama si wewe?


Oooh...

Kule ada, huku kodi ya pango

Mfukoni sina kitu, sina mambo

Sa ntamwambia nani kama si wewe?

Oooh Baba


[Chorus]

Unapowabariki wengine (Wengine)

Usiniache na mimi

Usiniache na mimi

Baba nakungoja


Unapowapa riziki wengine (Eeeh)

Unikumbuke na mimi

Unikumbuke na mimi

Baba nakungoja


Unapofuta machozi wengine

Usiniache na mimi

Usiniache na mimi

Baba nakungoja


Unapowainua wengine

Unikumbuke na mimi

Unikumbuke na mimi

Baba nakungoja


[Outro]

Ooooh

Baba nakungoja

Sina mwingine mi

Baba nakungoja


Video