1 Wafalme 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 9 (Swahili) 1st Kings 9 (English)

Ikawa Sulemani alipokwisha kuijenga nyumba ya Bwana, na nyumba ya mfalme, na mambo yote yaliyoingia moyoni mwake Sulemani, naye akataka kuyafanya, 1 Wafalme 9:1

It happened, when Solomon had finished the building of the house of Yahweh, and the king's house, and all Solomon's desire which he was pleased to do,

basi, Bwana akamtokea Sulemani mara ya pili kama alivyomtokea huko Gibeoni. 1 Wafalme 9:2

that Yahweh appeared to Solomon the second time, as he had appeared to him at Gibeon.

Bwana akamwambia, Nimeyasikia maombi yako na dua zako, ulizotoa mbele zangu. Nimeitakasa nyumba hii uliyoijenga ili niweke jina langu humo milele; tena macho yangu na moyo wangu utakuwapo hapo siku zote; 1 Wafalme 9:3

Yahweh said to him, I have heard your prayer and your supplication, that you have made before me: I have made this house holy, which you have built, to put my name there forever; and my eyes and my heart shall be there perpetually.

na wewe, ukienda mbele zangu kama alivyokwenda Daudi, baba yako, kwa ukamilifu wa moyo, na kwa adili, kufanya hayo yote niliyokuamuru, na kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, 1 Wafalme 9:4

As for you, if you will walk before me, as David your father walked, in integrity of heart, and in uprightness, to do according to all that I have commanded you, and will keep my statutes and my ordinances;

ndipo nitakapokifanya imara kiti cha ufalme wako juu ya Israeli milele; kama nilivyomwahidia Daudi, baba yako, nikisema, Hutakosa kuwa na mtu wa kukaa katika kiti cha enzi cha Israeli. 1 Wafalme 9:5

then I will establish the throne of your kingdom over Israel forever, according as I promised to David your father, saying, There shall not fail you a man on the throne of Israel.

Bali mkighairi, mkaacha kunifuata, ninyi na watoto wenu, msizishike sheria zangu na amri zangu, nilizoziweka mbele yenu, tena mkienda na kuitumikia miungu mingine na kuiabudu, 1 Wafalme 9:6

But if you shall turn away from following me, you or your children, and not keep my commandments and my statutes which I have set before you, but shall go and serve other gods, and worship them;

basi nitawakatilia Israeli mbali na nchi hii niliyowapa; na nyumba hii niliyoitakasa kwa jina langu, nitaitupilia mbali na macho yangu, na Israeli watakuwa mithali na neno la tusi katika mataifa yote. 1 Wafalme 9:7

then will I cut off Israel out of the land which I have given them; and this house, which I have made holy for my name, will I cast out of my sight; and Israel shall be a proverb and a byword among all peoples.

Na ijapokuwa nyumba hii imetukuka namna hii, lakini kila apitaye atasituka na kuizomea; nao watasema, Kwa nini Bwana ameitenda nchi hii na nyumba hii mambo haya? 1 Wafalme 9:8

Though this house is so high, yet shall everyone who passes by it be astonished, and shall hiss; and they shall say, Why has Yahweh done thus to this land, and to this house?

Na watu watajibu, Kwa sababu walimwacha Bwana, Mungu wao, aliyewatoa baba zao katika nchi ya Misri, wakashikamana na miungu mingine na kuiabudu na kuitumikia, basi ndiyo sababu Bwana ameleta mabaya haya yote juu yao. 1 Wafalme 9:9

and they shall answer, Because they forsook Yahweh their God, who brought forth their fathers out of the land of Egypt, and laid hold on other gods, and worshiped them, and served them: therefore has Yahweh brought all this evil on them.

Ikawa miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani alizijenga zile nyumba mbili, nyumba ya Bwana na nyumba yake mfalme, 1 Wafalme 9:10

It happened at the end of twenty years, in which Solomon had built the two houses, the house of Yahweh and the king's house

(basi Hiramu, mfalme wa Tiro, alikuwa amemletea Sulemani mierezi na miberoshi, na dhahabu, sawasawa na haja zake zote), ndipo mfalme Sulemani akampa Hiramu miji ishirini ya nchi ya Galilaya. 1 Wafalme 9:11

(now Hiram the king of Tyre had furnished Solomon with cedar trees and fir trees, and with gold, according to all his desire), that then king Solomon gave Hiram twenty cities in the land of Galilee.

Naye Hiramu akatoka Tiro kuitazama hiyo miji Sulemani aliyompa; wala haikumpendeza. 1 Wafalme 9:12

Hiram came out from Tyre to see the cities which Solomon had given him; and they didn't please him.

Akasema, Miji gani hii uliyonipa, ndugu yangu? Akaiita nchi ya Kabuli, hata leo. 1 Wafalme 9:13

He said, What cities are these which you have given me, my brother? He called them the land of Cabul to this day.

Hiramu akamletea mfalme talanta sitini za dhahabu. 1 Wafalme 9:14

Hiram sent to the king one hundred twenty talents of gold.

Na hii ndiyo sababu ya shokoa aliyoitoza mfalme Sulemani; ili kuijenga nyumba ya Bwana, na nyumba yake mwenyewe, na Milo, na ukuta wa Yerusalemu, na Hazori, na Megido, na Gezeri. 1 Wafalme 9:15

This is the reason of the levy which king Solomon raised, to build the house of Yahweh, and his own house, and Millo, and the wall of Jerusalem, and Hazor, and Megiddo, and Gezer.

Farao, mfalme wa Misri, alikuwa amepanda akautwaa Gezeri, na kuuteketeza kwa moto, akawaua Wakanaani waliokaa mjini, akampa zawadi binti yake, mkewe Sulemani. 1 Wafalme 9:16

Pharaoh king of Egypt had gone up, and taken Gezer, and burnt it with fire, and slain the Canaanites who lived in the city, and given it for a portion to his daughter, Solomon's wife.

Naye Sulemani akaujenga Gezeri, na Beth-horoni wa chini, 1 Wafalme 9:17

Solomon built Gezer, and Beth Horon the lower,

na Baalathi, na Tamari ulio nyikani, katika nchi; 1 Wafalme 9:18

and Baalath, and Tamar in the wilderness, in the land,

na miji yote ya hazina iliyokuwa yake Sulemani; na miji ya magari yake, na miji ya watu wake wapandao farasi, na kila alichopenda kujenga Sulemani huko Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake. 1 Wafalme 9:19

and all the store-cities that Solomon had, and the cities for his chariots, and the cities for his horsemen, and that which Solomon desired to build for his pleasure in Jerusalem, and in Lebanon, and in all the land of his dominion.

Kwa habari ya watu wote waliosalia, Waamori, Wahiti, Waperizi, Wahivi, na Wayebusi, wasiokuwa wa wana wa Israeli; 1 Wafalme 9:20

As for all the people who were left of the Amorites, the Hittites, the Perizzites, the Hivites, and the Jebusites, who were not of the children of Israel;

watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuweza kuwaharibu kabisa, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo. 1 Wafalme 9:21

their children who were left after them in the land, whom the children of Israel were not able utterly to destroy, of them did Solomon raise a levy of bondservants to this day.

Lakini wa wana wa Israeli Sulemani hakumtumikisha mtu shokoa; ila ndio watu wa vita, na wangoje wake, na wakuu wake, na akida zake, na wakuu, wa magari yake, na wa wapanda farasi wake. 1 Wafalme 9:22

But of the children of Israel did Solomon make no bondservants; but they were the men of war, and his servants, and his princes, and his captains, and rulers of his chariots and of his horsemen.

Hao maakida wakuu, waliokuwa juu ya kazi yake Sulemani, walikuwa mia tano na hamsini, waliowaamuru watu watendao kazi. 1 Wafalme 9:23

These were the chief officers who were over Solomon's work, five hundred fifty, who bore rule over the people who labored in the work.

Lakini binti Farao akapanda toka mji wa Daudi, mpaka hiyo nyumba yake Sulemani, aliyomjengea; kisha, aliijenga Milo. 1 Wafalme 9:24

But Pharaoh's daughter came up out of the city of David to her house which [Solomon] had built for her: then did he build Millo.

Na mara tatu kila mwaka Sulemani alikuwa akitoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani juu ya madhabahu aliyomjengea Bwana akafukiza uvumba pamoja nazo juu ya madhabahu iliyokuwako mbele za Bwana. Hivyo akaimaliza nyumba. 1 Wafalme 9:25

Three times a year did Solomon offer burnt offerings and peace-offerings on the altar which he built to Yahweh, burning incense therewith, [on the altar] that was before Yahweh. So he finished the house.

Tena, mfalme Sulemani akaunda merikebu huko Ezion-geberi, ulioko karibu na Elothi, pwani ya Bahari ya Shamu, katika nchi ya Edomu. 1 Wafalme 9:26

King Solomon made a navy of ships in Ezion Geber, which is beside Eloth, on the shore of the Red Sea, in the land of Edom.

Naye Hiramu akatuma merikebuni watumishi wake, wanamaji wenye kuijua bahari, pamoja na watumishi wake Sulemani. 1 Wafalme 9:27

Hiram sent in the navy his servants, sailors who had knowledge of the sea, with the servants of Solomon.

Wakafika Ofiri, wakachukua toka huko dhahabu, talanta mia nne na ishirini, wakamletea mfalme Sulemani.

1 Wafalme 9:28

They came to Ophir, and fetched from there gold, four hundred and twenty talents, and brought it to king Solomon.