1 Wafalme 1 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 1 (Swahili) 1st Kings 1 (English)

Mfalme Daudi alikuwa mzee, mkongwe katika siku zake, nao wakamfunika nguo, lakini asipate moto. 1 Wafalme 1:1

Now king David was old and stricken in years; and they covered him with clothes, but he got no heat.

Kwa hiyo watumishi wake wakamwambia, Bwana wangu mfalme na atafutiwe kijana mwanamwali; naye asimame mbele ya mfalme, amtunze; alale kifuani mwako, ili bwana wangu mfalme apate moto. 1 Wafalme 1:2

Therefore his servants said to him, Let there be sought for my lord the king a young virgin: and let her stand before the king, and cherish him; and let her lie in your bosom, that my lord the king may keep warm.

Basi wakatafuta kijana mzuri mipakani mwote mwa Israeli, wakamwona Abishagi, Mshunami, wakamleta kwa mfalme. 1 Wafalme 1:3

So they sought for a beautiful young lady throughout all the borders of Israel, and found Abishag the Shunammite, and brought her to the king.

Naye kijana huyo alikuwa mzuri sana; akamtunza mfalme, akamtumikia; walakini mfalme hakumjua. 1 Wafalme 1:4

The young lady was very beautiful; and she cherished the king, and ministered to him; but the king didn't know her intimately.

Ndipo Adonia mwana wa Hagithi akatakabari, akasema, Mimi nitakuwa mfalme. Akajiwekea tayari magari na wapanda farasi, na watu hamsini wapige mbio mbele yake. 1 Wafalme 1:5

Then Adonijah the son of Haggith exalted himself, saying, I will be king: and he prepared him chariots and horsemen, and fifty men to run before him.

Tena baba yake hakumchukiza wakati wo wote kwa kusema, Mbona umefanya hivi? Kisha, alikuwa mtu mzuri sana; naye alizaliwa baada ya Absalomu. 1 Wafalme 1:6

His father had not displeased him at any time in saying, Why have you done so? and he was also a very goodly man; and he was born after Absalom.

Akashauriana na Yoabu, mwana wa Seruya, na Abiathari, kuhani; nao wakamsaidia Adonia, wakamfuata. 1 Wafalme 1:7

He conferred with Joab the son of Zeruiah, and with Abiathar the priest: and they following Adonijah helped him.

Ila Sadoki, kuhani, na Benaya, mwana wa Yehoyada, na Nathani, nabii, na Shimei, na Rei, na mashujaa wa Daudi, hao hawakuwa pamoja na Adonia. 1 Wafalme 1:8

But Zadok the priest, and Benaiah the son of Jehoiada, and Nathan the prophet, and Shimei, and Rei, and the mighty men who belonged to David, were not with Adonijah.

Adonia akachinja kondoo, na ng'ombe, na vinono, karibu na jiwe la Zohelethi, lililo karibu na chemchemi Rogeli; akawaita ndugu zake wote, wana wa mfalme, na watu wote wa Yuda, watumishi wa mfalme; 1 Wafalme 1:9

Adonijah killed sheep and oxen and fatlings by the stone of Zoheleth, which is beside En Rogel; and he called all his brothers, the king's sons, and all the men of Judah, the king's servants:

ila Nathani, nabii, na Benaya, na mashujaa, na Sulemani nduguye, hakuwaita hao. 1 Wafalme 1:10

but Nathan the prophet, and Benaiah, and the mighty men, and Solomon his brother, he didn't call.

Ndipo Nathani akamwambia Bath-sheba, mamaye Sulemani, akasema, Je! Hukusikia ya kuwa Adonia, mwana wa Hagithi, anamiliki, na bwana wetu Daudi hana habari? 1 Wafalme 1:11

Then Nathan spoke to Bathsheba the mother of Solomon, saying, Haven't you heard that Adonijah the son of Haggith reigns, and David our lord doesn't know it?

Haya basi, nikupe shauri, tafadhali, upate kuiokoa roho yako, na roho ya mwanao Sulemani. 1 Wafalme 1:12

Now therefore come, please let me give you counsel, that you may save your own life, and the life of your son Solomon.

Enenda uingie ndani kwa mfalme Daudi, ukamwambie, Je! Hukuniapia mimi mjakazi wako, Ee mfalme, bwana wangu, kusema, Hakika yake Sulemani mwana wako atamiliki baada yangu, na kuketi katika kiti changu cha enzi? Mbona basi anamiliki Adonia? 1 Wafalme 1:13

Go and get you in to king David, and tell him, Didn't you, my lord, king, swear to your handmaid, saying, Assuredly Solomon your son shall reign after me, and he shall sit on my throne? why then does Adonijah reign?

Tazama, wakati ule utakapokuwa katika kusema na mfalme, mimi nami nitaingia nyuma yako, na kuyahakikisha maneno yako. 1 Wafalme 1:14

Behold, while you yet talk there with the king, I also will come in after you, and confirm your words.

Basi Bath-sheba akaingia ndani kwa mfalme, ndani ya chumba chake; naye mfalme alikuwa mzee sana; na Abishagi, Mshunami, alikuwa akimtumikia mfalme. 1 Wafalme 1:15

Bathsheba went in to the king into the chamber: and the king was very old; and Abishag the Shunammite was ministering to the king.

Bath-sheba akainama, akamsujudia mfalme. Naye mfalme akamwuliza, Wataka nini? 1 Wafalme 1:16

Bathsheba bowed, and did obeisance to the king. The king said, What would you?

Akamwambia, Bwana wangu, uliniapia mimi mjakazi wako kwa Bwana, Mungu wako, ya kwamba, bila shaka Sulemani mwanao atamiliki baada yangu, yeye ndiye atakayeketi katika kiti changu cha enzi. 1 Wafalme 1:17

She said to him, My lord, you swore by Yahweh your God to your handmaid, [saying], Assuredly Solomon your son shall reign after me, and he shall sit on my throne.

Na sasa, angalia, Adonia anamiliki; na wewe, bwana wangu mfalme, huna habari. 1 Wafalme 1:18

Now, behold, Adonijah reigns; and you, my lord the king, don't know it:

Tena amechinja ng'ombe, na vinono, na kondoo tele, na kuwaita wana wa mfalme wote pia, na Abiathari, kuhani, na Yoabu, jemadari wa jeshi. Ila Sulemani, mtumishi wako, huyu hakumwita. 1 Wafalme 1:19

and he has slain oxen and fatlings and sheep in abundance, and has called all the sons of the king, and Abiathar the priest, and Joab the captain of the host; but he hasn't called Solomon your servant.

Ee mfalme, bwana wangu, macho ya Israeli wote yanakuelekea wewe, kwamba uwaambie ni nani atakayeketi katika kiti chako cha enzi baada yako, Ee mfalme, bwana wangu. 1 Wafalme 1:20

You, my lord the king, the eyes of all Israel are on you, that you should tell them who shall sit on the throne of my lord the king after him.

Ama sivyo itakuwa, bwana wangu mfalme atakapolala pamoja na baba zake, mimi na mwanangu Sulemani tutahesabiwa kuwa wahalifu. 1 Wafalme 1:21

Otherwise it will happen, when my lord the king shall sleep with his fathers, that I and my son Solomon shall be counted offenders.

Basi tazama, alipokuwa katika kusema na mfalme, Nathani, nabii, aliingia. 1 Wafalme 1:22

Behold, while she yet talked with the king, Nathan the prophet came in.

Wakamwambia mfalme wakasema, Tazama, Nathani, nabii. Naye alipoingia ndani mbele ya mfalme, akamsujudia kifudifudi. 1 Wafalme 1:23

They told the king, saying, Behold, Nathan the prophet. When he was come in before the king, he bowed himself before the king with his face to the ground.

Nathani akasema, Ee mfalme, bwana wangu, je! Wewe umesema ya kwamba, Adonia atamiliki baada yangu, ndiye atakayeketi katika kiti changu cha enzi? 1 Wafalme 1:24

Nathan said, My lord, king, have you said, Adonijah shall reign after me, and he shall sit on my throne?

Maana leo ameshuka, na kuchinja ng'ombe, na vinono, na kondoo tele, naye amewaita wana wote wa mfalme, na majemadari wa jeshi, na Abiathari, kuhani; na tazama, wanakula na kunywa mbele yake, wakisema, Na aishi mfalme Adonia! 1 Wafalme 1:25

For he is gone down this day, and has slain oxen and fatlings and sheep in abundance, and has called all the king's sons, and the captains of the host, and Abiathar the priest; and, behold, they are eating and drinking before him, and say, [Long] live king Adonijah.

Walakini mimi, mimi mtumishi wako, na Sadoki, kuhani, na Benaya, mwana wa Yehoyada, na Sulemani, mtumishi wako, hakutuita sisi. 1 Wafalme 1:26

But he hasn't called me, even me your servant, and Zadok the priest, and Benaiah the son of Jehoiada, and your servant Solomon.

Je! Bwana wangu mfalme ndiye aliyelitenda jambo hili, bila kutujulisha sisi watumishi wako ni nani atakayeketi katika kiti cha enzi cha bwana wangu mfalme baada yake? 1 Wafalme 1:27

Is this thing done by my lord the king, and you haven't shown to your servants who should sit on the throne of my lord the king after him?

Ndipo mfalme Daudi akajibu, akasema, Niitieni Bath-sheba. Basi akaingia ndani kwa mfalme, akasimama mbele ya mfalme. 1 Wafalme 1:28

Then king David answered, Call to me Bathsheba. She came into the king's presence, and stood before the king.

Naye mfalme akaapa, akasema, Bwana aishivyo, aliyenikomboa roho yangu katika shida zote, 1 Wafalme 1:29

The king swore, and said, As Yahweh lives, who has redeemed my soul out of all adversity,

hakika yake nitafanya leo kama vile nilivyokuapia kwa Bwana, Mungu wa Israeli, nikasema, Kwa yakini Sulemani mwanao atamiliki baada yangu, naye ndiye atakayeketi katika kiti changu cha enzi badala yangu. 1 Wafalme 1:30

most assuredly as I swore to you by Yahweh, the God of Israel, saying, Assuredly Solomon your son shall reign after me, and he shall sit on my throne in my place; most assuredly so will I do this day.

Ndipo Bath-sheba akainama kifudifudi, akamsujudia mfalme, akasema, Bwana wangu mfalme Daudi na aishi milele. 1 Wafalme 1:31

Then Bathsheba bowed with her face to the earth, and did obeisance to the king, and said, Let my lord king David live forever.

Naye mfalme Daudi akasema, Niitie Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, na Benaya, mwana wa Yehoyada. Nao wakaingia ndani mbele ya mfalme. 1 Wafalme 1:32

King David said, Call to me Zadok the priest, and Nathan the prophet, and Benaiah the son of Jehoiada. They came before the king.

Naye mfalme akawaambia, Twaeni pamoja nanyi watumishi wa bwana wenu, mkampandishe Sulemani mwanangu juu ya nyumbu wangu mimi mkamtelemshe mpaka Gihoni; 1 Wafalme 1:33

The king said to them, Take with you the servants of your lord, and cause Solomon my son to ride on my own mule, and bring him down to Gihon:

kisha Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, na wamtie mafuta huko, awe mfalme juu ya Israeli; kapigeni panda, mkaseme, Mfalme Sulemani na aishi! 1 Wafalme 1:34

and let Zadok the priest and Nathan the prophet anoint him there king over Israel; and blow you the trumpet, and say, [Long] live king Solomon.

Kisha pandeni juu nyuma yake, naye atakuja ili aketi katika kiti changu cha enzi; kwa maana atakuwa mfalme badala yangu; ndiye niliyemweka awamiliki Israeli na Yuda. 1 Wafalme 1:35

Then you shall come up after him, and he shall come and sit on my throne; for he shall be king in my place; and I have appointed him to be prince over Israel and over Judah.

Basi Benaya, mwana wa Yehoyada, akamjibu mfalme, akasema, Amina; Bwana, Mungu na bwana wangu mfalme, na aseme vivyo hivyo. 1 Wafalme 1:36

Benaiah the son of Jehoiada answered the king, and said, Amen: Yahweh, the God of my lord the king, say so [too].

Kama vile Bwana alivyokuwa pamoja na bwana wangu mfalme, kadhalika na awe pamoja na Sulemani, na kufanya kiti chake cha enzi kuwa kitukufu kuliko kiti cha enzi cha bwana wangu mfalme Daudi. 1 Wafalme 1:37

As Yahweh has been with my lord the king, even so be he with Solomon, and make his throne greater than the throne of my lord king David.

Basi wakashuka Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, na Benaya, mwana wa Yehoyada, na Wakerethi, na Wapelethi, wakampandisha Sulemani juu ya nyumbu wa mfalme Daudi, wakampeleka mpaka Gihoni. 1 Wafalme 1:38

So Zadok the priest, and Nathan the prophet, and Benaiah the son of Jehoiada, and the Cherethites and the Pelethites, went down, and caused Solomon to ride on king David's mule, and brought him to Gihon.

Na Sadoki, kuhani, akatwaa ile pembe ya mafuta katika Hema, akamtia Sulemani mafuta. Nao wakapiga panda; na watu wote wakasema, Mfalme Sulemani na aishi! 1 Wafalme 1:39

Zadok the priest took the horn of oil out of the Tent, and anointed Solomon. They blew the trumpet; and all the people said, [Long] live king Solomon.

Kisha watu wote wakapanda juu nyuma yake, watu wakapiga mazomari, wakafurahi furaha kubwa mno, hata nchi ikapasuka kwa sauti zao. 1 Wafalme 1:40

All the people came up after him, and the people piped with pipes, and rejoiced with great joy, so that the earth shook with the sound of them.

Basi Adonia, na wageni wote waliokuwa pamoja naye, wakasikia hayo walipokuwa wamekwisha kula. Naye Yoabu aliposikia sauti ya panda alisema, Za nini kelele hizi za mji uliotaharuki? 1 Wafalme 1:41

Adonijah and all the guests who were with him heard it as they had made an end of eating. When Joab heard the sound of the trumpet, he said, Why is this noise of the city being in an uproar?

Naye alipokuwa katika kunena, tazama Yonathani, mwana wa Abiathari kuhani, akafika. Naye Adonia akasema, Karibu; maana wewe u mtu mwema, unaleta habari njema. 1 Wafalme 1:42

While he yet spoke, behold, Jonathan the son of Abiathar the priest came: and Adonijah said, Come in; for you are a worthy man, and bring good news.

Naye Yonathani akajibu, akamwambia Adonia, Hakika bwana wetu mfalme Daudi amemtawaza Sulemani. 1 Wafalme 1:43

Jonathan answered Adonijah, Most assuredly our lord king David has made Solomon king:

Tena mfalme alipeleka pamoja naye Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, na Benaya, mwana wa Yehoyada, na Wakerethi, na Wapelethi, wakampandisha juu ya nyumbu wa mfalme. 1 Wafalme 1:44

and the king has sent with him Zadok the priest, and Nathan the prophet, and Benaiah the son of Jehoiada, and the Cherethites and the Pelethites; and they have caused him to ride on the king's mule;

Kisha Sadoki, kuhani, na Nathani, nabii, wakamtia mafuta huko Gihoni, ili awe mfalme. Nao wamepanda juu kutoka huko wakifurahi, hata mji ukavuma. Ndizo kelele zile mlizozisikia. 1 Wafalme 1:45

and Zadok the priest and Nathan the prophet have anointed him king in Gihon; and they are come up from there rejoicing, so that the city rang again. This is the noise that you have heard.

Na tena, Sulemani ameketi katika kiti cha enzi cha ufalme. 1 Wafalme 1:46

Also Solomon sits on the throne of the kingdom.

Na tena, watumishi wa mfalme walifika, ili wambariki bwana wetu mfalme Daudi, wakisema, Mungu wako na alikuze jina la Sulemani kuliko jina lako, na kukifanya kiti chake cha enzi kuwa kitukufu kuliko kiti chako. Naye mfalme akainama chini juu ya kitanda chake. 1 Wafalme 1:47

Moreover the king's servants came to bless our lord king David, saying, Your God make the name of Solomon better than your name, and make his throne greater than your throne: and the king bowed himself on the bed.

Na tena, mfalme akasema hivi, Bwana, Mungu wa Israeli, ahimidiwe, aliyenipa leo hivi mtu wa kuketi katika kiti changu cha enzi, nayo macho yangu yakiwa yanaona hayo. 1 Wafalme 1:48

Also thus said the king, Blessed be Yahweh, the God of Israel, who has given one to sit on my throne this day, my eyes even seeing it.

Ndipo wageni wote waliokuwa pamoja na Adonia wakaogopa, wakaondoka, wakaenda zao kila mtu njia yake. 1 Wafalme 1:49

All the guests of Adonijah were afraid, and rose up, and went every man his way.

Adonia naye akaogopa mbele ya Sulemani; akaondoka, akaenda, akazishika pembe za madhabahu. 1 Wafalme 1:50

Adonijah feared because of Solomon; and he arose, and went, and caught hold on the horns of the altar.

Akaambiwa Sulemani, kusema, Tazama, Adonia amwogopa mfalme Sulemani; kwani, tazama, amezishika pembe za madhabahu, akisema, Mfalme Sulemani na aniapie leo kwamba hataniua mimi mtumwa wake kwa upanga. 1 Wafalme 1:51

It was told Solomon, saying, Behold, Adonijah fears king Solomon; for, behold, he has laid hold on the horns of the altar, saying, Let king Solomon swear to me first that he will not kill his servant with the sword.

Akasema Sulemani, Akionekana kuwa mtu wa kweli, hata unywele mmoja wake hautaanguka chini; lakini uovu ukionekana ndani yake, atakufa. 1 Wafalme 1:52

Solomon said, If he shall show himself a worthy man, there shall not a hair of him fall to the earth; but if wickedness be found in him, he shall die.

Basi mfalme Sulemani akatuma watu, wakamtelemsha toka madhabahuni. Naye akaja, akamwinamia mfalme Sulemani; naye Sulemani akamwambia, Enenda nyumbani kwako. 1 Wafalme 1:53

So king Solomon sent, and they brought him down from the altar. He came and did obeisance to king Solomon; and Solomon said to him, Go to your house.