1 Wafalme 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 11 (Swahili) 1st Kings 11 (English)

Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti, 1 Wafalme 11:1

Now king Solomon loved many foreign women, together with the daughter of Pharaoh, women of the Moabites, Ammonites, Edomites, Sidonians, and Hittites;

na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda. 1 Wafalme 11:2

of the nations concerning which Yahweh said to the children of Israel, You shall not go among them, neither shall they come among you; for surely they will turn away your heart after their gods: Solomon joined to these in love.

Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo. 1 Wafalme 11:3

He had seven hundred wives, princesses, and three hundred concubines; and his wives turned away his heart.

Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake. 1 Wafalme 11:4

For it happened, when Solomon was old, that his wives turned away his heart after other gods; and his heart was not perfect with Yahweh his God, as was the heart of David his father.

Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni. 1 Wafalme 11:5

For Solomon went after Ashtoreth the goddess of the Sidonians, and after Milcom the abomination of the Ammonites.

Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake. 1 Wafalme 11:6

Solomon did that which was evil in the sight of Yahweh, and didn't go fully after Yahweh, as did David his father.

Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni. 1 Wafalme 11:7

Then did Solomon build a high place for Chemosh the abomination of Moab, on the mountain that is before Jerusalem, and for Molech the abomination of the children of Ammon.

Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu. 1 Wafalme 11:8

So did he for all his foreign wives, who burnt incense and sacrificed to their gods.

Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili, 1 Wafalme 11:9

Yahweh was angry with Solomon, because his heart was turned away from Yahweh, the God of Israel, who had appeared to him twice,

akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana. 1 Wafalme 11:10

and had commanded him concerning this thing, that he should not go after other gods: but he didn't keep that which Yahweh commanded.

Kwa hiyo Bwana akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako. 1 Wafalme 11:11

Therefore Yahweh said to Solomon, Because this is done of you, and you have not kept my covenant and my statutes, which I have commanded you, I will surely tear the kingdom from you, and will give it to your servant.

Walakini katika siku zako sitafanya haya, kwa ajili ya Daudi baba yako; nitaurarua utoke katika mkono wa mwana wako. 1 Wafalme 11:12

Notwithstanding in your days I will not do it, for David your father's sake: but I will tear it out of the hand of your son.

Lakini sitauondoa ufalme wote pia; nitampa mwana wako kabila moja, kwa ajili ya Daudi mtumishi wangu, na kwa ajili ya Yerusalemu niliouchagua. 1 Wafalme 11:13

However I will not tear away all the kingdom; but I will give one tribe to your son, for David my servant's sake, and for Jerusalem's sake which I have chosen.

Ndipo Bwana akamwondokeshea Sulemani adui, Hadadi Mwedomi; yeye alikuwa wa wazao wake mfalme wa Edomu. 1 Wafalme 11:14

Yahweh raised up an adversary to Solomon, Hadad the Edomite: he was of the king's seed in Edom.

Kwa maana ikawa, Daudi alipokuwako Edomu, naye Yoabu, mkuu wa jeshi, amepanda awazike waliouawa, akiisha kumpiga kila mwanamume wa Edomu, 1 Wafalme 11:15

For it happened, when David was in Edom, and Joab the captain of the host was gone up to bury the slain, and had struck every male in Edom

(kwa kuwa Yoabu alikaa huko miezi sita pamoja na Israeli wote, hata alipompoteza kila mwanamume wa Edomu); 1 Wafalme 11:16

(for Joab and all Israel remained there six months, until he had cut off every male in Edom);

yule Hadadi alikimbia, yeye na Waedomi wengine, watumishi wa baba yake, pamoja naye, waende Misri; yule Hadadi akali ni mtoto mdogo. 1 Wafalme 11:17

that Hadad fled, he and certain Edomites of his father's servants with him, to go into Egypt, Hadad being yet a little child.

Wakaondoka katika Midiani, wakafika Parani; wakachukua pamoja nao watu toka Parani, wakafika Misri, kwa Farao mfalme wa Misri; aliyempa nyumba, akamwamria vyakula, akampa mashamba. 1 Wafalme 11:18

They arose out of Midian, and came to Paran; and they took men with them out of Paran, and they came to Egypt, to Pharaoh king of Egypt, who gave him a house, and appointed him food, and gave him land.

Hadadi akapendeza sana machoni pa Farao, hata akamwoza umbu la mkewe, umbu la Tapenesi aliyekuwa malkia. 1 Wafalme 11:19

Hadad found great favor in the sight of Pharaoh, so that he gave him as wife the sister of his own wife, the sister of Tahpenes the queen.

Naye huyo umbu la Tapenesi akamzalia Genubathi mwanawe, ambaye Tapenesi alimlea nyumbani mwa Farao; naye Genubathi akawako nyumbani mwa Farao pamoja na wana wa Farao. 1 Wafalme 11:20

The sister of Tahpenes bore him Genubath his son, whom Tahpenes weaned in Pharaoh's house; and Genubath was in Pharaoh's house among the sons of Pharaoh.

Naye Hadadi aliposikia huko Misri ya kuwa Daudi amelala na babaze, na Yoabu, jemadari wa jeshi, amekufa, Hadadi akamwambia Farao, Unipe ruhusa, niende mpaka nchi yangu. 1 Wafalme 11:21

When Hadad heard in Egypt that David slept with his fathers, and that Joab the captain of the host was dead, Hadad said to Pharaoh, Let me depart, that I may go to my own country.

Farao akamwambia, Umekosa nini kwangu, hata, tazama, unatafuta kuirudia nchi yako? Akajibu, Hakuna, lakini unipe ruhusa tu. 1 Wafalme 11:22

Then Pharaoh said to him, But what have you lacked with me, that behold, you seek to go to your own country? He answered, Nothing: however only let me depart.

Tena, Mungu akamwondokeshea adui mwingine, Rezoni mwana wa Eliada, aliyemkimbia bwana wake Hadadezeri mfalme wa Soba, 1 Wafalme 11:23

God raised up [another] adversary to him, Rezon the son of Eliada, who had fled from his lord Hadadezer king of Zobah.

naye akakusanya watu, akawa mkuu wa jeshi, hapo Daudi alipowaua hao watu wa Soba; wakaenda Dameski, wakakaa humo, na kumiliki huko Dameski. 1 Wafalme 11:24

He gathered men to him, and became captain over a troop, when David killed them [of Zobah]: and they went to Damascus, and lived therein, and reigned in Damascus.

Naye akawa adui wa Israeli siku zote za Sulemani, zaidi ya madhara yake Hadadi; naye akawachukia Israeli, akamiliki juu ya Shamu. 1 Wafalme 11:25

He was an adversary to Israel all the days of Solomon, besides the mischief that Hadad [did]: and he abhorred Israel, and reigned over Syria.

Na Yeroboamu wa Nebati, Mwefraimu wa Sereda, mtumwa wake Sulemani; ambaye jina lake mamaye aliitwa Serua, mwanamke aliyefiwa na mumewe; yeye naye akainua mkono wake juu ya mfalme. 1 Wafalme 11:26

Jeroboam the son of Nebat, an Ephraimite of Zeredah, a servant of Solomon, whose mother's name was Zeruah, a widow, he also lifted up his hand against the king.

Na hii ndiyo sababu ya yeye kumwinulia mfalme mkono. Sulemani aliijenga Milo, akapafunga palipobomoka pa mji wa baba yake Daudi. 1 Wafalme 11:27

This was the reason why he lifted up his hand against the king: Solomon built Millo, and repaired the breach of the city of David his father.

Na huyo Yeroboamu alikuwa mtu hodari, shujaa; Sulemani akaona ya kuwa kijana huyo ni mtu mwenye bidii, akamweka juu ya kazi yote ya nyumba ya Yusufu. 1 Wafalme 11:28

The man Jeroboam was a mighty man of valor; and Solomon saw the young man that he was industrious, and he gave him charge over all the labor of the house of Joseph.

Ikawa zamani zile Yeroboamu alipokuwa akitoka katika Yerusalemu, nabii Ahiya, Mshiloni, alikutana naye njiani; naye Ahiya amevaa vazi jipya, na hao wawili walikuwa peke yao mashambani. 1 Wafalme 11:29

It happened at that time, when Jeroboam went out of Jerusalem, that the prophet Ahijah the Shilonite found him in the way; now [Ahijah] had clad himself with a new garment; and they two were alone in the field.

Ahiya akalishika lile vazi jipya alilokuwa amelivaa, akalirarua vipande kumi na viwili. 1 Wafalme 11:30

Ahijah laid hold of the new garment that was on him, and tore it in twelve pieces.

Akamwambia Yeroboamu, Twaa wewe vipande kumi, maana Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nitaurarua ufalme, na kuuondoa katika mkono wa Sulemani, nami nitakupa wewe kabila kumi, 1 Wafalme 11:31

He said to Jeroboam, Take ten pieces; for thus says Yahweh, the God of Israel, Behold, I will tear the kingdom out of the hand of Solomon, and will give ten tribes to you

(lakini yeye atakuwa na kabila moja kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi, na kwa ajili ya Yerusalemu mji ule niliouchagua katika miji yote ya kabila za Israeli); 1 Wafalme 11:32

(but he shall have one tribe, for my servant David's sake and for Jerusalem's sake, the city which I have chosen out of all the tribes of Israel);

kwa sababu wameniacha mimi wakaabudu Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni, na Kemoshi, mungu wa Wamoabi, na Milkomu, mungu wa wana wa Amoni wala hawakuenda katika njia zangu, kutenda mema machoni pangu, kuzishika sheria zangu na hukumu zangu, kama Daudi baba yake. 1 Wafalme 11:33

because that they have forsaken me, and have worshiped Ashtoreth the goddess of the Sidonians, Chemosh the god of Moab, and Milcom the god of the children of Ammon; and they have not walked in my ways, to do that which is right in my eyes, and [to keep] my statutes and my ordinances, as did David his father.

Walakini sitauondoa ufalme wote katika mkono wake; lakini nitamfanya awe mkuu siku zote za maisha yake, kwa ajili ya mtumishi wangu Daudi niliyemchagua kwa maana alizishika amri zangu na sheria zangu, 1 Wafalme 11:34

However I will not take the whole kingdom out of his hand; but I will make him prince all the days of his life, for David my servant's sake whom I chose, who kept my commandments and my statutes;

lakini nitauondoa ufalme katika mkono wa mwanawe, nami nitakupa wewe kabila kumi. 1 Wafalme 11:35

but I will take the kingdom out of his son's hand, and will give it to you, even ten tribes.

Nami nitampa mwana wake kabila moja, ili Daudi, mtumishi wangu, apate kuwa na taa siku zote mbele zangu katika Yerusalemu, mji ule niliouchagua niweke jina langu huko. 1 Wafalme 11:36

To his son will I give one tribe, that David my servant may have a lamp always before me in Jerusalem, the city which I have chosen me to put my name there.

Nami nitakutwaa wewe, nawe utatawala kama roho yako inavyotamani, nawe utakuwa mfalme juu ya Israeli. 1 Wafalme 11:37

I will take you, and you shall reign according to all that your soul desires, and shall be king over Israel.

Tena itakuwa, ukiyasikia yote nitakayokuamuru, na kuenda katika njia zangu, na kutenda yaliyo mema machoni pangu, ili kuzishika amri zangu na hukumu zangu kama Daudi mtumishi wangu alivyotenda, basi, nitakuwa pamoja nawe, nitakujengea nyumba iliyo imara, kama nilivyomjengea Daudi, nami nitakupa wewe Israeli. 1 Wafalme 11:38

It shall be, if you will listen to all that I command you, and will walk in my ways, and do that which is right in my eyes, to keep my statutes and my commandments, as David my servant did; that I will be with you, and will build you a sure house, as I built for David, and will give Israel to you.

Tena nitawatesa wazao wa Daudi kwa sababu hii, lakini si daima. 1 Wafalme 11:39

I will for this afflict the seed of David, but not forever.

Basi Sulemani akataka kumwua Yeroboamu, lakini Yeroboamu akaondoka, akakimbilia Misri, kwa Shishaki, mfalme wa Misri, akakaa katika Misri hata wakati wa kufa kwake Sulemani. 1 Wafalme 11:40

Solomon sought therefore to kill Jeroboam; but Jeroboam arose, and fled into Egypt, to Shishak king of Egypt, and was in Egypt until the death of Solomon.

Nayo yaliyosalia ya Sulemani, mambo yake na yote aliyoyafanya, na hekima yake, je! Hayo siyo yaliyoandikwa kitabuni mwa mambo yake Sulemani? 1 Wafalme 11:41

Now the rest of the acts of Solomon, and all that he did, and his wisdom, aren't they written in the book of the acts of Solomon?

Na siku alizotawala Sulemani katika Yerusalemu juu ya Israeli wote zilikuwa miaka arobaini. 1 Wafalme 11:42

The time that Solomon reigned in Jerusalem over all Israel was forty years.

Naye Sulemani akalala na baba zake, akazikwa katika mji wa Daudi baba yake; na Rehoboamu mwanawe akatawala mahali pake. 1 Wafalme 11:43

Solomon slept with his fathers, and was buried in the city of David his father: and Rehoboam his son reigned in his place.