1 Wafalme 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
1 Wafalme 12 (Swahili) 1st Kings 12 (English)

Rehoboamu akaenda Shekemu; maana Israeli wote walikuwa wamekwenda Shekemu, ili kumfanya mfalme. 1 Wafalme 12:1

Rehoboam went to Shechem: for all Israel were come to Shechem to make him king.

Ikawa Yeroboamu mwana wa Nebati alipopata habari (maana alikuwa akaliko Misri, huko alikokimbilia awe mbali na mfalme Sulemani; Yeroboamu akakaa huko Misri, 1 Wafalme 12:2

It happened, when Jeroboam the son of Nebat heard of it (for he was yet in Egypt, where he had fled from the presence of king Solomon, and Jeroboam lived in Egypt,

wakapeleka watu kwenda kumwita); basi Yeroboamu na jamii yote ya Israeli wakaenda, wakamwambia Rehoboamu, wakasema, 1 Wafalme 12:3

and they sent and called him), that Jeroboam and all the assembly of Israel came, and spoke to Rehoboam, saying,

Baba yako alilifanya zito kongwa letu; basi sasa utupunguzie utumwa mzito tuliotumikishwa na baba yako, na lile kongwa zito alilotutwika, nasi tutakutumikia. 1 Wafalme 12:4

Your father made our yoke grievous: now therefore make you the grievous service of your father, and his heavy yoke which he put on us, lighter, and we will serve you.

Akawaambia, Enendeni zenu hata siku ya tatu, kisha mnirudie tena. Watu wakaenda zao. 1 Wafalme 12:5

He said to them, Depart yet for three days, then come again to me. The people departed.

Mfalme Rehoboamu akataka shauri kwa wazee waliokuwa wakisimama mbele ya Sulemani, baba yake, alipokuwa hai, akasema, Mwanipa shauri gani ili niwajibu watu hawa? 1 Wafalme 12:6

King Rehoboam took counsel with the old men, who had stood before Solomon his father while he yet lived, saying, What counsel give you me to return answer to this people?

Wakamwambia wakasema, Ukikubali kuwa mtumishi wa watu hawa leo, na kuwatumikia, na kuwajibu, na kuwapa maneno mazuri, basi watakuwa watumishi wako daima. 1 Wafalme 12:7

They spoke to him, saying, If you will be a servant to this people this day, and will serve them, and answer them, and speak good words to them, then they will be your servants forever.

Lakini akaliacha shauri lile la wazee, walilompa, akataka shauri kwa wale vijana waliokua pamoja naye, na kusimama mbele yake. 1 Wafalme 12:8

But he forsook the counsel of the old men which they had given him, and took counsel with the young men who had grown up with him, who stood before him.

Akawaambia, Mwanipa shauri gani ili tuwajibu watu hawa, waliosema nami, wakinena Utufanyie jepesi kongwa lile alilotutwika baba yako? 1 Wafalme 12:9

He said to them, What counsel do you give, that we may return answer to this people, who have spoken to me, saying, Make the yoke that your father did put on us lighter?

Na wale vijana waliokua pamoja naye wakamwambia, wakasema, Uwaambie hivi watu wale waliokuambia, wakisema, Baba yako alilifanya zito kongwa letu, bali wewe utufanyie jepesi, uwaambie hivi, Kidole changu cha mwisho ni kinene kuliko kiuno cha baba yangu. 1 Wafalme 12:10

The young men who had grown up with him spoke to him, saying, Thus shall you tell this people who spoke to you, saying, Your father made our yoke heavy, but make you it lighter to us; thus shall you speak to them, My little finger is thicker than my father's loins.

Basi kama vile baba yangu alivyowatwika kongwa zito, mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, bali mimi nitawapigeni kwa nge. 1 Wafalme 12:11

Now whereas my father did lade you with a heavy yoke, I will add to your yoke: my father chastised you with whips, but I will chastise you with scorpions.

Basi, Yeroboamu na watu wote wakamfikia Rehoboamu siku ya tatu, kama mfalme alivyoamuru, akisema, Mnirudie siku ya tatu. 1 Wafalme 12:12

So Jeroboam and all the people came to Rehoboam the third day, as the king bade, saying, Come to me again the third day.

Mfalme akawajibu watu wale kwa ukali, akaliacha shauri lile wazee walilompa; 1 Wafalme 12:13

The king answered the people roughly, and forsook the counsel of the old men which they had given him,

akawajibu kama vile walivyomshauri vijana, akasema, Baba yangu alilifanya zito kongwa lenu, bali mimi nitaongeza kongwa lenu; baba yangu aliwapiga kwa mijeledi, bali mimi nitawapigeni kwa nge. 1 Wafalme 12:14

and spoke to them after the counsel of the young men, saying, My father made your yoke heavy, but I will add to your yoke: my father chastised you with whips, but I will chastise you with scorpions.

Basi mfalme hakuwasikia wale watu; maana jambo hili lilitoka kwa Bwana, ili alitimize neno lake, Bwana alilomwambia Yeroboamu mwana wa Nebati kwa kinywa cha Ahiya Mshiloni. 1 Wafalme 12:15

So the king didn't listen to the people; for it was a thing brought about of Yahweh, that he might establish his word, which Yahweh spoke by Ahijah the Shilonite to Jeroboam the son of Nebat.

Basi Israeli wote walipoona ya kuwa mfalme hakuwasikia, hao watu walimjibu mfalme, wakasema, Tuna sehemu gani katika Daudi? Wala hatuna urithi katika mwana wa Yese. Haya! Nendeni zenu hemani kwenu, enyi Israeli; sasa itunze nyumba yako mwenyewe, Ee Daudi. Hivyo Israeli wakaenda zao hemani kwao. 1 Wafalme 12:16

When all Israel saw that the king didn't listen to them, the people answered the king, saying, What portion have we in David? neither have we inheritance in the son of Jesse: to your tents, Israel: now see to your own house, David. So Israel departed to their tents.

Lakini kwa habari za wana wa Israeli waliokaa katika miji ya Yuda, Rehoboamu aliwatawala wao. 1 Wafalme 12:17

But as for the children of Israel who lived in the cities of Judah, Rehoboam reigned over them.

Ndipo mfalme Rehoboamu akampeleka Adoramu, aliyekuwa juu ya shokoa, nao Israeli wote wakampiga kwa mawe hata akafa. Mfalme Rehoboamu akafanya haraka kupanda katika gari, ili akimbilie Yerusalemu. 1 Wafalme 12:18

Then king Rehoboam sent Adoram, who was over the men subject to forced labor; and all Israel stoned him to death with stones. King Rehoboam made speed to get him up to his chariot, to flee to Jerusalem.

Hivyo Israeli wakaasi juu ya nyumba ya Daudi hata leo. 1 Wafalme 12:19

So Israel rebelled against the house of David to this day.

Ikawa, Israeli wote waliposikia ya kwamba Yeroboamu amerudi, wakapeleka watu wakamwita aje mkutanoni, wakamfanya mfalme juu ya Israeli wote; wala hapakuwa na mtu aliyeshikamana na nyumba ya Daudi, ila kabila ya Yuda peke yake. 1 Wafalme 12:20

It happened, when all Israel heard that Jeroboam was returned, that they sent and called him to the congregation, and made him king over all Israel: there was none who followed the house of David, but the tribe of Judah only.

Hata Rehoboamu alipofika Yerusalemu, akakusanya nyumba yote ya Yuda, pamoja na kabila ya Benyamini, watu wateule mia na themanini elfu, waliokuwa watu wa vita, ili wapigane na nyumba ya Israeli, waurudishe ufalme tena kwa Rehoboamu mwana wa Sulemani. 1 Wafalme 12:21

When Rehoboam was come to Jerusalem, he assembled all the house of Judah, and the tribe of Benjamin, a hundred and eighty thousand chosen men, who were warriors, to fight against the house of Israel, to bring the kingdom again to Rehoboam the son of Solomon.

Lakini likaja neno la Mungu kwa Shemaya mtu wa Mungu, kusema, 1 Wafalme 12:22

But the word of God came to Shemaiah the man of God, saying,

Mwambie Rehoboamu mwana wa Sulemani, mfalme wa Yuda, na jamaa yote ya Yuda na Benyamini, na watu waliosalia, ukisema, 1 Wafalme 12:23

Speak to Rehoboam the son of Solomon, king of Judah, and to all the house of Judah and Benjamin, and to the rest of the people, saying,

Bwana asema hivi, Msiende, wala msipigane na ndugu zenu wana wa Israeli; rudini kila mtu nyumbani kwake; kwa kuwa jambo hili limetoka kwangu. Basi, wakalisikiliza neno la Bwana, wakarudi, wakaenda zao, sawasawa na neno la Bwana. 1 Wafalme 12:24

Thus says Yahweh, You shall not go up, nor fight against your brothers the children of Israel: return every man to his house; for this thing is of me. So they listened to the word of Yahweh, and returned and went their way, according to the word of Yahweh.

Ndipo Yeroboamu akajenga Shekemu katika milima ya Efraimu, akakaa huko. Akatoka huko akajenga Penueli. 1 Wafalme 12:25

Then Jeroboam built Shechem in the hill-country of Ephraim, and lived therein; and he went out from there, and built Penuel.

Yeroboamu akasema moyoni mwake, Basi ufalme utairudia nyumba ya Daudi. 1 Wafalme 12:26

Jeroboam said in his heart, Now will the kingdom return to the house of David:

Kama watu hawa wakipanda kwenda kutoa dhabihu katika nyumba ya Bwana huko Yerusalemu, ndipo mioyo ya watu hawa itamrudia bwana wao, yaani Rehoboamu, mfalme wa Yuda; nao wataniua mimi, na kumrudia Rehoboamu, mfalme wa Yuda. 1 Wafalme 12:27

if this people go up to offer sacrifices in the house of Yahweh at Jerusalem, then will the heart of this people turn again to their lord, even to Rehoboam king of Judah; and they will kill me, and return to Rehoboam king of Judah.

Kwa hiyo mfalme akafanya shauri, akafanyiza ng'ombe wawili wa dhahabu, akawaambia watu, Ni vigumu kwenu kupanda kwenda Yerusalemu; tazama, hii ndiyo miungu yenu, enyi Israeli, iliyowapandisha kutoka nchi ya Misri. 1 Wafalme 12:28

Whereupon the king took counsel, and made two calves of gold; and he said to them, It is too much for you to go up to Jerusalem: see your gods, Israel, which brought you up out of the land of Egypt.

Akamweka mmoja katika Betheli, na wa pili akamweka katika Dani. 1 Wafalme 12:29

He set the one in Bethel, and the other put he in Dan.

Jambo hili likawa dhambi, maana watu walikwenda kuabudu mbele ya kila mmoja, hata huko Dani. 1 Wafalme 12:30

This thing became a sin; for the people went [to worship] before the one, even to Dan.

Tena akafanya nyumba za mahali pa juu, akafanya na watu wo wote, watu wasio wa wana wa Lawi, kuwa makuhani. 1 Wafalme 12:31

He made houses of high places, and made priests from among all the people, who were not of the sons of Levi.

Yeroboamu akaamuru kushika sikukuu katika mwezi wa nane, siku ya kumi na tano ya mwezi, mfano wa sikukuu iliyokuwa katika Yuda, akapanda juu ili kuiendea madhabahu. Akafanya vivyo katika Betheli akiwatolea dhabihu wale ng'ombe aliowafanya; akawaweka katika Betheli wale makuhani wa mahali pa juu alipokuwa amepafanya. 1 Wafalme 12:32

Jeroboam ordained a feast in the eighth month, on the fifteenth day of the month, like the feast that is in Judah, and he went up to the altar; so did he in Bethel, sacrificing to the calves that he had made: and he placed in Bethel the priests of the high places that he had made.

Akatoa dhabihu juu ya ile madhabahu aliyoifanya katika Betheli, siku ya kumi na tano ya mwezi wa nane, mwezi aliouwaza moyoni mwake mwenyewe; akawaamuru wana wa Israeli waishike sikukuu hiyo, akapanda kuiendea madhabahu, ili kufukiza uvumba. 1 Wafalme 12:33

He went up to the altar which he had made in Bethel on the fifteenth day in the eighth month, even in the month which he had devised of his own heart: and he ordained a feast for the children of Israel, and went up to the altar, to burn incense.