1 Wafalme Mlango 4 1st Kings

1 Wafalme 4:1

Basi mfalme Sulemani akawa mfalme juu ya Israeli wote.

1 Wafalme 4:2

Na hawa ndio wakuu aliokuwa nao; Azaria mwana wa Sadoki, kuhani,

1 Wafalme 4:3

Elihorefu na Ahiya, wana wa Shausha, waandishi; Yehoshafati mwana wa Ahiludi mwenye kuandika tarehe;

1 Wafalme 4:4

na Benaya mwana wa Yehoyada alikuwa juu ya jeshi; na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani;

1 Wafalme 4:5

na Azaria mwana wa Nathani alikuwa juu ya maakida; na Zabudi mwana wa Nathani alikuwa kuhani, rafiki wake mfalme.

1 Wafalme 4:6

Na Ahishari alikuwa juu ya nyumba; na Adoramu mwana wa Abda alikuwa juu ya shokoa.

1 Wafalme 4:7

Sulemani alikuwa na maakida kumi na wawili juu ya Israeli wote, walioleta chakula cha mfalme na nyumba yake; kila mtu alikuwa na mwezi mmoja katika mwaka kuleta chakula.

1 Wafalme 4:8

Na haya ndiyo majina yao. Mwana wa Huri, mlimani mwa Efraimu.

1 Wafalme 4:9

Mwana wa Dekari, kutoka Makasi, na Shaalbimu na Bethshemeshi na Elon-beth-hanani.

1 Wafalme 4:10

Mwana wa Hesedi, katika Arubothi; na Soko ilikuwa kwake na nchi yote ya Heferi.

1 Wafalme 4:11

Mwana wa Abinadabu katika Nafath-dori yote; ndiye aliyekuwa naye Tafathi binti Sulemani kuwa mke wake.

1 Wafalme 4:12

Baana mwana wa Ahiludi, katika Taanaki na Megido, na Beth-sheani yote, iliyo kando ya Sarethani, chini ya Yezreeli, tangu Beth-sheani mpaka Abel-mehola, hata kupita Yokmeamu.

1 Wafalme 4:13

Mwana wa Geberi katika Ramoth-gileadi; na kwake ilikuwa miji ya Yairi mwana wa Manase iliyomo Gileadi; na kwake ilikuwa wilaya ya Argobu, iliyomo Bashani, miji mikubwa sitini yenye kuta na makomeo ya shaba.

1 Wafalme 4:14

Ahinadabu mwana wa Ido, katika Mahanaimu.

1 Wafalme 4:15

Ahimaasi, katika Naftali; naye ndiye aliyemwoa Basemathi binti Sulemani.

1 Wafalme 4:16

Baana mwana wa Hushai, katika Asheri na Bealothi.

1 Wafalme 4:17

Yehoshafati mwana wa Parua, katika Isakari.

1 Wafalme 4:18

Shimei mwana wa Ela, katika Benyamini.

1 Wafalme 4:19

Geberi mwana wa Uri, katika nchi ya Gileadi, nchi ya Sihoni mfalme wa Waamori, na Ogu mfalme wa Bashani; naye alikuwa akida wa pekee katika nchi hiyo.

1 Wafalme 4:20

Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani kwa wingi, wakila, na kunywa, na kufurahi.

1 Wafalme 4:21

Sulemani akatawala juu ya falme zote, toka Mto mpaka nchi ya Wafilisti, na hata mpaka wa Misri; walimletea tunu, na kumtumikia Sulemani siku zote za maisha yake.

1 Wafalme 4:22

Na vyakula vya Sulemani vya siku moja vilikuwa kori therathini za unga wa mzuri, na kori sitini za ngano.

1 Wafalme 4:23

na ng'ombe kumi walionona, na ng'ombe ishirini za malisho, na kondoo mia, pamoja na ayala, na paa, na kulungu, na kuku walionona.

1 Wafalme 4:24

Kwani alikuwa akitawala nchi yote upande huu wa Mto, toka Tifsa mpaka Gaza, juu ya wafalme wote wa upande huu wa Mto; naye alikuwa na amani pande zake zote.

1 Wafalme 4:25

Yuda na Israeli wakakaa salama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, tokea Dani mpaka Beer-sheba, siku zote za Sulemani.

1 Wafalme 4:26

Tena Sulemani alikuwa na mabanda ya farasi arobaini elfu kwa magari yake, na wapandao farasi kumi na mbili elfu.

1 Wafalme 4:27

Na maakida wale wakaleta chakula kwa mfalme Sulemani na kwa wote walioijia meza ya mfalme Sulemani, kila mtu katika mwezi wake, kisipunguke kitu.

1 Wafalme 4:28

Shayiri pia na majani kwa farasi, na kwa wanyama wenye mbio, wakaleta mahali walipokuwapo, kila mtu kwa kadiri ya kazi yake.

1 Wafalme 4:29

Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani.

1 Wafalme 4:30

Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri.

1 Wafalme 4:31

Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka.

1 Wafalme 4:32

Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano.

1 Wafalme 4:33

Akanena habari za miti tangu mwerezi ulioko Lebanoni hata hisopo umeao ukutani; pia akanena habari za wanyama, na za ndege, na vitambaavyo, na samaki.

1 Wafalme 4:34

Wakaja wa mataifa yote ili waisikie hekima ya Sulemani, toka wafalme wote wa ulimwengu, waliokuwa wamepata habari za hekima yake.