Sifa Lyrics

Mwana by Joel Lwaga cover art

Joel Lwaga - Mwana Lyrics

Artist:
Joel Lwaga
Album:
Thamani - EP
Official Release:
07 Aug 2020

Lyrics

Nilifikiri moyoni mwangu
Nikamwambia Baba 
Nipe sehemu ya mali yangu


Nikaondoka nyumbani kwetu
Nikaenda mbali
Nikatumia mali yote


Nikacheza na muda
Nikaruhusu mali initawale
Eeh eeh


Maisha yakawa magumu 
Nikafikiri moyoni mwangu
Nitaenda wapi? 


Eeh Nyumbani
Nimeshaondoka aah
Nitafanya nini mimi?
Mwana mpotevu


Aah.. aah


Nilipozingatia
Moyoni mwangu mimi
Nikaona bora nirudi kwa baba


Yanini kuendelea 
Kula na nguruwe hapa
Wakati watumishi wa baba 
Nyumbani wanakula na kusaza


Oooh nikaona bora nirudi
Kwa baba nitamwambia nimekosa
Ju ya mbingu na mbele yako
Sistahili tena kuitwa mwanao
(Oooh oooh)


Lakini baba aliponiona
Kutoka mbali akanikimbilia
Akanivika mavazi mazuri
Na pete kidoleni mwangu 
(Aah aah)


Akanikumbatia 
Na kunibusu shingoni
Akaamuru sherehe ifanyike


Maana mwanae aliyekufa
Sasa anaishi tena
Mwanae aliyepotea
Amerudi


Akasema sitakufanya
Kuwa mmoja wa wajakazi wangu
Wewe ni mwanangu aah
Wewe ni mwanangu (Aah mmmh..)


Video