Sifa Lyrics

Muda by Joel Lwaga cover art

Joel Lwaga - Muda Lyrics

Artist:
Joel Lwaga
Album:
Muda - Single
Official Release:
16 May 2025

Lyrics

Verse 1


Jitu
Ni kweli naonekana niko Nyuma
Kila kukicha watu washamiri, kwa magari majumba
Juzi juzi wengine tulikuwa nao sawa tu
Ila kwa sasa si wenzangu tena, siwagusi hata nukta
Ni kama niko duniani kuwasindikiza wao
Usipotulia unaweza sema Mungu ni wa peke yao
Ila maisha ni kama foleni inajongea Mdogo Mdogo
Mungu wao ndio Mungu wangu, ndio wa Isaka na Yakobo


Pre-Chorus


Wakati na Bahati huwapata wote
Zamu yangu itafika, Wacha niingojee
La maana ni uhai, Mungu ni wote
Ndio anapanga aanze nani, nani afuate


Chorus


Yani ni suala la Muda
MUDA, nipeni tu MUDA
Mungu ni wa wote jamani
MUDA, nipeni tu MUDA
Yani ni suala la Muda
MUDA, nipeni tu MUDA
Kikubwa niko kwa foleni
MUDA, nipeni tu MUDA


Verse 2


Najua wengi husema kila asiyenacho hunyenyekea
Ila nimemwomba Mungu nisibadilike Akinipea
Vile nawaona Watu na kuwachukulia nikiwa Sina
Nisije jiona Mungu mtu pindi mambo yakininyookea
Najitahidi kugawana hichi kidogo Nilichonacho na wenzangu
Nimejifunza kwamba kutoa ni Moyo siyo mpaka kiwe kingi changu
Kwenye sadaka sinaga visingizio hio ni kama Pai kwangu
Hata nikiwa sina kabisa siku hyo, Mungu anaujua Moyo wangu


Pre-Chorus (Repeat)


Wakati na Bahati huwapata wote
Zamu yangu itafika, Wacha niingojee
La maana ni uhai, Mungu ni wote
Ndio anapanga aanze nani, nani afuate


Chorus (Repeat)


Yani ni suala la Muda
MUDA, nipeni tu MUDA
Mungu ni wa wote jamani
MUDA, nipeni tu MUDA
Yani ni suala la Muda
MUDA, nipeni tu MUDA
Kikubwa niko kwa foleni
MUDA, nipeni tu MUDA
Yani ni suala la Muda
MUDA, nipeni tu MUDA
Mungu ni mwaminifu
MUDA, nipeni tu MUDA


Bridge


Maana maisha ni foleni
Kila siku inatembea pole pole
Namwamini Mungu
ipo siku nitafanikiwa
Maana maisha ni foleni
Kila siku inatembea pole pole
Namwamini Mungu
ipo siku nitafanikiwa


Outro


Kweli ni suala la Muda
MUDA, nipeni tu MUDA
Mungu ni mwaminifu jamani!
MUDA, nipeni tu MUDA


Video

Meaning & Inspiration

“Muda,” which means “Time,” by Joel Lwaga is a Swahili song about waiting for one’s turn. The first verse admits to feeling left behind while others prosper with cars and houses, then adds that God is the same God of Isaac and Jacob, so there is no reason to think He belongs only to them. Life is compared to a queue that moves forward slowly.

The pre-chorus says that time and chance come to all and that the singer will wait for his turn, since God decides who goes first. The chorus is a plain request, “nipeni tu muda” (just give me time). The second verse adds that the singer prays not to change when blessings arrive, shares even a little, and says giving comes from the heart and not from abundance. That is close to 2 Corinthians 9:7 and Exodus 3:6.

The bridge repeats trust in God and the belief that success will come one day, echoing Ecclesiastes 9:11 and Habakkuk 2:3. The song’s message is patience, humility, and generosity while waiting.

Related Scripture