Sifa Lyrics

Hatua Kwa Hatua by Mercy Masika + Rebekah Dawn cover art

Mercy Masika + Rebekah Dawn - Hatua Kwa Hatua Lyrics

Artist:
Mercy Masika + Rebekah Dawn
Album:
This Chosen Road
Official Release:
02 Oct 2021

Lyrics

Sauti nyingi zinanizingira
Mawaitha mingi, njia nyingi
Lakini najua Sauti moja tu la kufuata
Sina Mchungaji mwingine ila Yesu


Hata wengine wakiteleza njiani
Nitazidi kuwa mwaminifu Kwake
Nitaamini neno Lake
Hajawahi kunipotosha


Hatua kwa hatua, nitaendelea
Mungu mbele yangu, nitamfuata
Hakuna njia ingine najua
Hatua kwa hatua, nitaendelea


Njia zake zaaminika
Neno lake ni la kweli
Kwa hilo nitasimama
Sitainamia dunia
Sina Mwongozo mwingine ila Yesu


Sijawahi ona mwenye haki ameachwa
Waliokuchagua hawajawahi kujuta
Kwa hivyo nitazidii Nawe, hata nisipoelewa


Hatua kwa hatua, nitaendelea
Mungu mbele yangu, nitamfuata
Hakuna njia ingine najua
Hatua kwa hatua, nitaendelea


Oooh, nitakufuata
Nitakufuata Yesu, Kiongozi mwema


Mkombozi, sina mwingine
Mfalme, sina mwingine
Mwenye Enzi, sina mwingine
Msaidizi, sina mwingine
Mponyaji, sina mwingine
Mtetezi, sina mwingine
Mwokozi, sina mwingine
Mfariji, sina mwingine


Hatua kwa hatua, nitaendelea
Mungu mbele yangu, nitamfuata
Hakuna njia ingine najua


Video