Nitakuwa Na Wewe

Nitakuwa Na Wewe Lyrics

Kama ni kukupenda niko sawa 
Kuwa nawe niko sawa 
Niko tayari walimwengu wanitenge 
Kama kuwa nawe ni kushamba 
Kuishi nawe si kujanja 
Niko tayari walimwengu wanicheke  .

Sababu ninaelewa nikiwa na wewe napata raha 
Ninaelewa kuishi na wewe ni furaha 
Ninelewa iyee ninaelewa oooh .

Hata iweje wafanyeje wasemeje 
Mimi sitakuacha 
Hata iweje wafanyeje wasemeje mimi sitakuacha 
Nitakuwa na wewe (iyee) 
Nikae na wewe (iyee) 
Nitembee na wewe (milele) 
Mwokozi wangu  .

Maneno neno ya wanadamu yanavunja moyo yanapotosha 
Dhumuni lake ni kunitenga mbali nawe 
Kwa damu uliyo mwaga msalabani ili mimi niwe wathamani 
Sio rahisi kwa mwanadamu kunitenga nawe   .

Kwangu ninaelewa nikiwa na wewe napata raha 
Ninaelewa kuishi na wewe ni furaha 
Ninelewa iyee ninaelewa oooh  .

Hata iweje wafanyeje wasemeje 
Mimi sitakuacha 
Hata iweje wafanyeje wasemeje mimi sitakuacha 
Nitakuwa na wewe (iyee) 
Nikae na wewe (iyee) 
Nitembee na wewe (milele) 
Mwokozi wangu  .

Moyo wangu nimekukabidhi 
Na mwili wangu hekalu lako 
Wewe Bwana nimekubali ukae nami 
Nitakuwa nawe siku zote 
Milele na milele sitokuacha 
Nitakubali kuacha vyote nikufuate wewe 
Sababu ninaelewa, ninaelewa 
Ninaelewa  .

Nitakuwa na wewe (iyee) 
Nikae na wewe (iyee) 
Nitembee na wewe (milele) 
Mwokozi wangu 


Top Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Nitakuwa Na Wewe:

0 Comments/Reviews