Sifa Lyrics

Mbali Sana by Beda Andrew cover art

Beda Andrew - Mbali Sana Lyrics

Artist:
Beda Andrew

Lyrics

Na na na na... 


Nalikuwa sijiwezi unyonge ulinilemea 


Sikuwa na tumaini ya mbele kuendelea 


Imani ilififia sikuona kabisa


Kama moja ya nyenzo iliyotikisika aah 


Nalikosa tabasamu usoni 


Tegemeo sikuona maishani 


Nikashindwa endelea mbele 


Hali iliyofanya nikwame kule 


Ulikonitoa ni mbali sana 


Ni kweli umenikomboa nashukuru sana 


Ulikonitoa ni mbali sana 


Ukanikomboa na zile laana 


Mbali sana, mbali sana 


Mbali sana nashukuru Bwana 


Uliona haiko shwari mimi kupotea njia 


Sijui namna gani uliwaza ukanihurumia 


Nalifanya nia jangwa mvua kutonyeshe 


Nami mche mbichi maji yalinikaukia 


Shida mateso sina tena, yamewekwa nyuma 


Mimi wa Yesu mwingine sina 


Wa kurudisha nyuma 


Wakati wa kuokolewa umekubalika 


Kwa haki na ushupavu wake ukatibitika 


Ulikonitoa ni mbali sana 


Ni kweli umenikomboa nashukuru sana 


Ulikonitoa ni mbali sana 


Ukanikomboa na zile laana 


Mbali sana, mbali sana 


Mbali sana nashukuru Bwana 


oooh oh oh oooh 


...


Video