Sifa Lyrics

Nguvu za Mungu by Beda Andrew cover art

Beda Andrew - Nguvu za Mungu Lyrics

Artist:
Beda Andrew

Lyrics

Rafiki hivi unavyoniona
Ni kwa neema tu
Na hata uzima nilio nao
Ni upendeleo tu


Na kufika hapa sio sababu ya kuwa
Mimi ni mwema sana (Kuliko wale)
Tena natambua kama si wake mkono
Ningeshatumbukia shimoni na nipotee


Ninalindwa, kwa nguvu za Mungu
Ni kwa nguvu za Mungu
Si kwa ujanja wala akili zangu
Ila ni kwa nguvu za Mungu


Ninalindwa, kwa nguvu za Mungu
Ni kwa nguvu za Mungu
Si kwa ujanja wala akili zangu
Ila ni kwa nguvu za Mungu


Nia ya mwovu ni kutaka ona mi naangamia
Kusudi la Mungu maishani mwangu nisipate timia 
Anatega mitego, ili mradi kuniangamiza
Kunimaliza kunipoteza, ila Yahweh ananilinda


Nimeokolewa na ajali
Magonjwa na kila hatari
Mpaka sasa nipo hai
Nakushukuru jemedari


Uzima wangu, hauko mikoni mwangu
Uzima wangu, uko mikononi mwake


Kwa nguvu za Mungu
Ni kwa nguvu za Mungu
Kwa nguvu za Mungu
Ni kwa nguvu za Mungu


Ni kwa nguvu za Mungu
Si kwa ujanja wala akili zangu
Ila ni kwa nguvu za Mungu


Ninalindwa, kwa nguvu za Mungu
Ni kwa nguvu za Mungu
Si kwa ujanja wala akili zangu
Ila ni kwa nguvu za Mungu


Ninalindwa, kwa nguvu za Mungu
Ni kwa nguvu za Mungu
Si kwa ujanja wala akili zangu


Ni kwa neema tu za aliye juu
Aliye juu ni Mungu mkuu
Ni kwa neema tu za aliye juu
Aliye juu ni Mungu mkuu


Ni kwa neema tu za aliye juu
Aliye juu ni Mungu mkuu
Ni kwa neema tu za aliye juu
Aliye juu ni Mungu mkuu


Kwa nguvu za Mungu
Ni kwa nguvu za Mungu
Si kwa ujanja wala akili zangu
Ila ni kwa nguvu za Mungu


Video