Sifa Lyrics

Asante by Angel Benard cover art

Angel Benard - Asante Lyrics

Artist:
Angel Benard

Lyrics

Ngome imara, mwenye haki
Hukukimbilia na kuipata salama
Ndiwe Mungu, mwenye nguvu ya kutoa
Na nguvu ya kutwaa
Wewe pekee ndiwe Mungu


Hekima yako inazidi hekima ya dunia
Na ujuzi wa wanadamu
Hofu iliinuka ikakutana na wewe
Ikafungwa kinywa tumeinuka
Taabu za dunia zinapokutana na wewe
Tunashinda yote tunainuka


Asante, wewe ni Mungu usiyeshindwa
Asante, wewe ni Mungu usiyeshindwa


Macho yangu yameona 
Mkono wa Bwana unaotenda mema
Dunia yanyamaza, hekima zimekoma
Utaalamu umenyamaza, ujuzi umeshindwa


Damu inanena mema
Na Mungu uliyeyatenda hayo
Ndiwe utatenda yale
Tuko salama nawe


Jamaa taabu za dunia
Zikikutana na mfalme
Zinafichwa nguvu tunainuka
Hio hofu ya maisha
Ikikutana na Bwana
Inafungwa kinywa tunainuka


Asante, wewe ni Mungu usiyeshindwa
Asante, wewe ni Mungu usiyeshindwa


Hao wanataja magari
Wale wanazisifu mali
Sisi twakutaja wewe
Mungu usiyeshindwa


Hao wanataja magari
Wale wanazisifu mali
Sisi twakutaja wewe
Mungu usiyeshindwa


Hao wanataja magari
Wale wanazisifu mali
Sisi twakutaja wewe
Mungu usiyeshindwa


Hao wanataja magari
Wale wanazisifu mali
Sisi twakutaja wewe
Mungu usiyeshindwa


Asante, wewe ni Mungu usiyeshindwa
Asante, wewe ni Mungu usiyeshindwa
Asante, wewe ni Mungu usiyeshindwa
Asante, wewe ni Mungu usiyeshindwa


Video