1
Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi.
Then Jesus called the Twelve together and gave them power and authority over all demons, and power to cure diseases.
2
Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa.
And He sent them out to proclaim the kingdom of God and to heal the sick.
3
Akawaambia, Msichukue kitu kwa safari yenu, fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala mmoja wenu asiwe na kanzu mbili.
“Take nothing for the journey,” He told them, “no staff, no bag, no bread, no money, no second tunic.
4
Na nyumba yo yote mtakayoingia kaeni humo, mpaka mtoke mjini.
Whatever house you enter, stay there until you leave that area.
5
Na wale wasiowakaribisha, mtokapo katika mji huo, yakung'uteni hata mavumbi ya miguuni mwenu, kuwa ushuhuda juu yao.
If anyone does not welcome you, shake the dust off your feet when you leave that town, as a testimony against them.”
6
Wakaenda, wakazunguka katika vijiji, wakihubiri injili, na kupoza watu kila mahali.
So they set out and went from village to village, preaching the gospel and healing people everywhere.
7
Na Herode mfalme akasikia habari za yote yaliyotendeka, akafadhaika kwa sababu watu wengine walisema ya kwamba Yohana amefufuka katika wafu,
When Herod the tetrarch heard about all that was happening, he was perplexed. For some were saying that John had risen from the dead,
8
na wengine ya kwamba Eliya ametokea, na wengine ya kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.
others that Elijah had appeared, and still others that a prophet of old had arisen.
9
Lakini Herode akasema, Yohana nilimkata kichwa; basi ni nani huyu ambaye ninasikia mambo haya juu yake? Akataka kumwona.
“I beheaded John,” Herod said, “but who is this man I hear such things about?” And he kept trying to see Jesus.
10
Basi wale mitume waliporudi walimweleza mambo yote waliyoyatenda; akawachukua, akaenda nao faraghani mpaka mji mmoja uitwao Bethsaida.
Then the apostles returned and reported to Jesus all that they had done. Taking them away privately, He withdrew to a town called Bethsaida.
11
Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa.
But the crowds found out and followed Him. He welcomed them and spoke to them about the kingdom of God, and He healed those who needed healing.
12
Na jua likaanza kushuka; wakamwendea wale Thenashara, wakamwambia, Uage mkutano, ili waende katika vijiji na mashamba ya kandokando wapate mahali pa kulala na vyakula, maana hapa tulipo ni nyika tupu.
As the day neared its end, the Twelve came to Jesus and said, “Dismiss the crowd so they can go to the surrounding villages and countryside for lodging and provisions. For we are in a desolate place here.”
13
Akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakasema, Hatuna kitu zaidi ya mikate mitano na samaki wawili, tusipokwenda tukawanunulie watu hawa wote vyakula.
But Jesus told them, “You give them something to eat.” “We have only five loaves of bread and two fish,” they answered, “unless we go and buy food for all these people.”
14
Kwa kuwa wanaume waliokuwako walipata kama elfu tano. Akawaambia wanafunzi wake, Waketisheni watu kwa safu, kila safu watu hamsini.
(There were about five thousand men.) He told His disciples, “Have them sit down in groups of about fifty each.”
15
Wakafanya hivyo, wakawaketisha wote.
They did so, and everyone was seated.
16
Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi wake ili wawaandikie mkutano.
Taking the five loaves and the two fish and looking up to heaven, Jesus spoke a blessing and broke them. Then He gave them to the disciples to set before the people.
17
Wakala, wakashiba wote; na katika vile vipande vilivyowabakia walikusanya vikapu kumi na viwili.
They all ate and were satisfied, and the disciples picked up twelve basketfuls of broken pieces that were left over.
18
Ikawa alipokuwa akisali kwa faragha, wanafunzi wake walikuwapo pamoja naye, akawauliza, Je! Makutano hao wanasema ya kuwa mimi ni nani?
One day as Jesus was praying in private and the disciples were with Him, He questioned them: “Who do the crowds say I am?”
19
Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini wengine, Eliya; na wengine kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka.
They replied, “Some say John the Baptist; others say Elijah; and still others, that a prophet of old has arisen.”
20
Akawaambia, Nanyi mwasema ya kwamba mimi ni nani? Petro akamjibu akasema, Ndiwe Kristo wa Mungu.
“But what about you?” Jesus asked. “Who do you say I am?” Peter answered, “The Christ of God.”
21
Akawaonya, akawakataza wasimwambie mtu neno hilo;
Jesus strictly warned them not to tell this to anyone.
22
akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka.
“The Son of Man must suffer many things,” He said. “He must be rejected by the elders, chief priests, and scribes, and He must be killed and on the third day be raised to life.”
23
Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.
Then Jesus said to all of them, “If anyone wants to come after Me, he must deny himself and take up his cross daily and follow Me.
24
Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha.
For whoever wants to save his life will lose it, but whoever loses his life for My sake will save it.
25
Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe?
What does it profit a man to gain the whole world, yet lose or forfeit his very self?
26
Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu.
If anyone is ashamed of Me and My words, the Son of Man will be ashamed of him when He comes in His glory and in the glory of the Father and of the holy angels.
27
Nami nawaambia kweli, Wapo katika hawa wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata wauone kwanza ufalme wa Mungu.
But I tell you truly, some who are standing here will not taste death before they see the kingdom of God.”
28
Baada ya maneno hayo yapata siku nane, aliwatwaa Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani ili kuomba.
About eight days after Jesus had said these things, He took with Him Peter, John, and James, and went up on a mountain to pray.
29
Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimeta-meta.
And as He was praying, the appearance of His face changed, and His clothes became radiantly white.
30
Na tazama, watu wawili walikuwa wakizungumza naye, nao ni Musa na Eliya;
Suddenly two men, Moses and Elijah, began talking with Jesus.
31
walioonekana katika utukufu, wakanena habari za kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemu.
They appeared in glory and spoke about His departure, which He was about to accomplish at Jerusalem.
32
Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na usingizi; lakini walipokwisha amka waliuona utukufu wake, na wale wawili waliosimama pamoja naye.
Meanwhile Peter and his companions were overcome by sleep, but when they awoke, they saw Jesus’ glory and the two men standing with Him.
33
Ikawa hao walipokuwa wakijitenga naye, Petro alimwambia Yesu, Bwana mkubwa, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu; kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya; hali hajui asemalo.
As Moses and Elijah were leaving, Peter said to Jesus, “Master, it is good for us to be here. Let us put up three shelters—one for You, one for Moses, and one for Elijah.” (He did not know what he was saying.)
34
Alipokuwa akisema hayo, lilitokea wingu likawatia uvuli, wakaogopa walipoingia katika wingu hilo.
While Peter was speaking, a cloud appeared and enveloped them, and they were afraid as they entered the cloud.
35
Sauti ikatoka katika wingu, ikisema, Huyu ni Mwanangu, mteule wangu, msikieni yeye.
And a voice came from the cloud, saying, “This is My Son, whom I have chosen. Listen to Him!”
36
Na sauti hiyo ilipokwisha, Yesu alionekana yu peke yake. Nao wakanyamaza, wasitangaze kwa mtu siku zile lo lote katika hayo waliyoyaona.
After the voice had spoken, only Jesus was present with them. The disciples kept this to themselves, and in those days they did not tell anyone what they had seen.
37
Ikawa siku ya pili yake, waliposhuka mlimani, mkutano mkubwa ulikutana naye.
The next day, when they came down from the mountain, Jesus was met by a large crowd.
38
Na tazama, mtu mmoja katika mkutano alipaza sauti, akisema, Mwalimu, nakuomba umwangalie mwanangu; kwa kuwa yeye ni mwanangu pekee.
Suddenly a man in the crowd cried out, “Teacher, I beg You to look at my son, for he is my only child.
39
Na tazama, pepo humpagaa, naye mara hupiga kelele; tena humtia kifafa, huku anatokwa na povu, wala hamwachi ila kwa shida, akimchubua-chubua.
A spirit keeps seizing him, and he screams abruptly. It throws him into convulsions so that he foams at the mouth. It keeps mauling him and rarely departs from him.
40
Nikawasihi wanafunzi wako wamtoe, wasiweze.
I begged Your disciples to drive it out, but they were unable.”
41
Yesu akajibu akasema, Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka, nitakaa nanyi na kuwachukulia hata lini? Mlete mwanao hapa.
“O unbelieving and perverse generation!” Jesus replied. “How long must I remain with you and put up with you? Bring your son here.”
42
Alipokuwa katika kumwendea, pepo akambwaga chini, akamtia kifafa. Yesu akamkemea pepo mchafu, akamponya mtoto, akamrudishia babaye.
Even while the boy was approaching, the demon slammed him to the ground in a convulsion. But Jesus rebuked the unclean spirit, healed the boy, and gave him back to his father.
43
Wote wakashangaa, wakiuona ukuu wa Mungu. Nao walipokuwa wakiyastaajabia mambo yote aliyoyafanya, aliwaambia wanafunzi wake,
And they were all astonished at the greatness of God. While everyone was marveling at all that Jesus was doing, He said to His disciples,
44
Yashikeni maneno haya masikioni mwenu, kwa kuwa Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu.
“Let these words sink into your ears: The Son of Man is about to be delivered into the hands of men.”
45
Lakini hawakulifahamu neno lile, likafichwa kwao wasilitambue; wakaogopa kumwuliza maana yake neno lile.
But they did not understand this statement. It was veiled from them so that they could not comprehend it, and they were afraid to ask Him about it.
46
Wakaanza kuhojiana, ni nani atakayekuwa mkubwa miongoni mwao.
Then an argument started among the disciples as to which of them would be the greatest.
47
Naye Yesu alipotambua mawazo ya mioyo yao, alitwaa mtoto mdogo akamweka karibu naye,
But Jesus, knowing the thoughts of their hearts, had a little child stand beside Him.
48
akawaambia, Ye yote atakayempokea mtoto huyu kwa jina langu anipokea mimi; na ye yote atakayenipokea mimi ampokea yeye aliyenituma. Kwa kuwa aliye mdogo miongoni mwenu nyote huyo ndiye mkubwa.
And He said to them, “Whoever welcomes this little child in My name welcomes Me, and whoever welcomes Me welcomes the One who sent Me. For whoever is the least among all of you, he is the greatest.”
49
Yohana akajibu akamwambia; Bwana mkubwa, tuliona mtu anatoa pepo kwa jina lako; tukamkataza, kwa sababu hafuatani na sisi.
“Master,” said John, “we saw someone driving out demons in Your name, and we tried to stop him, because he does not accompany us.”
50
Yesu akamwambia, Msimkataze, kwa kuwa yeye ambaye si kinyume chenu yu upande wenu.
“Do not stop him,” Jesus replied, “for whoever is not against you is for you.”
51
Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu;
As the day of His ascension approached, Jesus resolutely set out for Jerusalem.
52
akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali.
He sent messengers on ahead, who went into a village of the Samaritans to make arrangements for Him.
53
Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu.
But the people there refused to welcome Him, because He was heading for Jerusalem.
54
Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]?
When the disciples James and John saw this, they asked, “Lord, do You want us to call down fire from heaven to consume them?”
55
Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.]
But Jesus turned and rebuked them.
56
Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine.
And He and His disciples went on to another village.
57
Nao walipokuwa wakienda njiani, mtu mmoja alimwambia, Nitakufuata ko kote utakakokwenda.
As they were walking along the road, someone said to Jesus, “I will follow You wherever You go.”
58
Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake.
Jesus replied, “Foxes have dens and birds of the air have nests, but the Son of Man has no place to lay His head.”
59
Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema, Bwana, nipe ruhusa kwanza niende nikamzike baba yangu.
Then He said to another man, “Follow Me.” The man replied, “Lord, first let me go and bury my father.”
60
Akamwambia Waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe enenda ukautangaze ufalme wa Mungu.
But Jesus told him, “Let the dead bury their own dead. You, however, go and proclaim the kingdom of God.”
61
Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu.
Still another said, “I will follow You, Lord; but first let me bid farewell to my family.”
62
Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.
Then Jesus declared, “No one who puts his hand to the plow and then looks back is fit for the kingdom of God.”