Luka 23 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 23 (Swahili) Luke 23 (English)

Wakasimama mkutano wote, wakampeleka kwa Pilato. Luka 23:1

The whole company of them rose up and brought him before Pilate.

Wakaanza kumshitaki, wakisema, Tumemwona huyu akipotosha taifa letu, na kuwazuia watu wasimpe Kaisari kodi, akisema kwamba yeye mwenyewe ni Kristo, mfalme. Luka 23:2

They began to accuse him, saying, "We found this man perverting the nation, forbidding paying taxes to Caesar, and saying that he himself is Christ, a king."

Pilato akamwuliza, akisema, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu akamwambia, Wewe wasema. Luka 23:3

Pilate asked him, "Are you the King of the Jews?" He answered him, "So you say."

Pilato akawaambia wakuu wa makuhani na makutano, Sioni neno lililo ovu katika mtu huyu. Luka 23:4

Pilate said to the chief priests and the multitudes, "I find no basis for a charge against this man."

Nao walikaza sana, wakisema, Huwataharakisha watu, akifundisha katika Uyahudi yote, tokea Galilaya mpaka huku. Luka 23:5

But they insisted, saying, "He stirs up the people, teaching throughout all Judea, beginning from Galilee even to this place."

Pilato aliposikia hayo aliuliza kama huyu ni mtu wa Galilaya. Luka 23:6

But when Pilate heard Galilee mentioned, he asked if the man was a Galilean.

Na alipopata habari ya kuwa yu chini ya mamlaka ya Herode, alimpeleka kwa Herode, kwa kuwa yeye naye alikuwapo Yerusalemu siku zile. Luka 23:7

When he found out that he was in Herod's jurisdiction, he sent him to Herod, who was also in Jerusalem during those days.

Na Herode alipomwona Yesu alifurahi sana, kwa sababu alikuwa akitaka sana kumwona tangu siku nyingi, maana amesikia habari zake, akataraji kuona ishara iliyofanywa na yeye. Luka 23:8

Now when Herod saw Jesus, he was exceedingly glad, for he had wanted to see him for a long time, because he had heard many things about him. He hoped to see some miracle done by him.

Akamwuliza maneno mengi, yeye asimjibu lo lote. Luka 23:9

He questioned him with many words, but he gave no answers.

Wakuu wa makuhani na waandishi wakasimama wakamshitaki kwa nguvu sana. Luka 23:10

The chief priests and the scribes stood, vehemently accusing him.

Basi Herode akamfanya duni, pamoja na askari zake, akamdhihaki, na kumvika mavazi mazuri; kisha akamrudisha kwa Pilato. Luka 23:11

Herod with his soldiers humiliated him and mocked him. Dressing him in luxurious clothing, they sent him back to Pilate.

Basi siku ile ile Herode na Pilato walipatana kwa urafiki kwa maana hapo kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao. Luka 23:12

Herod and Pilate became friends with each other that very day, for before that they were enemies with each other.

Na Pilato akawakutanisha wakuu wa makuhani, na wakubwa, na watu, Luka 23:13

Pilate called together the chief priests and the rulers and the people,

akawaambia, Mtu huyu mmemleta kwangu kana kwamba anapotosha watu; nami, tazama, nimeamua mambo yake mbele yenu, ila sikuona kwake kosa lo lote katika mambo hayo mliyomshitaki; Luka 23:14

and said to them, "You brought this man to me as one that perverts the people, and see, I have examined him before you, and found no basis for a charge against this man concerning those things of which you accuse him.

wala hata Herode, kwa maana amemrudisha kwetu; basi tazama, hakuna neno lo lote alilolitenda lipasalo kufa. Luka 23:15

Neither has Herod, for I sent you to him, and see, nothing worthy of death has been done by him.

Kwa hiyo nitamrudi, kisha nitamfungua. [ Luka 23:16

I will therefore chastise him and release him."

Maana ilimlazimu kuwafungulia mfungwa mmoja wakati wa sikukuu.] Luka 23:17

Now he had to release one prisoner to them at the feast.

Wakapiga kelele wote pamoja, wakisema, Mwondoe huyu, utufungulie Baraba. Luka 23:18

But they all cried out together, saying, "Away with this man! Release to us Barabbas!" --

Naye ni mtu aliyetupwa gerezani kwa ajili ya fitina iliyotokea mjini, na kwa uuaji Luka 23:19

one who was thrown into prison for a certain revolt in the city, and for murder.

Basi Pilato alisema nao mara ya pili, kwa vile alivyotaka kumfungua Yesu. Luka 23:20

Then Pilate spoke to them again, wanting to release Jesus,

Lakini wakapiga kelele, wakisema, Msulibishe. Msulibishe. Luka 23:21

but they shouted, saying, "Crucify! Crucify him!"

Akawaambia mara ya tatu, Kwa sababu gani? Huyu ametenda uovu gani? Sikuona kwake hata neno lipasalo kufa. Basi nikiisha kumrudi nitamfungua. Luka 23:22

He said to them the third time, "Why? What evil has this man done? I have found no capital crime in him. I will therefore chastise him and release him."

Lakini wakatoa sauti zao kwa nguvu sana, wakitaka asulibiwe. Sauti zao zikashinda. Luka 23:23

But they were urgent with loud voices, asking that he might be crucified. Their voices and the voices of the chief priests prevailed.

Pilato akahukumu kwamba haja yao ifanyike. Luka 23:24

Pilate decreed that what they asked for should be done.

Akamfungua yule aliyetupwa gerezani kwa ajili ya fitina na uuaji, yule waliyemtaka, akamtoa Yesu wamfanyie watakavyo. Luka 23:25

He released him who had been thrown into prison for insurrection and murder, for whom they asked, but he delivered Jesus up to their will.

Na walipokuwa wakimwondoa walimkamata mtu mmoja, Simoni Mkirene, aliyekuwa ametoka shamba, wakamtwika msalaba, auchukue nyuma yake Yesu. Luka 23:26

When they led him away, they grabbed one Simon of Cyrene, coming from the country, and laid on him the cross, to carry it after Jesus.

Mkutano mkubwa wa watu wakamfuata, na wanawake waliokuwa wakijipiga vifua na kumwombolezea. Luka 23:27

A great multitude of the people followed him, including women who also mourned and lamented him.

Yesu akawageukia, akasema, Enyi binti za Yerusalemu, msinililie mimi, bali jililieni nafsi zenu na watoto wenu. Luka 23:28

But Jesus, turning to them, said, "Daughters of Jerusalem, don't weep for me, but weep for yourselves and for your children.

Kwa maana tazama, siku zitakuja watakaposema, Heri walio tasa, na matumbo yasiyozaa, na maziwa yasiyonyonyesha. Luka 23:29

For behold, the days are coming in which they will say, 'Blessed are the barren, the wombs that never bore, and the breasts that never nursed.'

Ndipo watakapoanza kuiambia milima, Tuangukieni, na vilima, Tufunikeni. Luka 23:30

Then they will begin to tell the mountains, 'Fall on us!' and tell the hills, 'Cover us.'

Kwa kuwa kama wakitenda mambo haya katika mti mbichi, itakuwaje katika mkavu? Luka 23:31

For if they do these things in the green tree, what will be done in the dry?"

Wakapelekwa na wawili wengine, wahalifu, wauawe pamoja naye. Luka 23:32

There were also others, two criminals, led with him to be put to death.

Na walipofika mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, ndipo walipomsulibisha yeye, na wale wahalifu, mmoja upande wa kuume, na mmoja upande wa kushoto. Luka 23:33

When they came to the place that is called The Skull, they crucified him there with the criminals, one on the right and the other on the left.

Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo. Wakagawa mavazi yake, wakipiga kura. Luka 23:34

Jesus said, "Father, forgive them, for they don't know what they are doing." Dividing his garments among them, they cast lots.

Watu wakasimama wakitazama. Wale wakuu nao walikuwa wakimfanyia mzaha, wakisema, Aliokoa wengine; na ajiokoe mwenyewe, kama ndiye Kristo wa Mungu, mteule wake. Luka 23:35

The people stood watching. The rulers with them also scoffed at him, saying, "He saved others. Let him save himself, if this is the Christ of God, his chosen one!"

Wale askari nao wakamfanyia dhihaka, wakimwendea na kumletea siki, Luka 23:36

The soldiers also mocked him, coming to him and offering him vinegar,

huku wakisema, Kama wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi, ujiokoe mwenyewe. Luka 23:37

and saying, "If you are the King of the Jews, save yourself!"

Na juu yake palikuwa na anwani; HUYU NDIYE MFALME WA WAYAHUDI. Luka 23:38

An inscription was also written over him in letters of Greek, Latin, and Hebrew: "THIS IS THE KING OF THE JEWS."

Na mmoja wa wale wahalifu waliotungikwa alimtukana, akisema, Je! Wewe si Kristo? Jiokoe nafsi yako na sisi. Luka 23:39

One of the criminals who was hanged insulted him, saying, "If you are the Christ, save yourself and us!"

Lakini yule wa pili akamjibu akamkemea, akisema, Wewe humwogopi hata Mungu, nawe u katika hukumu iyo hiyo? Luka 23:40

But the other answered, and rebuking him said, "Don't you even fear God, seeing you are under the same condemnation?

Nayo ni haki kwetu sisi, kwa kuwa tunapokea malipo tuliyostahili kwa matendo yetu; bali huyu hakutenda lo lote lisilofaa. Luka 23:41

And we indeed justly, for we receive the due reward for our deeds, but this man has done nothing wrong."

Kisha akasema, Ee Yesu, nikumbuke utakapoingia katika ufalme wako. Luka 23:42

He said to Jesus, "Lord, remember me when you come into your Kingdom."

Yesu akamwambia, Amin, nakuambia, leo hivi utakuwa pamoja nami peponi. Luka 23:43

Jesus said to him, "Assuredly I tell you, today you will be with me in Paradise."

Hapo ilikuwa yapata saa sita, kukawa giza juu ya nchi yote hata saa kenda, Luka 23:44

It was now about the sixth hour{Time was counted from sunrise, so the sixth hour was about noon.}, and darkness came over the whole land until the ninth hour.{3:00 PM}

jua limepungua nuru yake; pazia la hekalu likapasuka katikati. Luka 23:45

The sun was darkened, and the veil of the temple was torn in two.

Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, Ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu. Luka 23:46

Jesus, crying with a loud voice, said, "Father, into your hands I commit my spirit!" Having said this, he breathed his last.

Alipokwisha kusema hayo alikata roho. Yule akida alipoona yaliyotukia, alimtukuza Mungu, akisema, Hakika yake, mtu huyu alikuwa mwenye haki. Luka 23:47

When the centurion saw what was done, he glorified God, saying, "Certainly this was a righteous man."

Na makutano yote ya watu waliokuwa wamekutanika kutazama mambo hayo, walipoona yaliyotendeka, wakaenda zao kwao, wakijipiga-piga vifua. Luka 23:48

All the multitudes that came together to see this, when they saw the things that were done, returned home beating their breasts.

Na wote waliojuana naye, na wale wanawake walioandamana naye toka Galilaya, wakasimama kwa mbali, wakitazama mambo hayo. Luka 23:49

All his acquaintances, and the women who followed with him from Galilee, stood at a distance, watching these things.

Na tazama, akatoka mtu mmoja, jina lake Yusufu, ambaye ni mtu wa baraza, mtu mwema, mwenye haki; Luka 23:50

Behold, a man named Joseph, who was a member of the council, a good and righteous man

(wala hakulikubali shauri na tendo lao), naye ni mtu wa Arimathaya, mji mmoja wa Wayahudi, tena anautazamia ufalme wa Mungu; Luka 23:51

(he had not consented to their counsel and deed), from Arimathaea, a city of the Jews, who was also waiting for the Kingdom of God:

mtu huyo alikwenda kwa Pilato, akataka kupewa mwili wa Yesu. Luka 23:52

this man went to Pilate, and asked for Jesus' body.

Akaushusha, akauzinga sanda ya kitani, akauweka katika kaburi lililochongwa mwambani, ambalo hajalazwa mtu bado ndani yake. Luka 23:53

He took it down, and wrapped it in a linen cloth, and laid him in a tomb that was cut in stone, where no one had ever been laid.

Na siku ile ilikuwa siku ya Maandalio, na sabato ikaanza kuingia. Luka 23:54

It was the day of the Preparation, and the Sabbath was drawing near.

Na wale wanawake waliokuja naye toka Galilaya walifuata, wakaliona kaburi, na jinsi mwili wake ulivyowekwa. Luka 23:55

The women, who had come with him out of Galilee, followed after, and saw the tomb, and how his body was laid.

Wakarudi, wakafanya tayari manukato na marhamu. Na siku ya sabato walistarehe kama ilivyoamriwa. Luka 23:56

They returned, and prepared spices and ointments. On the Sabbath they rested according to the commandment.