Luka 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 16 (Swahili) Luke 16 (English)

Tena, aliwaambia wanafunzi wake, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyekuwa na wakili wake; huyu alishitakiwa kwake kuwa anatapanya mali zake. Luka 16:1

He also said to his disciples, "There was a certain rich man who had a manager. An accusation was made to him that this man was wasting his possessions.

Akamwita, akamwambia, Ni habari gani hii ninayosikia juu yako? Toa hesabu ya uwakili wako, kwa kuwa huwezi kuwa wakili tena. Luka 16:2

He called him, and said to him, 'What is this that I hear about you? Give an accounting of your management, for you can no longer be manager.'

Yule wakili akasema moyoni mwake, Nifanyeje? Maana, bwana wangu ananiondolea uwakili. Kulima, siwezi; kuomba, naona haya. Luka 16:3

"The manager said within himself, 'What will I do, seeing that my lord is taking away the management position from me? I don't have strength to dig. I am ashamed to beg.

Najua nitakalotenda, ili nitakapotolewa katika uwakili, wanikaribishe nyumbani mwao. Luka 16:4

I know what I will do, so that when I am removed from management, they may receive me into their houses.'

Akawaita wadeni wa bwana wake, kila mmoja; akamwambia wa kwanza, Wawiwani na bwana wangu? Luka 16:5

Calling each one of his lord's debtors to him, he said to the first, 'How much do you owe to my lord?'

Akasema, Vipimo mia vya mafuta. Akamwambia, Twaa hati yako, keti upesi, andika hamsini. Luka 16:6

He said, 'A hundred batos{100 batos is about 395 litres, 104 U. S. gallons, or 87 imperial gallons.} of oil.' He said to him, 'Take your bill, and sit down quickly and write fifty.'

Kisha akamwambia mwingine, Na wewe wawiwani? Akasema, Makanda mia ya ngano. Akamwambia, Twaa hati yako, andika themanini. Luka 16:7

Then said he to another, 'How much do you owe?' He said, 'A hundred cors{ 100 cors = about 3,910 litres or 600 bushels. } of wheat.' He said to him, 'Take your bill, and write eighty.'

Yule bwana akamsifu wakili dhalimu kwa vile alivyotenda kwa busara; kwa kuwa wana wa ulimwengu huu katika kizazi chao wenyewe huwa na busara kuliko wana wa nuru. Luka 16:8

"His lord commended the dishonest manager because he had done wisely, for the children of this world are, in their own generation, wiser than the children of the light.

Nami nawaambia, Jifanyieni rafiki kwa mali ya udhalimu, ili itakapokosekana wawakaribishe katika makao ya milele. Luka 16:9

I tell you, make for yourselves friends by means of unrighteous mammon, so that when you fail, they may receive you into the eternal tents.

Aliye mwaminifu katika lililo dogo sana, huwa mwaminifu katika lililo kubwa pia; na aliye dhalimu katika lililo dogo, huwa dhalimu katika lililo kubwa pia. Luka 16:10

He who is faithful in a very little is faithful also in much. He who is dishonest in a very little is also dishonest in much.

Basi, kama ninyi hamkuwa waaminifu katika mali ya udhalimu, ni nani atakayewapa amana mali ya kweli? Luka 16:11

If therefore you have not been faithful in the unrighteous mammon, who will commit to your trust the true riches?

Na kama hamkuwa waaminifu katika mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa iliyo yenu wenyewe? Luka 16:12

If you have not been faithful in that which is another's, who will give you that which is your own?

Hakuna mtumishi awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana, ama atamchukia huyu na kumpenda huyu, ama atashikamana na huyu na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali. Luka 16:13

No servant can serve two masters, for either he will hate the one, and love the other; or else he will hold to one, and despise the other. You aren't able to serve God and mammon{"Mammon" refers to riches or a false god of wealth.}."

Basi Mafarisayo, ambao wenyewe ni wapenda fedha, waliyasikia hayo yote, wakamdhihaki. Luka 16:14

The Pharisees, who were lovers of money, also heard all these things, and they scoffed at him.

Akawaambia, Ninyi ndinyi mnaojidai haki mbele ya wanadamu, lakini Mungu awajua mioyo yenu; kwa kuwa lililotukuka kwa wanadamu huwa chukizo mbele za Mungu. Luka 16:15

He said to them, "You are those who justify yourselves in the sight of men, but God knows your hearts. For that which is exalted among men is an abomination in the sight of God.

Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu. Luka 16:16

The law and the prophets were until John. From that time the Gospel of the Kingdom of God is preached, and everyone is forcing his way into it.

Lakini ni vyepesi zaidi mbingu na nchi vitoweke, kuliko itanguke nukta moja ya torati. Luka 16:17

But it is easier for heaven and earth to pass away, than for one tiny stroke of a pen in the law to fall.

Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine azini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe azini. Luka 16:18

Everyone who divorces his wife, and marries another, commits adultery. He who marries one who is divorced from a husband commits adultery.

Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa. Luka 16:19

"Now there was a certain rich man, and he was clothed in purple and fine linen, living in luxury every day.

Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, huwekwa mlangoni pake, ana vidonda vingi, Luka 16:20

A certain beggar, named Lazarus, was laid at his gate, full of sores,

naye alikuwa akitamani kushibishwa kwa makombo yaliyoanguka katika meza ya yule tajiri; hata mbwa wakaja wakamramba vidonda vyake. Luka 16:21

and desiring to be fed with the crumbs that fell from the rich man's table. Yes, even the dogs came and licked his sores.

Ikawa yule maskini alikufa, akachukuliwa na malaika mpaka kifuani kwa Ibrahimu. Yule tajiri naye akafa, akazikwa. Luka 16:22

It happened that the beggar died, and that he was carried away by the angels to Abraham's bosom. The rich man also died, and was buried.

Basi, kule kuzimu aliyainua macho yake, alipokuwa katika mateso, akamwona Ibrahimu kwa mbali, na Lazaro kifuani mwake. Luka 16:23

In Hades, he lifted up his eyes, being in torment, and saw Abraham far off, and Lazarus at his bosom.

Akalia, akasema, Ee baba Ibrahimu, nihurumie, umtume Lazaro achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa sababu ninateswa katika moto huu. Luka 16:24

He cried and said, 'Father Abraham, have mercy on me, and send Lazarus, that he may dip the tip of his finger in water, and cool my tongue! For I am in anguish in this flame.'

Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kwamba wewe uliyapokea mambo mema yako katika maisha yako, na Lazaro vivyo alipata mabaya; na sasa yeye yupo hapa anafarijiwa, na wewe unaumizwa. Luka 16:25

"But Abraham said, 'Son, remember that you, in your lifetime, received your good things, and Lazarus, in like manner, bad things. But now here he is comforted and you are in anguish.

Na zaidi ya hayo, kati yetu sisi na ninyi kumewekwa shimo kubwa, ili wale watakao kutoka huku kwenda kwenu wasiweze; wala watu wa kwenu wasivuke kuja kwetu. Luka 16:26

Besides all this, between us and you there is a great gulf fixed, that those who want to pass from here to you are not able, and that none may cross over from there to us.'

Akasema, Basi, baba, nakuomba, umtume nyumbani kwa baba yangu, Luka 16:27

"He said, 'I ask you therefore, father, that you would send him to my father's house;

kwa kuwa ninao ndugu watano, ili awashuhudie, wasije wao pia wakafika mahali hapa pa mateso. Luka 16:28

for I have five brothers, that he may testify to them, so they won't also come into this place of torment.'

Ibrahimu akasema, Wanao Musa na manabii; na wawasikilize wao. Luka 16:29

"But Abraham said to him, 'They have Moses and the prophets. Let them listen to them.'

Akasema, La, baba Ibrahimu, lakini kama akiwaendea mtu atokaye kwa wafu, watatubu. Luka 16:30

"He said, 'No, father Abraham, but if one goes to them from the dead, they will repent.'

Akamwambia, Wasipowasikia Musa na manabii, hawatashawishwa hata mtu akifufuka katika wafu. Luka 16:31

"He said to him, 'If they don't listen to Moses and the prophets, neither will they be persuaded if one rises from the dead.'"