Luka 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 2 (Swahili) Luke 2 (English)

Siku zile amri ilitoka kwa Kaisari Augusto ya kwamba iandikwe orodha ya majina ya watu wote wa ulimwengu. Luka 2:1

Now it happened in those days, that a decree went out from Caesar Augustus that all the world should be enrolled.

Orodha hii ndiyo ya kwanza iliyoandikwa hapo Kirenio alipokuwa liwali wa Shamu. Luka 2:2

This was the first enrollment made when Quirinius was governor of Syria.

Watu wote wakaenda kuandikwa, kila mtu mjini kwao. Luka 2:3

All went to enroll themselves, everyone to his own city.

Yusufu naye aliondoka Galilaya, toka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Uyahudi mpaka mji wa Daudi, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye ni wa mbari na jamaa ya Daudi; Luka 2:4

Joseph also went up from Galilee, out of the city of Nazareth, into Judea, to the city of David, which is called Bethlehem, because he was of the house and family of David;

ili aandikwe pamoja na Mariamu mkewe, ambaye amemposa, naye ana mimba. Luka 2:5

to enroll himself with Mary, who was pledged to be married to him as wife, being pregnant.

Ikawa, katika kukaa huko, siku zake za kuzaa zikatimia, Luka 2:6

It happened, while they were there, that the day had come that she should give birth.

akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng'ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni. Luka 2:7

She brought forth her firstborn son, and she wrapped him in bands of cloth, and laid him in a feeding trough, because there was no room for them in the inn.

Na katika nchi ile ile walikuwako wachungaji wakikaa makondeni na kulinda kundi lao kwa zamu usiku. Luka 2:8

There were shepherds in the same country staying in the field, and keeping watch by night over their flock.

Malaika wa Bwana akawatokea ghafula, utukufu wa Bwana ukawang'aria pande zote, wakaingiwa na hofu kuu. Luka 2:9

Behold, an angel of the Lord stood by them, and the glory of the Lord shone around them, and they were terrified.

Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; Luka 2:10

The angel said to them, "Don't be afraid, for behold, I bring you good news of great joy which will be to all the people.

maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. Luka 2:11

For there is born to you, this day, in the city of David, a Savior, who is Christ the Lord.

Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe. Luka 2:12

This is the sign to you: you will find a baby wrapped in strips of cloth, lying in a feeding trough."

Mara walikuwapo pamoja na huyo malaika, wingi wa jeshi la mbinguni, wakimsifu Mungu, na kusema, Luka 2:13

Suddenly, there was with the angel a multitude of the heavenly host praising God, and saying,

Atukuzwe Mungu juu mbinguni, Na duniani iwe amani kwa watu aliowaridhia. Luka 2:14

"Glory to God in the highest, On earth peace, good will toward men."

Ikawa, malaika hao walipoondoka kwenda zao mbinguni, wale wachungaji waliambiana, Haya, na twendeni mpaka Bethlehemu, tukalione hilo lililofanyika, alilotujulisha Bwana. Luka 2:15

It happened, when the angels went away from them into the sky, that the shepherds said one to another, "Let's go to Bethlehem, now, and see this thing that has happened, which the Lord has made known to us."

Wakaenda kwa haraka wakamkuta Mariamu na Yusufu, na yule mtoto mchanga amelala horini. Luka 2:16

They came with haste, and found both Mary and Joseph, and the baby was lying in the feeding trough.

Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto. Luka 2:17

When they saw it, they publicized widely the saying which was spoken to them about this child.

Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji. Luka 2:18

All who heard it wondered at the things which were spoken to them by the shepherds.

Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake. Luka 2:19

But Mary kept all these sayings, pondering them in her heart.

Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa. Luka 2:20

The shepherds returned, glorifying and praising God for all the things that they had heard and seen, just as it was told them.

Hata zilipotumia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu; kama alivyoitwa na malaika kabla hajachukuliwa mimba. Luka 2:21

When eight days were fulfilled for the circumcision of the child, his name was called Jesus, which was given by the angel before he was conceived in the womb.

Kisha, zilipotimia siku za kutakasika kwao, kama ilivyo torati ya Musa walikwenda naye hata Yerusalemu, wamweke kwa Bwana, Luka 2:22

When the days of their purification according to the law of Moses were fulfilled, they brought him up to Jerusalem, to present him to the Lord

(kama ilivyoandikwa katika sheria ya Bwana, Kila mtoto mwanamume aliye kifungua mimba ya mamaye na aitwe mtakatifu kwa Bwana), Luka 2:23

(as it is written in the law of the Lord, "Every male who opens the womb shall be called holy to the Lord"),

wakatoe na sadaka, kama ilivyonenwa katika sheria ya Bwana, Hua wawili au makinda ya njiwa wawili. Luka 2:24

and to offer a sacrifice according to that which is said in the law of the Lord, "A pair of turtledoves, or two young pigeons."

Na tazama, pale Yerusalemu palikuwa na mtu, jina lake Simeoni, naye ni mtu mwenye haki, mcha Mungu, akiitarajia faraja ya Israeli; na Roho Mtakatifu alikuwa juu yake. Luka 2:25

Behold, there was a man in Jerusalem whose name was Simeon. This man was righteous and devout, looking for the consolation of Israel, and the Holy Spirit was on him.

Naye alikuwa ameonywa na Roho Mtakatifu ya kwamba hataona mauti kabla ya kumwona Kristo wa Bwana. Luka 2:26

It had been revealed to him by the Holy Spirit that he should not see death before he had seen the Lord's Christ.{"Christ" (Greek) and "Messiah" (Hebrew) both mean "Anointed One"}

Basi akaja hekaluni ameongozwa na Roho; na wale wazazi walipomleta mtoto Yesu ndani, ili wamfanyie kama ilivyokuwa desturi ya sheria, Luka 2:27

He came in the Spirit into the temple. When the parents brought in the child, Jesus, that they might do concerning him according to the custom of the law,

yeye mwenyewe alimpokea mikononi mwake, akamshukuru Mungu, akisema, Luka 2:28

then he received him into his arms, and blessed God, and said,

Sasa, Bwana, wamruhusu mtumishi wako, Kwa amani, kama ulivyosema; Luka 2:29

"Now you are releasing your servant, Master, According to your word, in peace;

Kwa kuwa macho yangu yameuona wokovu wako, Luka 2:30

For my eyes have seen your salvation,

Uliouweka tayari machoni pa watu wote; Luka 2:31

Which you have prepared before the face of all peoples;

Nuru ya kuwa mwangaza wa Mataifa, Na kuwa utukufu wa watu wako Israeli. Luka 2:32

A light for revelation to the Gentiles, And the glory of your people Israel."

Na babaye na mamaye walikuwa wakiyastaajabia hayo yaliyonenwa juu yake. Luka 2:33

Joseph and his mother were marveling at the things which were spoken concerning him,

Simeoni akawabariki, akamwambia Mariamu mama yake, Tazama, huyu amewekwa kwa kuanguka na kuinuka wengi walio katika Israeli, na kuwa ishara itakayonenewa. Luka 2:34

and Simeon blessed them, and said to Mary, his mother, "Behold, this child is set for the falling and the rising of many in Israel, and for a sign which is spoken against.

Nawe mwenyewe, upanga utaingia moyoni mwako, ili yafunuliwe mawazo ya mioyo mingi. Luka 2:35

Yes, a sword will pierce through your own soul, that the thoughts of many hearts may be revealed."

Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. Luka 2:36

There was one Anna, a prophetess, the daughter of Phanuel, of the tribe of Asher (she was of a great age, having lived with a husband seven years from her virginity,

Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. Luka 2:37

and she had been a widow for about eighty-four years), who didn't depart from the temple, worshipping with fastings and petitions night and day.

Huyu alitokea saa ile ile akamshukuru Mungu, na wote waliokuwa wakiutarajia ukombozi katika Yerusalemu akawatolea habari zake. Luka 2:38

Coming up at that very hour, she gave thanks to the Lord, and spoke of him to all those who were looking for redemption in Jerusalem.

Basi, walipokwisha kuyatimiza yote kama yalivyoagizwa katika sheria ya Bwana, walirejea Galilaya mpaka mjini kwao, Nazareti. Luka 2:39

When they had accomplished all things that were according to the law of the Lord, they returned into Galilee, to their own city, Nazareth.

Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu, amejaa hekima, na neema ya Mungu ilikuwa juu yake. Luka 2:40

The child was growing, and was becoming strong in spirit, being filled with wisdom, and the grace of God was upon him.

Basi, wazee wake huenda Yerusalemu kila mwaka, wakati wa sikukuu ya Pasaka. Luka 2:41

His parents went every year to Jerusalem at the feast of the Passover.

Na alipopata umri wake miaka kumi na miwili, walipanda kama ilivyokuwa desturi ya sikukuu; Luka 2:42

When he was twelve years old, they went up to Jerusalem according to the custom of the feast,

na walipokwisha kuzitimiza siku, wakati wa kurudi kwao, yule mtoto Yesu alibaki nyuma huko Yerusalemu, na wazee wake walikuwa hawana habari. Luka 2:43

and when they had fulfilled the days, as they were returning, the boy Jesus stayed behind in Jerusalem. Joseph and his mother didn't know it,

Nao wakadhani ya kuwa yumo katika msafara; wakaenenda mwendo wa kutwa, wakawa wakimtafuta katika jamaa zao na wenzao; Luka 2:44

but supposing him to be in the company, they went a day's journey, and they looked for him among their relatives and acquaintances.

na walipomkosa, wakarejea Yerusalemu, huku wakimtafuta. Luka 2:45

When they didn't find him, they returned to Jerusalem, looking for him.

Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. Luka 2:46

It happened after three days they found him in the temple, sitting in the midst of the teachers, both listening to them, and asking them questions.

Nao wote waliomsikia walistaajabia fahamu zake na majibu yake. Luka 2:47

All who heard him were amazed at his understanding and his answers.

Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni. Luka 2:48

When they saw him, they were astonished, and his mother said to him, "Son, why have you treated us this way? Behold, your father and I were anxiously looking for you."

Akawaambia, Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu? Luka 2:49

He said to them, "Why were you looking for me? Didn't you know that I must be in my Father's house?"

Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia. Luka 2:50

They didn't understand the saying which he spoke to them.

Akashuka pamoja nao mpaka Nazareti, naye alikuwa akiwatii; na mamaye aliyaweka hayo yote moyoni mwake. Luka 2:51

And he went down with them, and came to Nazareth. He was subject to them, and his mother kept all these sayings in her heart.

Naye Yesu akazidi kuendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu. Luka 2:52

And Jesus increased in wisdom and stature, and in favor with God and men.