Luka 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 9 (Swahili) Luke 9 (English)

Akawaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi. Luka 9:1

He called the twelve{TR reads "his twelve disciples" instead of "the twelve"} together, and gave them power and authority over all demons, and to cure diseases.

Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa. Luka 9:2

He sent them forth to preach the Kingdom of God, and to heal the sick.

Akawaambia, Msichukue kitu kwa safari yenu, fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala mmoja wenu asiwe na kanzu mbili. Luka 9:3

He said to them, "Take nothing for your journey--neither staffs, nor wallet, nor bread, nor money; neither have two coats apiece.

Na nyumba yo yote mtakayoingia kaeni humo, mpaka mtoke mjini. Luka 9:4

Into whatever house you enter, stay there, and depart from there.

Na wale wasiowakaribisha, mtokapo katika mji huo, yakung'uteni hata mavumbi ya miguuni mwenu, kuwa ushuhuda juu yao. Luka 9:5

As many as don't receive you, when you depart from that city, shake off even the dust from your feet for a testimony against them."

Wakaenda, wakazunguka katika vijiji, wakihubiri injili, na kupoza watu kila mahali. Luka 9:6

They departed, and went throughout the villages, preaching the Gospel, and healing everywhere.

Na Herode mfalme akasikia habari za yote yaliyotendeka, akafadhaika kwa sababu watu wengine walisema ya kwamba Yohana amefufuka katika wafu, Luka 9:7

Now Herod the tetrarch heard of all that was done by him; and he was very perplexed, because it was said by some that John had risen from the dead,

na wengine ya kwamba Eliya ametokea, na wengine ya kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka. Luka 9:8

and by some that Elijah had appeared, and by others that one of the old prophets had risen again.

Lakini Herode akasema, Yohana nilimkata kichwa; basi ni nani huyu ambaye ninasikia mambo haya juu yake? Akataka kumwona. Luka 9:9

Herod said, "John I beheaded, but who is this, about whom I hear such things?" He sought to see him.

Basi wale mitume waliporudi walimweleza mambo yote waliyoyatenda; akawachukua, akaenda nao faraghani mpaka mji mmoja uitwao Bethsaida. Luka 9:10

The apostles, when they had returned, told him what things they had done. He took them, and withdrew apart to a deserted place of a city called Bethsaida.

Na makutano walipojua walimfuata; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa. Luka 9:11

But the multitudes, perceiving it, followed him. He welcomed them, and spoke to them of the Kingdom of God, and he cured those who needed healing.

Na jua likaanza kushuka; wakamwendea wale Thenashara, wakamwambia, Uage mkutano, ili waende katika vijiji na mashamba ya kandokando wapate mahali pa kulala na vyakula, maana hapa tulipo ni nyika tupu. Luka 9:12

The day began to wear away; and the twelve came, and said to him, "Send the multitude away, that they may go into the surrounding villages and farms, and lodge, and get food, for we are here in a deserted place."

Akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakasema, Hatuna kitu zaidi ya mikate mitano na samaki wawili, tusipokwenda tukawanunulie watu hawa wote vyakula. Luka 9:13

But he said to them, "You give them something to eat." They said, "We have no more than five loaves and two fish, unless we should go and buy food for all these people."

Kwa kuwa wanaume waliokuwako walipata kama elfu tano. Akawaambia wanafunzi wake, Waketisheni watu kwa safu, kila safu watu hamsini. Luka 9:14

For they were about five thousand men. He said to his disciples, "Make them sit down in groups of about fifty each."

Wakafanya hivyo, wakawaketisha wote. Luka 9:15

They did so, and made them all sit down.

Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi wake ili wawaandikie mkutano. Luka 9:16

He took the five loaves and the two fish, and looking up to the sky, he blessed them, and broke them, and gave them to the disciples to set before the multitude.

Wakala, wakashiba wote; na katika vile vipande vilivyowabakia walikusanya vikapu kumi na viwili. Luka 9:17

They ate, and were all filled. They gathered up twelve baskets of broken pieces that were left over.

Ikawa alipokuwa akisali kwa faragha, wanafunzi wake walikuwapo pamoja naye, akawauliza, Je! Makutano hao wanasema ya kuwa mimi ni nani? Luka 9:18

It happened, as he was praying alone, that the disciples were with him, and he asked them, "Who do the multitudes say that I am?"

Wakamjibu wakisema, Yohana Mbatizaji; lakini wengine, Eliya; na wengine kwamba mmojawapo wa manabii wa kale amefufuka. Luka 9:19

They answered, "'John the Baptizer,' but others say, 'Elijah,' and others, that one of the old prophets is risen again."

Akawaambia, Nanyi mwasema ya kwamba mimi ni nani? Petro akamjibu akasema, Ndiwe Kristo wa Mungu. Luka 9:20

He said to them, "But who do you say that I am?" Peter answered, "The Christ of God."

Akawaonya, akawakataza wasimwambie mtu neno hilo; Luka 9:21

But he warned them, and commanded them to tell this to no one,

akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, na kuuawa na siku ya tatu kufufuka. Luka 9:22

saying, "The Son of Man must suffer many things, and be rejected by the elders, chief priests, and scribes, and be killed, and the third day be raised up."

Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate. Luka 9:23

He said to all, "If anyone desires to come after me, let him deny himself, take up his cross,{TR, NU add "daily"} and follow me.

Kwa kuwa mtu atakaye kuiponya nafsi yake ataiangamiza, na mtu atakayeiangamiza nafsi yake kwa ajili yangu ndiye atakayeisalimisha. Luka 9:24

For whoever desires to save his life will lose it, but whoever will lose his life for my sake, the same will save it.

Kwa kuwa yamfaa nini mtu kuupata ulimwengu wote, kama akijiangamiza, au kujipoteza mwenyewe? Luka 9:25

For what does it profit a man if he gains the whole world, and loses or forfeits his own self?

Kwa sababu kila atakayenionea haya mimi na maneno yangu, Mwana wa Adamu atamwonea haya mtu huyo, atakapokuja katika utukufu wake na wa Baba na wa malaika watakatifu. Luka 9:26

For whoever will be ashamed of me and of my words, of him will the Son of Man be ashamed, when he comes in his glory, and the glory of the Father, and of the holy angels.

Nami nawaambia kweli, Wapo katika hawa wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hata wauone kwanza ufalme wa Mungu. Luka 9:27

But I tell you the truth: There are some of those who stand here, who will in no way taste of death, until they see the Kingdom of God."

Baada ya maneno hayo yapata siku nane, aliwatwaa Petro na Yohana na Yakobo, akapanda mlimani ili kuomba. Luka 9:28

It happened about eight days after these sayings, that he took with him Peter, John, and James, and went up onto the mountain to pray.

Ikawa katika kusali kwake sura ya uso wake ikageuka, mavazi yake yakawa meupe, yakimeta-meta. Luka 9:29

As he was praying, the appearance of his face was altered, and his clothing became white and dazzling.

Na tazama, watu wawili walikuwa wakizungumza naye, nao ni Musa na Eliya; Luka 9:30

Behold, two men were talking with him, who were Moses and Elijah,

walioonekana katika utukufu, wakanena habari za kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemu. Luka 9:31

who appeared in glory, and spoke of his departure,{Literally, "exodus"} which he was about to accomplish at Jerusalem.

Petro na wale waliokuwa pamoja naye walikuwa wamelemewa na usingizi; lakini walipokwisha amka waliuona utukufu wake, na wale wawili waliosimama pamoja naye. Luka 9:32

Now Peter and those who were with him were heavy with sleep, but when they were fully awake, they saw his glory, and the two men who stood with him.

Ikawa hao walipokuwa wakijitenga naye, Petro alimwambia Yesu, Bwana mkubwa, ni vizuri sisi kuwapo hapa; na tufanye vibanda vitatu; kimoja chako wewe, na kimoja cha Musa, na kimoja cha Eliya; hali hajui asemalo. Luka 9:33

It happened, as they were parting from him, that Peter said to Jesus, "Master, it is good for us to be here. Let's make three tents: one for you, and one for Moses, and one for Elijah," not knowing what he said.

Alipokuwa akisema hayo, lilitokea wingu likawatia uvuli, wakaogopa walipoingia katika wingu hilo. Luka 9:34

While he said these things, a cloud came and overshadowed them, and they were afraid as they entered into the cloud.

Sauti ikatoka katika wingu, ikisema, Huyu ni Mwanangu, mteule wangu, msikieni yeye. Luka 9:35

A voice came out of the cloud, saying, "This is my beloved Son. Listen to him!"

Na sauti hiyo ilipokwisha, Yesu alionekana yu peke yake. Nao wakanyamaza, wasitangaze kwa mtu siku zile lo lote katika hayo waliyoyaona. Luka 9:36

When the voice came, Jesus was found alone. They were silent, and told no one in those days any of the things which they had seen.

Ikawa siku ya pili yake, waliposhuka mlimani, mkutano mkubwa ulikutana naye. Luka 9:37

It happened on the next day, when they had come down from the mountain, that a great multitude met him.

Na tazama, mtu mmoja katika mkutano alipaza sauti, akisema, Mwalimu, nakuomba umwangalie mwanangu; kwa kuwa yeye ni mwanangu pekee. Luka 9:38

Behold, a man from the crowd called out, saying, "Teacher, I beg you to look at my son, for he is my only child.

Na tazama, pepo humpagaa, naye mara hupiga kelele; tena humtia kifafa, huku anatokwa na povu, wala hamwachi ila kwa shida, akimchubua-chubua. Luka 9:39

Behold, a spirit takes him, he suddenly cries out, and it convulses him so that he foams, and it hardly departs from him, bruising him severely.

Nikawasihi wanafunzi wako wamtoe, wasiweze. Luka 9:40

I begged your disciples to cast it out, and they couldn't."

Yesu akajibu akasema, Enyi kizazi kisicho na imani, kilichopotoka, nitakaa nanyi na kuwachukulia hata lini? Mlete mwanao hapa. Luka 9:41

Jesus answered, "Faithless and perverse generation, how long shall I be with you and bear with you? Bring your son here."

Alipokuwa katika kumwendea, pepo akambwaga chini, akamtia kifafa. Yesu akamkemea pepo mchafu, akamponya mtoto, akamrudishia babaye. Luka 9:42

While he was still coming, the demon threw him down and convulsed him violently. But Jesus rebuked the unclean spirit, and healed the boy, and gave him back to his father.

Wote wakashangaa, wakiuona ukuu wa Mungu. Nao walipokuwa wakiyastaajabia mambo yote aliyoyafanya, aliwaambia wanafunzi wake, Luka 9:43

They were all astonished at the majesty of God. But while all were marveling at all the things which Jesus did, he said to his disciples,

Yashikeni maneno haya masikioni mwenu, kwa kuwa Mwana wa Adamu anakwenda kutiwa katika mikono ya watu. Luka 9:44

"Let these words sink into your ears, for the Son of Man will be delivered up into the hands of men."

Lakini hawakulifahamu neno lile, likafichwa kwao wasilitambue; wakaogopa kumwuliza maana yake neno lile. Luka 9:45

But they didn't understand this saying. It was concealed from them, that they should not perceive it, and they were afraid to ask him about this saying.

Wakaanza kuhojiana, ni nani atakayekuwa mkubwa miongoni mwao. Luka 9:46

There arose an argument among them about which of them was the greatest.

Naye Yesu alipotambua mawazo ya mioyo yao, alitwaa mtoto mdogo akamweka karibu naye, Luka 9:47

Jesus, perceiving the reasoning of their hearts, took a little child, and set him by his side,

akawaambia, Ye yote atakayempokea mtoto huyu kwa jina langu anipokea mimi; na ye yote atakayenipokea mimi ampokea yeye aliyenituma. Kwa kuwa aliye mdogo miongoni mwenu nyote huyo ndiye mkubwa. Luka 9:48

and said to them, "Whoever receives this little child in my name receives me. Whoever receives me receives him who sent me. For whoever is least among you all, this one will be great."

Yohana akajibu akamwambia; Bwana mkubwa, tuliona mtu anatoa pepo kwa jina lako; tukamkataza, kwa sababu hafuatani na sisi. Luka 9:49

John answered, "Master, we saw someone casting out demons in your name, and we forbade him, because he doesn't follow with us."

Yesu akamwambia, Msimkataze, kwa kuwa yeye ambaye si kinyume chenu yu upande wenu. Luka 9:50

Jesus said to him, "Don't forbid him, for he who is not against us is for us."

Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, yeye aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu; Luka 9:51

It came to pass, when the days were near that he should be taken up, he intently set his face to go to Jerusalem,

akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali. Luka 9:52

and sent messengers before his face. They went, and entered into a village of the Samaritans, so as to prepare for him.

Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu. Luka 9:53

They didn't receive him, because he was traveling with his face set towards Jerusalem.

Wanafunzi wake Yakobo na Yohana walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]? Luka 9:54

When his disciples, James and John, saw this, they said, "Lord, do you want us to command fire to come down from the sky, and destroy them, just as Elijah did?"

Akawageukia, akawakanya. [Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo.] Luka 9:55

But he turned and rebuked them, "You don't know of what kind of spirit you are.

Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine. Luka 9:56

For the Son of Man didn't come to destroy men's lives, but to save them." They went to another village.

Nao walipokuwa wakienda njiani, mtu mmoja alimwambia, Nitakufuata ko kote utakakokwenda. Luka 9:57

As they went on the way, a certain man said to him, "I want to follow you wherever you go, Lord."

Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake. Luka 9:58

Jesus said to him, "The foxes have holes, and the birds of the sky have nests, but the Son of Man has no place to lay his head."

Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema, Bwana, nipe ruhusa kwanza niende nikamzike baba yangu. Luka 9:59

He said to another, "Follow me!" But he said, "Lord, allow me first to go and bury my father."

Akamwambia Waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe enenda ukautangaze ufalme wa Mungu. Luka 9:60

But Jesus said to him, "Leave the dead to bury their own dead, but you go and announce the Kingdom of God."

Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana, nitakufuata; lakini, nipe ruhusa kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu. Luka 9:61

Another also said, "I want to follow you, Lord, but first allow me to bid farewell to those who are at my house."

Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu. Luka 9:62

But Jesus said to him, "No one, having put his hand to the plow, and looking back, is fit for the Kingdom of God."