Luka 24 Swahili & English

Listen/Download Audio
Luka 24 (Swahili) Luke 24 (English)

Hata siku ya kwanza ya juma, ilipoanza kupambazuka, walikwenda kaburini, wakiyaleta manukato waliyoweka tayari. Luka 24:1

But on the first day of the week, at early dawn, they and some others came to the tomb, bringing the spices which they had prepared.

Wakalikuta lile jiwe limevingirishwa mbali na kaburi, Luka 24:2

They found the stone rolled away from the tomb.

Wakaingia, wasiuone mwili wa Bwana Yesu. Luka 24:3

They entered in, and didn't find the Lord Jesus' body.

Ikawa walipokuwa wakifadhaika kwa ajili ya neno hilo, tazama, watu wawili walisimama karibu nao, wamevaa nguo za kumeta-meta; Luka 24:4

It happened, while they were greatly perplexed about this, behold, two men stood by them in dazzling clothing.

nao walipoingiwa na hofu na kuinama kifudifudi hata nchi, hao waliwaambia, Kwa nini mnamtafuta aliye hai katika wafu? Luka 24:5

Becoming terrified, they bowed their faces down to the earth. They said to them, "Why do you seek the living among the dead?

Hayupo hapa, amefufuka. Kumbukeni alivyosema nanyi alipokuwa akaliko Galilaya, Luka 24:6

He isn't here, but is risen. Remember what he told you when he was still in Galilee,

akisema, Imempasa Mwana wa Adamu kutiwa mikononi mwa wenye dhambi, na kusulibiwa, na kufufuka siku ya tatu. Luka 24:7

saying that the Son of Man must be delivered up into the hands of sinful men, and be crucified, and the third day rise again?"

Wakayakumbuka maneno yake. Luka 24:8

They remembered his words,

Wakaondoka kaburini, wakarudi; wakawaarifu wale kumi na mmoja na wengine wote habari za mambo hayo yote. Luka 24:9

returned from the tomb, and told all these things to the eleven, and to all the rest.

Nao ni Mariamu Magdalene, na Yoana, na Mariamu mamaye Yakobo, na wale wanawake wengine waliokuwa pamoja nao; Luka 24:10

Now they were Mary Magdalene, Joanna, and Mary the mother of James. The other women with them told these things to the apostles.

hao waliwaambia mitume habari ya mambo hayo. Luka 24:11

These words seemed to them to be nonsense, and they didn't believe them.

Maneno yao yakaonekana kuwa kama upuzi kwao, wala hawakuwasadiki. Lakini Petro aliondoka akaenda mbio hata kaburini, akainama akachungulia ndani, akaviona vile vitambaa vya sanda tu; akaenda zake akiyastaajabia yaliyotukia. Luka 24:12

But Peter got up and ran to the tomb. Stooping and looking in, he saw the strips of linen lying by themselves, and he departed to his home, wondering what had happened.

Na tazama, siku ile ile watu wawili miongoni mwao walikuwa wakienda kijiji kimoja, jina lake Emau, kilichokuwa mbali na Yerusalemu kama mwendo wa saa mbili. Luka 24:13

Behold, two of them were going that very day to a village named Emmaus, which was sixty stadia{60 stadia = about 11 kilometers or about 7 miles.} from Jerusalem.

Nao walikuwa wakizungumza wao kwa wao habari za mambo hayo yote yaliyotukia. Luka 24:14

They talked with each other about all of these things which had happened.

Ikawa katika kuzungumza na kuulizana kwao, Yesu mwenyewe alikaribia, akaandamana nao. Luka 24:15

It happened, while they talked and questioned together, that Jesus himself came near, and went with them.

Macho yao yakafumbwa wasimtambue. Luka 24:16

But their eyes were kept from recognizing him.

Akawaambia, Ni maneno gani haya mnayosemezana hivi mnapotembea? Wakasimama wamekunja nyuso zao. Luka 24:17

He said to them, "What are you talking about as you walk, and are sad?"

Akajibu mmoja wao, jina lake Kleopa, akamwambia, Je! Wewe peke yako u mgeni katika Yerusalemu, hata huyajui yaliyotukia humo siku hizi? Luka 24:18

One of them, named Cleopas, answered him, "Are you the only stranger in Jerusalem who doesn't know the things which have happened there in these days?"

Akawauliza, Mambo gani? Wakamwambia, Mambo ya Yesu wa Nazareti, aliyekuwa mtu nabii, mwenye uwezo katika kutenda na kunena mbele za Mungu na watu wote; Luka 24:19

He said to them, "What things?" They said to him, "The things concerning Jesus, the Nazarene, who was a prophet mighty in deed and word before God and all the people;

tena jinsi wakuu wa makuhani na wakubwa wetu walivyomtia katika hukumu ya kufa, wakamsulibisha. Luka 24:20

and how the chief priests and our rulers delivered him up to be condemned to death, and crucified him.

Nasi tulikuwa tukitumaini ya kuwa yeye ndiye atakayewakomboa Israeli. Zaidi ya hayo yote, leo ni siku ya tatu tangu yalipotendeka mambo hayo; Luka 24:21

But we were hoping that it was he who would redeem Israel. Yes, and besides all this, it is now the third day since these things happened.

tena, wanawake kadha wa kadha wa kwetu walitushitusha, waliokwenda kaburini asubuhi na mapema, Luka 24:22

Also, certain women of our company amazed us, having arrived early at the tomb;

wasiuone mwili wake; wakaja wakasema ya kwamba wametokewa na malaika waliosema kwamba yu hai. Luka 24:23

and when they didn't find his body, they came saying that they had also seen a vision of angels, who said that he was alive.

Na wengine waliokuwa pamoja nasi walikwenda kaburini wakaona vivyo hivyo kama wale wanawake walivyosema, ila yeye hawakumwona. Luka 24:24

Some of us went to the tomb, and found it just like the women had said, but they didn't see him."

Akawaambia, Enyi msiofahamu, wenye mioyo mizito ya kuamini yote waliyoyasema manabii! Luka 24:25

He said to them, "Foolish men, and slow of heart to believe in all that the prophets have spoken!

Je! Haikumpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake? Luka 24:26

Didn't the Christ have to suffer these things and to enter into his glory?"

Akaanza kutoka Musa na manabii wote, akawaeleza katika maandiko yote mambo yaliyomhusu yeye mwenyewe. Luka 24:27

Beginning from Moses and from all the prophets, he explained to them in all the Scriptures the things concerning himself.

Wakakikaribia kile kijiji walichokuwa wakienda, naye alifanya kama anataka kuendelea mbele. Luka 24:28

They drew near to the village, where they were going, and he acted like he would go further.

Wakamshawishi wakisema, Kaa pamoja nasi, kwa kuwa kumekuchwa, na mchana unakwisha. Akaingia ndani kukaa nao. Luka 24:29

They urged him, saying, "Stay with us, for it is almost evening, and the day is almost over." He went in to stay with them.

Ikawa alipokuwa ameketi nao chakulani, alitwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawapa. Luka 24:30

It happened, that when he had sat down at the table with them, he took the bread and gave thanks. Breaking it, he gave to them.

Yakafumbuliwa macho yao, wakamtambua; kisha akatoweka mbele yao. Luka 24:31

Their eyes were opened, and they recognized him, and he vanished out of their sight.

Wakaambiana, Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu hapo alipokuwa akisema nasi njiani, na kutufunulia maandiko? Luka 24:32

They said one to another, "Weren't our hearts burning within us, while he spoke to us along the way, and while he opened the Scriptures to us?"

Wakaondoka saa ile ile, wakarejea Yerusalemu, wakawakuta wale kumi na mmoja wamekutanika, wao na wale waliokuwa pamoja nao, Luka 24:33

They rose up that very hour, returned to Jerusalem, and found the eleven gathered together, and those who were with them,

wakisema, Bwana amefufuka kweli kweli, naye amemtokea Simoni. Luka 24:34

saying, "The Lord is risen indeed, and has appeared to Simon!"

Nao waliwapa habari ya mambo yale ya njiani, na jinsi alivyotambulikana nao katika kuumega mkate. Luka 24:35

They related the things that happened along the way, and how he was recognized by them in the breaking of the bread.

Na walipokuwa katika kusema habari hiyo, yeye mwenyewe alisimama katikati yao, akawaambia, Amani iwe kwenu. Luka 24:36

As they said these things, Jesus himself stood among them, and said to them, "Peace be to you."

Wakashituka, wakaogopa sana, wakidhani ya kwamba wanaona roho. Luka 24:37

But they were terrified and filled with fear, and supposed that they had seen a spirit.

Akawaambia, Mbona mnafadhaika? Na kwa nini mnaona shaka mioyoni mwenu? Luka 24:38

He said to them, "Why are you troubled? Why do doubts arise in your hearts?

Tazameni mikono yangu na miguu yangu, ya kuwa ni mimi mwenyewe. Nishikenishikeni, mwone; kwa kuwa roho haina mwili na mifupa kama mnavyoniona mimi kuwa nayo. Luka 24:39

See my hands and my feet, that it is truly me. Touch me and see, for a spirit doesn't have flesh and bones, as you see that I have."

Na baada ya kusema hayo aliwaonyesha mikono yake na miguu yake. Luka 24:40

When he had said this, he showed them his hands and his feet.

Basi walipokuwa hawajaamini kwa furaha, huku wakistaajabu, aliwaambia, Mna chakula cho chote hapa? Luka 24:41

While they still didn't believe for joy, and wondered, he said to them, "Do you have anything here to eat?"

Wakampa kipande cha samaki wa kuokwa. Luka 24:42

They gave him a piece of a broiled fish and some honeycomb.

Akakitwaa, akala mbele yao. Luka 24:43

He took them, and ate in front of them.

Kisha akawaambia, Hayo ndiyo maneno yangu niliyowaambia nilipokuwa nikali pamoja nanyi, ya kwamba ni lazima yatimizwe yote niliyoandikiwa katika Torati ya Musa, na katika Manabii na Zaburi. Luka 24:44

He said to them, "This is what I told you, while I was still with you, that all things which are written in the law of Moses, the prophets, and the psalms, concerning me must be fulfilled."

Ndipo akawafunulia akili zao wapate kuelewa na maandiko. Luka 24:45

Then he opened their minds, that they might understand the Scriptures.

Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, kwamba Kristo atateswa na kufufuka siku ya tatu; Luka 24:46

He said to them, "Thus it is written, and thus it was necessary for the Christ to suffer and to rise from the dead the third day,

na kwamba mataifa yote watahubiriwa kwa jina lake habari ya toba na ondoleo la dhambi, kuanza tangu Yerusalemu. Luka 24:47

and that repentance and remission of sins should be preached in his name to all the nations, beginning at Jerusalem.

Nanyi ndinyi mashahidi wa mambo haya. Luka 24:48

You are witnesses of these things.

Na tazama, nawaletea juu yenu ahadi ya Baba yangu; lakini kaeni humu mjini, hata mvikwe uwezo utokao juu. Luka 24:49

Behold, I send forth the promise of my Father on you. But wait in the city of Jerusalem until you are clothed with power from on high."

Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki. Luka 24:50

He led them out as far as Bethany, and he lifted up his hands, and blessed them.

Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni. Luka 24:51

It happened, while he blessed them, that he withdrew from them, and was carried up into heaven.

Wakamwabudu; kisha wakarudi Yerusalemu wenye furaha kuu. Luka 24:52

They worshiped him, and returned to Jerusalem with great joy,

Nao walikuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu. Luka 24:53

and were continually in the temple, praising and blessing God. Amen.