Yohana 4 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 4 (Swahili) John 4 (English)

Kwa hiyo Bwana, alipofahamu ya kuwa Mafarisayo wamesikia ya kwamba, Yesu anafanya wanafunzi wengi kuliko Yohana, na kuwabatiza, Yohana 4:1

Therefore when the Lord knew that the Pharisees had heard that Jesus was making and baptizing more disciples than John

(lakini Yesu mwenyewe hakubatiza, bali wanafunzi wake,) Yohana 4:2

(although Jesus himself didn't baptize, but his disciples),

aliacha Uyahudi, akaenda zake tena mpaka Galilaya. Yohana 4:3

he left Judea, and departed into Galilee.

Naye alikuwa hana budi kupita katikati ya Samaria. Yohana 4:4

He needed to pass through Samaria.

Basi akafika kunako mji wa Samaria, uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusufu mwanawe. Yohana 4:5

So he came to a city of Samaria, called Sychar, near the parcel of ground that Jacob gave to his son, Joseph.

Na hapo palikuwa na kisima cha Yakobo. Basi Yesu, kwa sababu amechoka kwa safari yake, akaketi vivi hivi kisimani. Nayo ilikuwa yapata saa sita. Yohana 4:6

Jacob's well was there. Jesus therefore, being tired from his journey, sat down by the well. It was about the sixth hour{noon}.

Akaja mwanamke Msamaria kuteka maji. Yesu akamwambia, Nipe maji ninywe. Yohana 4:7

A woman of Samaria came to draw water. Jesus said to her, "Give me a drink."

Kwa maana wanafunzi wake wamekwenda mjini kununua chakula. Yohana 4:8

For his disciples had gone away into the city to buy food.

Basi yule mwanamke Msamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke Msamaria? (Maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.) Yohana 4:9

The Samaritan woman therefore said to him, "How is it that you, being a Jew, ask for a drink from me, a Samaritan woman?" (For Jews have no dealings with Samaritans.)

Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai. Yohana 4:10

Jesus answered her, "If you knew the gift of God, and who it is who says to you, 'Give me a drink,' you would have asked him, and he would have given you living water."

Yule mwanamke akamwambia, Bwana, huna kitu cha kutekea, na kisima ni kirefu; basi umeyapata wapi hayo maji yaliyo hai? Yohana 4:11

The woman said to him, "Sir, you have nothing to draw with, and the well is deep. From where then have you that living water?

Je! Wewe u mkubwa kuliko baba yetu, Yakobo, aliyetupa kisima hiki, naye mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na wanyama wake? Yohana 4:12

Are you greater than our father, Jacob, who gave us the well, and drank of it himself, as did his children, and his cattle?"

Yesu akajibu, akamwambia, Kila anywaye maji haya ataona kiu tena; Yohana 4:13

Jesus answered her, "Everyone who drinks of this water will thirst again,

walakini ye yote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele. Yohana 4:14

but whoever drinks of the water that I will give him will never thirst again; but the water that I will give him will become in him a well of water springing up to eternal life."

Yule mwanamke akamwambia, Bwana, unipe maji hayo, nisione kiu, wala nisije hapa kuteka. Yohana 4:15

The woman said to him, "Sir, give me this water, so that I don't get thirsty, neither come all the way here to draw."

Yesu akamwambia, Nenda kamwite mumeo, uje naye hapa. Yohana 4:16

Jesus said to her, "Go, call your husband, and come here."

Yule mwanamke akajibu, akasema, Sina mume. Yesu akamwambia, Umesema vema, Sina mume; Yohana 4:17

The woman answered, "I have no husband." Jesus said to her, "You said well, 'I have no husband,'

kwa maana umekuwa na waume watano, naye uliye naye sasa siye mume wako; hapo umesema kweli. Yohana 4:18

for you have had five husbands; and he whom you now have is not your husband. This you have said truly."

Yule mwanamke akamwambia, Bwana, naona ya kuwa u nabii! Yohana 4:19

The woman said to him, "Sir, I perceive that you are a prophet.

Baba zetu waliabudu katika mlima huu, nanyi husema ya kwamba huko Yerusalemu ni mahali patupasapo kuabudia. Yohana 4:20

Our fathers worshiped in this mountain, and you Jews say that in Jerusalem is the place where people ought to worship."

Yesu akamwambia, Mama, unisadiki, saa inakuja ambayo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala kule Yerusalemu. Yohana 4:21

Jesus said to her, "Woman, believe me, the hour comes, when neither in this mountain, nor in Jerusalem, will you worship the Father.

Ninyi mnaabudu msichokijua; sisi tunaabudu tukijuacho; kwa kuwa wokovu watoka kwa Wayahudi. Yohana 4:22

You worship that which you don't know. We worship that which we know; for salvation is from the Jews.

Lakini saa inakuja, nayo sasa ipo, ambayo waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba awatafuta watu kama hao wamwabudu. Yohana 4:23

But the hour comes, and now is, when the true worshippers will worship the Father in spirit and truth, for the Father seeks such to be his worshippers.

Mungu ni Roho, nao wamwabuduo yeye imewapasa kumwabudu katika roho na kweli. Yohana 4:24

God is spirit, and those who worship him must worship in spirit and truth."

Yule mwanamke akamwambia, Najua ya kuwa yuaja Masihi, (aitwaye Kristo); naye atakapokuja, yeye atatufunulia mambo yote. Yohana 4:25

The woman said to him, "I know that Messiah comes," (he who is called Christ). "When he has come, he will declare to us all things."

Yesu akamwambia, Mimi ninayesema nawe, ndiye. Yohana 4:26

Jesus said to her, "I am he, the one who speaks to you."

Mara hiyo wakaja wanafunzi wake, wakastaajabu kwa sababu alikuwa akisema na mwanamke; lakini hakuna aliyesema, Unatafuta nini? Au, Mbona unasema naye? Yohana 4:27

At this, his disciples came. They marveled that he was speaking with a woman; yet no one said, "What are you looking for?" or, "Why do you speak with her?"

Basi yule mwanamke akauacha mtungi wake, akaenda zake mjini, akawaambia watu, Yohana 4:28

So the woman left her water pot, and went away into the city, and said to the people,

Njoni, mtazame mtu aliyeniambia mambo yote niliyoyatenda. Je! Haimkini huyu kuwa ndiye Kristo? Yohana 4:29

"Come, see a man who told me everything that I did. Can this be the Christ?"

Basi wakatoka mjini, wakamwendea. Yohana 4:30

They went out of the city, and were coming to him.

Huko nyuma wanafunzi wakamsihi wakisema, Rabi, ule. Yohana 4:31

In the meanwhile, the disciples urged him, saying, "Rabbi, eat."

Akawaambia, Mimi ninacho chakula msichokijua ninyi. Yohana 4:32

But he said to them, "I have food to eat that you don't know about."

Basi wanafunzi wake wakasemezana, Je! Mtu amemletea chakula? Yohana 4:33

The disciples therefore said one to another, "Has anyone brought him something to eat?"

Yesu akawaambia, Chakula changu ndicho hiki, niyatende mapenzi yake aliyenipeleka, nikaimalize kazi yake. Yohana 4:34

Jesus said to them, "My food is to do the will of him who sent me, and to accomplish his work.

Hamsemi ninyi, Bado miezi minne, ndipo yaja mavuno? Tazama, mimi nawaambieni, Inueni macho yenu myatazame mashamba, ya kuwa yamekwisha kuwa meupe, tayari kwa mavuno. Yohana 4:35

Don't you say, 'There are yet four months until the harvest?' Behold, I tell you, lift up your eyes, and look at the fields, that they are white for harvest already.

Naye avunaye hupokea mshahara, na kukusanya matunda kwa uzima wa milele, ili yeye apandaye na yeye avunaye wapate kufurahi pamoja. Yohana 4:36

He who reaps receives wages, and gathers fruit to eternal life; that both he who sows and he who reaps may rejoice together.

Kwa maana hapo neno hilo huwa kweli, Mmoja hupanda akavuna mwingine. Yohana 4:37

For in this the saying is true, 'One sows, and another reaps.'

Mimi naliwatuma myavune yale msiyoyataabikia; wengine walitaabika, nanyi mmeingia katika taabu yao. Yohana 4:38

I sent you to reap that for which you haven't labored. Others have labored, and you have entered into their labor."

Na katika mji ule Wasamaria wengi walimwamini kwa sababu ya neno la yule mwanamke, aliyeshuhudia kwamba, Aliniambia mambo yote niliyoyatenda. Yohana 4:39

From that city many of the Samaritans believed in him because of the word of the woman, who testified, "He told me everything that I did."

Basi wale Wasamaria walipomwendea, walimsihi akae kwao; naye akakaa huko siku mbili. Yohana 4:40

So when the Samaritans came to him, they begged him to stay with them. He stayed there two days.

Watu wengi zaidi wakaamini kwa sababu ya neno lake. Yohana 4:41

Many more believed because of his word.

Wakamwambia yule mwanamke, Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu; maana sisi tumesikia wenyewe, tena twajua ya kuwa hakika huyu ndiye Mwokozi wa ulimwengu. Yohana 4:42

They said to the woman, "Now we believe, not because of your speaking; for we have heard for ourselves, and know that this is indeed the Christ, the Savior of the world."

Na baada ya siku mbili hizo akaondoka huko, akaenda Galilaya. Yohana 4:43

After the two days he went out from there and went into Galilee.

Kwa maana Yesu mwenyewe alishuhudia ya kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe. Yohana 4:44

For Jesus himself testified that a prophet has no honor in his own country.

Basi alipotoka Galilaya, Wagalilaya walimpokea; kwa kuwa wameyaona mambo yote aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa sikukuu; maana hao nao waliiendea sikukuu. Yohana 4:45

So when he came into Galilee, the Galileans received him, having seen all the things that he did in Jerusalem at the feast, for they also went to the feast.

Basi alifika tena Kana ya Galilaya, hapo alipoyafanya yale maji kuwa divai. Na palikuwa na diwani mmoja ambaye mwanawe hawezi huko Kapernaumu. Yohana 4:46

Jesus came therefore again to Cana of Galilee, where he made the water into wine. There was a certain nobleman whose son was sick at Capernaum.

Huyo aliposikia ya kwamba Yesu amekuja kutoka Uyahudi mpaka Galilaya, alimwendea, akamsihi ashuke na kumponya mwanawe; kwa maana alikuwa kufani. Yohana 4:47

When he heard that Jesus had come out of Judea into Galilee, he went to him, and begged him that he would come down and heal his son, for he was at the point of death.

Basi Yesu akamwambia, Msipoona ishara na maajabu hamtaamini kabisa? Yohana 4:48

Jesus therefore said to him, "Unless you see signs and wonders, you will in no way believe."

Yule diwani akamwambia, Bwana, ushuke asijakufa mtoto wangu. Yohana 4:49

The nobleman said to him, "Sir, come down before my child dies."

Yesu akamwambia, Enenda; mwanao yu hai. Mtu yule akalisadiki lile neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia. Yohana 4:50

Jesus said to him, "Go your way. Your son lives." The man believed the word that Jesus spoke to him, and he went his way.

Hata alipokuwa akishuka, watumwa wake walimlaki, wakisema ya kwamba mtoto wake yu hai. Yohana 4:51

As he was now going down, his servants met him and reported, saying "Your child lives!"

Basi akawauliza habari ya saa alipoanza kuwa hajambo; nao wakamwambia, Jana, saa saba, homa ilimwacha. Yohana 4:52

So he inquired of them the hour when he began to get better. They said therefore to him, "Yesterday at the seventh hour,{1:00 P. M.} the fever left him."

Basi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai. Akaamini yeye na wote wa nyumbani mwake. Yohana 4:53

So the father knew that it was at that hour in which Jesus said to him, "Your son lives." He believed, as did his whole house.

Hiyo ni ishara ya pili aliyoifanya Yesu, alipokuwa ametoka Uyahudi kufika Galilaya. Yohana 4:54

This is again the second sign that Jesus did, having come out of Judea into Galilee.