Yohana 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 20 (Swahili) John 20 (English)

Hata siku ya kwanza ya juma Mariamu Magdalene alikwenda kaburini alfajiri, kungali giza bado; akaliona lile jiwe limeondolewa kaburini. Yohana 20:1

Now on the first day of the week, Mary Magdalene went early, while it was still dark, to the tomb, and saw the stone taken away from the tomb.

Basi akaenda mbio, akafika kwa Simoni Petro na kwa yule mwanafunzi mwingine ambaye Yesu alimpenda, akawaambia, Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka. Yohana 20:2

Therefore she ran and came to Simon Peter, and to the other disciple whom Jesus loved, and said to them, "They have taken away the Lord out of the tomb, and we don't know where they have laid him!"

Basi Petro akatoka, na yule mwanafunzi mwingine, wakashika njia kwenda kaburini. Yohana 20:3

Therefore Peter and the other disciple went out, and they went toward the tomb.

Wakaenda mbio wote wawili; na yule mwanafunzi mwingine akaenda mbio upesi kuliko Petro, akawa wa kwanza kufika kaburini. Yohana 20:4

They both ran together. The other disciple outran Peter, and came to the tomb first.

Akainama na kuchungulia, akaona vitambaa vya sanda vimelala; lakini hakuingia. Yohana 20:5

Stooping and looking in, he saw the linen cloths lying, yet he didn't enter in.

Basi akaja na Simoni Petro, akaingia ndani ya kaburi; akavitazama vitambaa vilivyolala, Yohana 20:6

Then Simon Peter came, following him, and entered into the tomb. He saw the linen cloths lying,

na ile leso iliyokuwako kichwani pake; haikulala pamoja na vitambaa, bali imezongwa-zongwa mbali mahali pa peke yake. Yohana 20:7

and the cloth that had been on his head, not lying with the linen cloths, but rolled up in a place by itself.

Basi ndipo alipoingia naye yule mwanafunzi mwingine aliyekuwa wa kwanza wa kufika kaburini, akaona na kuamini. Yohana 20:8

So then the other disciple who came first to the tomb also entered in, and he saw and believed.

Kwa maana hawajalifahamu bado andiko, ya kwamba imempasa kufufuka. Yohana 20:9

For as yet they didn't know the Scripture, that he must rise from the dead.

Basi wale wanafunzi wakaenda zao tena nyumbani kwao. Yohana 20:10

So the disciples went away again to their own homes.

Lakini Mariamu alikuwa akisimama karibu na kaburi, nje yake, analia. Basi akilia hivi, aliinama na kuchungulia ndani ya kaburi. Yohana 20:11

But Mary was standing outside at the tomb weeping. So, as she wept, she stooped and looked into the tomb,

Akaona malaika wawili, wenye mavazi meupe, wameketi, mmoja kichwani na mmoja miguuni, hapo ulipolazwa mwili wake Yesu. Yohana 20:12

and she saw two angels in white sitting, one at the head, and one at the feet, where the body of Jesus had lain.

Nao wakamwambia, Mama, unalilia nini? Akawaambia, Kwa sababu wamemwondoa Bwana wangu, wala mimi sijui walikomweka. Yohana 20:13

They told her, "Woman, why are you weeping?" She said to them, "Because they have taken away my Lord, and I don't know where they have laid him."

Naye akiisha kusema hayo, akageuka nyuma, akamwona Yesu amesimama, asijue ya kuwa ni Yesu. Yohana 20:14

When she had said this, she turned around and saw Jesus standing, and didn't know that it was Jesus.

Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana, ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa. Yohana 20:15

Jesus said to her, "Woman, why are you weeping? Who are you looking for?" She, supposing him to be the gardener, said to him, "Sir, if you have carried him away, tell me where you have laid him, and I will take him away."

Yesu akamwambia, Mariamu. Yeye akageuka, akamwambia kwa Kiebrania, Raboni! (Yaani, Mwalimu wangu). Yohana 20:16

Jesus said to her, "Mary." She turned and said to him, "Rhabbouni!" which is to say, "Teacher!"

Yesu akamwambia. Usinishike; kwa maana sijapaa kwenda kwa Baba. Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu. Yohana 20:17

Jesus said to her, "Don't touch me, for I haven't yet ascended to my Father; but go to my brothers, and tell them, 'I am ascending to my Father and your Father, to my God and your God.'"

Mariamu Magdalene akaenda, akawapasha wanafunzi habari ya kwamba, Nimemwona Bwana, na ya kwamba amemwambia hayo. Yohana 20:18

Mary Magdalene came and told the disciples that she had seen the Lord, and that he had said these things to her.

Ikawa jioni, siku ile ya kwanza ya juma, pale walipokuwapo wanafunzi, milango imefungwa kwa hofu ya Wayahudi; akaja Yesu, akasimama katikati, akawaambia, Amani iwe kwenu. Yohana 20:19

When therefore it was evening, on that day, the first day of the week, and when the doors were locked where the disciples were assembled, for fear of the Jews, Jesus came and stood in the midst, and said to them, "Peace be to you."

Naye akiisha kusema hayo, akawaonyesha mikono yake na ubavu wake. Basi wale wanafunzi wakafurahi walipomwona Bwana. Yohana 20:20

When he had said this, he showed them his hands and his side. The disciples therefore were glad when they saw the Lord.

Basi Yesu akawaambia tena, Amani iwe kwenu; kama Baba alivyonituma mimi, mimi nami nawapeleka ninyi. Yohana 20:21

Jesus therefore said to them again, "Peace be to you. As the Father has sent me, even so I send you."

Naye akiisha kusema hayo, akawavuvia, akawaambia, Pokeeni Roho Mtakatifu. Yohana 20:22

When he had said this, he breathed on them, and said to them, "Receive the Holy Spirit!

Wo wote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wo wote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa. Yohana 20:23

Whoever's sins you forgive, they are forgiven them. Whoever's sins you retain, they have been retained."

Walakini mmoja wa wale Thenashara, Tomaso, aitwaye Pacha, hakuwako pamoja nao alipokuja Yesu. Yohana 20:24

But Thomas, one of the twelve, called Didymus, wasn't with them when Jesus came.

Basi wanafunzi wengine wakamwambia, Tumemwona Bwana. Akawaambia, Mimi nisipoziona mikononi mwake kovu za misumari, na kutia kidole changu katika mahali pa misumari, na kutia mkono wangu katika ubavu wake, mimi sisadiki hata kidogo. Yohana 20:25

The other disciples therefore said to him, "We have seen the Lord!" But he said to them, "Unless I see in his hands the print of the nails, and put my hand into his side, I will not believe."

Basi, baada ya siku nane, wanafunzi wake walikuwamo ndani tena, na Tomaso pamoja nao. Akaja Yesu, na milango imefungwa, akasimama katikati, akasema, Amani iwe kwenu. Yohana 20:26

After eight days again his disciples were inside, and Thomas was with them. Jesus came, the doors being locked, and stood in the midst, and said, "Peace be to you."

Kisha akamwambia Tomaso, Lete hapa kidole chako; uitazame mikono yangu; ulete na mkono wako uutie ubavuni mwangu, wala usiwe asiyeamini, bali aaminiye. Yohana 20:27

Then he said to Thomas, "Reach here your finger, and see my hands. Reach here your hand, and put it into my side. Don't be unbelieving, but believing."

Tomaso akajibu, akamwambia, Bwana wangu na Mungu wangu! Yohana 20:28

Thomas answered him, "My Lord and my God!"

Yesu akamwambia, Wewe, kwa kuwa umeniona, umesadiki; wa heri wale wasioona, wakasadiki. Yohana 20:29

Jesus said to him, "Because you have seen me,{TR adds " Thomas,"} you have believed. Blessed are those who have not seen, and have believed."

Basi kuna ishara nyingine nyingi alizozifanya Yesu mbele ya wanafunzi wake, zisizoandikwa katika kitabu hiki. Yohana 20:30

Therefore Jesus did many other signs in the presence of his disciples, which are not written in this book;

Lakini hizi zimeandikwa ili mpate kuamini ya kwamba Yesu ndiye Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake. Yohana 20:31

but these are written, that you may believe that Jesus is the Christ, the Son of God, and that believing you may have life in his name.