Yohana 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 16 (Swahili) John 16 (English)

Maneno hayo nimewaambia, msije mkachukizwa. Yohana 16:1

"These things have I spoken to you, so that you wouldn't be caused to stumble.

Watawatenga na masinagogi; naam, saa yaja atakapodhania kila mtu awauaye ya kuwa anamtolea Mungu ibada. Yohana 16:2

They will put you out of the synagogues. Yes, the time comes that whoever kills you will think that he offers service to God.

Na hayo watawatenda kwa sababu hawakumjua Baba wala mimi. Yohana 16:3

They will do these things{TR adds "to you"} because they have not known the Father, nor me.

Lakini nimewaambia hayo, ili makusudi saa ile itakapokuja myakumbuke ya kuwa mimi naliwaambia. Sikuwaambia hayo tangu mwanzo, kwa sababu nalikuwapo pamoja nanyi. Yohana 16:4

But I have told you these things, so that when the time comes, you may remember that I told you about them. I didn't tell you these things from the beginning, because I was with you.

Lakini sasa mimi naenda zangu kwake yeye aliyenipeleka, wala hakuna mmoja wenu aniulizaye, Unakwendapi? Yohana 16:5

But now I am going to him who sent me, and none of you asks me, 'Where are you going?'

Ila kwa sababu nimewaambia hayo huzuni imejaa mioyoni mwenu. Yohana 16:6

But because I have told you these things, sorrow has filled your heart.

Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu. Yohana 16:7

Nevertheless I tell you the truth: It is to your advantage that I go away, for if I don't go away, the Counselor won't come to you. But if I go, I will send him to you.

Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu. Yohana 16:8

When he has come, he will convict the world about sin, about righteousness, and about judgment;

Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi; Yohana 16:9

about sin, because they don't believe in me;

kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena; Yohana 16:10

about righteousness, because I am going to my Father, and you won't see me any more;

kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa. Yohana 16:11

about judgment, because the prince of this world has been judged.

Hata bado nikali ninayo mengi ya kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili hivi sasa. Yohana 16:12

"I have yet many things to tell you, but you can't bear them now.

Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote; kwa maana hatanena kwa shauri lake mwenyewe, lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atawapasha habari yake. Yohana 16:13

However when he, the Spirit of truth, has come, he will guide you into all truth, for he will not speak from himself; but whatever he hears, he will speak. He will declare to you things that are coming.

Yeye atanitukuza mimi, kwa kuwa atatwaa katika yaliyo yangu na kuwapasha habari. Yohana 16:14

He will glorify me, for he will take from what is mine, and will declare it to you.

Na yote aliyo nayo Baba ni yangu; kwa hiyo nalisema ya kwamba atatwaa katika yaliyo yangu, na kuwapasheni habari. Yohana 16:15

All things whatever the Father has are mine; therefore I said that he takes{TR reads "will take" instead of "takes"} of mine, and will declare it to you.

Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni; na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona. Yohana 16:16

A little while, and you will not see me. Again a little while, and you will see me."

Basi baadhi ya wanafunzi wake wakasemezana, Neno gani hilo asemalo, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? Na hilo, Kwa sababu naenda zangu kwa Baba? Yohana 16:17

Some of his disciples therefore said to one another, "What is this that he says to us, 'A little while, and you won't see me, and again a little while, and you will see me;' and, 'Because I go to the Father?'"

Basi walisema, Neno gani hilo asemalo; hilo, Bado kitambo kidogo? Hatujui asemalo. Yohana 16:18

They said therefore, "What is this that he says, 'A little while?' We don't know what he is saying."

Yesu alifahamu ya kwamba wanataka kumwuliza, akawaambia, Ndilo hilo mnaloulizana, ya kuwa nalisema, Bado kitambo kidogo nanyi hamnioni, na tena bado kitambo kidogo nanyi mtaniona? Yohana 16:19

Therefore Jesus perceived that they wanted to ask him, and he said to them, "Do you inquire among yourselves concerning this, that I said, 'A little while, and you won't see me, and again a little while, and you will see me?'

Amin, amin, nawaambia, Ninyi mtalia na kuomboleza, bali ulimwengu utafurahi; ninyi mtahuzunishwa, lakini huzuni yenu itageuka kuwa furaha. Yohana 16:20

Most assuredly I tell you, that you will weep and lament, but the world will rejoice. You will be sorrowful, but your sorrow will be turned into joy.

Mwanamke azaapo, yuna huzuni kwa kuwa saa yake imefika; lakini akiisha kuzaa mwana, haikumbuki tena ile dhiki, kwa sababu ya furaha ya kuzaliwa mtu ulimwenguni. Yohana 16:21

A woman, when she gives birth, has sorrow, because her time has come. But when she has delivered the child, she doesn't remember the anguish any more, for the joy that a human being is born into the world.

Basi ninyi hivi sasa mna huzuni; lakini mimi nitawaona tena; na mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye. Yohana 16:22

Therefore you now have sorrow, but I will see you again, and your heart will rejoice, and no one will take your joy away from you.

Tena siku ile hamtaniuliza neno lo lote. Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Yohana 16:23

"In that day you will ask me no questions. Most assuredly I tell you, whatever you may ask of the Father in my name, he will give it to you.

Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. Yohana 16:24

Until now, you have asked nothing in my name. Ask, and you will receive, that your joy may be made full.

Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambapo sitasema nanyi tena kwa mithali, lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba. Yohana 16:25

I have spoken these things to you in figures of speech. But the time is coming when I will no more speak to you in figures of speech, but will tell you plainly about the Father.

Na siku ile mtaomba kwa jina langu, wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba; Yohana 16:26

In that day you will ask in my name; and I don't say to you, that I will pray to the Father for you,

kwa maana Baba mwenyewe awapenda kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, na kusadiki ya kwamba mimi nalitoka kwa Baba. Yohana 16:27

for the Father himself loves you, because you have loved me, and have believed that I came forth from God.

Nalitoka kwa Baba, nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; na kwenda kwa Baba. Yohana 16:28

I came out from the Father, and have come into the world. Again, I leave the world, and go to the Father."

Basi wanafunzi wake wakasema, Tazama, sasa wasema waziwazi, wala huneni mithali yo yote. Yohana 16:29

His disciples said to him, "Behold, now you speak plainly, and speak no figures of speech.

Sasa tumejua ya kuwa wewe wafahamu mambo yote, wala huna haja ya mtu akuulize; kwa hiyo twasadiki ya kwamba ulitoka kwa Mungu. Yohana 16:30

Now we know that you know all things, and don't need for anyone to question you. By this we believe that you came forth from God."

Yesu akawajibu, Je! Mnasadiki sasa? Yohana 16:31

Jesus answered them, "Do you now believe?

Tazama, saa yaja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami. Yohana 16:32

Behold, the time is coming, yes, and has now come, that you will be scattered, everyone to his own place, and you will leave me alone. Yet I am not alone, because the Father is with me.

Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. Yohana 16:33

I have told you these things, that in me you may have peace. In the world you have oppression; but cheer up! I have overcome the world."