Yohana 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 9 (Swahili) John 9 (English)

Hata alipokuwa akipita alimwona mtu, kipofu tangu kuzaliwa. Yohana 9:1

As he passed by, he saw a man blind from birth.

Wanafunzi wake wakamwuliza wakisema, Rabi, ni yupi aliyetenda dhambi, mtu huyu au wazazi wake, hata azaliwe kipofu? Yohana 9:2

His disciples asked him, "Rabbi, who sinned, this man or his parents, that he was born blind?"

Yesu akajibu, Huyu hakutenda dhambi, wala wazazi wake; bali kazi za Mungu zidhihirishwe ndani yake. Yohana 9:3

Jesus answered, "Neither did this man sin, nor his parents; but, that the works of God might be revealed in him.

Imetupasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenipeleka maadamu ni mchana, usiku waja asipoweza mtu kufanya kazi. Yohana 9:4

I must work the works of him who sent me, while it is day. The night is coming, when no one can work.

Muda nilipo ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu. Yohana 9:5

While I am in the world, I am the light of the world."

Alipokwisha kusema hayo, alitema mate chini, akafanya tope kwa yale mate. Akampaka kipofu tope za macho, Yohana 9:6

When he had said this, he spat on the ground, made mud with the saliva, anointed the blind man's eyes with the mud,

akamwambia, Nenda kanawe katika birika ya Siloamu, (maana yake, Aliyetumwa). Basi akaenda na kunawa; akarudi anaona. Yohana 9:7

and said to him, "Go, wash in the pool of Siloam" (which means "Sent"). So he went away, washed, and came back seeing.

Basi jirani zake, na wale waliomwona zamani kuwa ni mwombaji, wakasema, Je! Huyu siye yule aliyekuwa akiketi na kuomba? Yohana 9:8

The neighbors therefore, and those who saw that he was blind before, said, "Isn't this he who sat and begged?"

Wengine wakasema, Ndiye. Wengine wakasema, La, lakini amefanana naye. Yeye mwenyewe alisema, Mimi ndiye. Yohana 9:9

Others were saying, "It is he." Still others were saying, "He looks like him." He said, "I am he."

Basi wakamwambia, Macho yako yalifumbuliwaje? Yohana 9:10

They therefore were asking him, "How were your eyes opened?"

Yeye akajibu, Mtu yule aitwaye Yesu alifanya tope, akanipaka macho akaniambia, Nenda Siloamu ukanawe; basi nikaenda na kunawa, nikapata kuona. Yohana 9:11

He answered, "A man called Jesus made mud, anointed my eyes, and said to me, 'Go to the pool of Siloam, and wash.' So I went away and washed, and I received sight."

Wakamwambia, Yuko wapi huyo? Akasema, Mimi sijui. Yohana 9:12

Then they asked him, "Where is he?" He said, "I don't know."

Basi wakampeleka kwa Mafarisayo yule aliyekuwa kipofu zamani. Yohana 9:13

They brought him who had been blind to the Pharisees.

Nayo ilikuwa sabato, hapo Yesu alipofanya zile tope na kumfumbua macho. Yohana 9:14

It was a Sabbath when Jesus made the mud and opened his eyes.

Basi Mafarisayo nao wakamwuliza tena jinsi gani alivyopata kuona. Akawaambia, Alinitia tope juu ya macho, nami nikanawa, na sasa naona. Yohana 9:15

Again therefore the Pharisees also asked him how he received his sight. He said to them, "He put mud on my eyes, I washed, and I see."

Basi baadhi ya Mafarisayo wakasema, Mtu huyo hakutoka kwa Mungu, kwa sababu haishiki sabato. Wengine wakasema, Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya ishara kama hizo? Kukawa matengano kati yao. Yohana 9:16

Some therefore of the Pharisees said, "This man is not from God, because he doesn't keep the Sabbath." Others said, "How can a man who is a sinner do such signs?" There was division among them.

Basi wakamwambia yule kipofu mara ya pili, Wewe wasemaje katika habari zake kwa vile alivyokufumbua macho? Akasema, Ni nabii. Yohana 9:17

Therefore they asked the blind man again, "What do you say about him, because he opened your eyes?" He said, "He is a prophet."

Basi Wayahudi hawakusadiki habari zake, ya kuwa alikuwa kipofu, kisha akapata kuona; hata walipowaita wazazi wake yule aliyepata kuona. Yohana 9:18

The Jews therefore did not believe concerning him, that he had been blind, and had received his sight, until they called the parents of him who had received his sight,

Wakawauliza wakisema, Huyu ndiye mwana wenu, ambaye mnasema kwamba alizaliwa kipofu? Amepataje, basi, kuona sasa? Yohana 9:19

and asked them, "Is this your son, who you say was born blind? How then does he now see?"

Wazazi wake wakawajibu, wakasema, Tunajua ya kuwa huyu ndiye mwana wetu, tena ya kuwa alizaliwa kipofu; Yohana 9:20

His parents answered them, "We know that this is our son, and that he was born blind;

lakini jinsi aonavyo sasa hatujui; wala hatujui ni nani aliyemfumbua macho. Mwulizeni yeye mwenyewe; yeye ni mtu mzima; atajisemea mwenyewe. Yohana 9:21

but how he now sees, we don't know; or who opened his eyes, we don't know. He is of age. Ask him. He will speak for himself."

Wazazi wake waliyasema hayo kwa sababu waliwaogopa Wayahudi; kwa maana Wayahudi walikuwa wamekwisha kuafikiana kwamba mtu akimkiri kuwa ni Kristo, atatengwa na sinagogi. Yohana 9:22

His parents said these things because they feared the Jews; for the Jews had already agreed that if any man would confess him as Christ, he would be put out of the synagogue.

Ndiyo sababu wale wazazi wake walisema, Ni mtu mzima, mwulizeni yeye. Yohana 9:23

Therefore his parents said, "He is of age. Ask him."

Basi mara ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu, wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyo ni mwenye dhambi. Yohana 9:24

So they called the man who was blind a second time, and said to him, "Give glory to God. We know that this man is a sinner."

Basi yule mtu akajibu, Kwamba yeye ni mwenye dhambi sijui. Najua neno moja, kuwa mimi nalikuwa kipofu na sasa naona. Yohana 9:25

He therefore answered, "I don't know if he is a sinner. One thing I do know: that though I was blind, now I see."

Basi wakamwambia, Alikutendea nini? Alikufumbua macho jinsi gani? Yohana 9:26

They said to him again, "What did he do to you? How did he open your eyes?"

Akawajibu, Nimekwisha kuwaambia, wala hamkusikia; mbona mnataka kusikia tena? Ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake? Yohana 9:27

He answered them, "I told you already, and you didn't listen. Why do you want to hear it again? You don't also want to become his disciples, do you?"

Basi wakamshutumu, wakasema, Wewe u mwanafunzi wake yule; sisi tu wanafunzi wa Musa. Yohana 9:28

They insulted him and said, "You are his disciple, but we are disciples of Moses.

Sisi tunajua ya kuwa Mungu alisema na Musa; bali yule hatujui atokako. Yohana 9:29

We know that God has spoken to Moses. But as for this man, we don't know where he comes from."

Yule mtu akajibu, akawaambia, Hii ni ajabu! Kwamba ninyi hamjui atokako, naye alinifumbua macho! Yohana 9:30

The man answered them, "How amazing! You don't know where he comes from, yet he opened my eyes.

Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo. Yohana 9:31

We know that God doesn't listen to sinners, but if anyone is a worshipper of God, and does his will, he listens to him.

Tokea hapo haijasikiwa ya kuwa mtu ameyafumbua macho ya kipofu, ambaye alizaliwa hali hiyo. Yohana 9:32

Since the world began it has never been heard of that anyone opened the eyes of someone born blind.

Kama huyo asingalitoka kwa Mungu, asingeweza kutenda neno lo lote. Yohana 9:33

If this man were not from God, he could do nothing."

Wakajibu, wakamwambia, Ama! Wewe ulizaliwa katika dhambi tupu, nawe unatufundisha sisi? Wakamtoa nje. Yohana 9:34

They answered him, "You were altogether born in sins, and do you teach us?" They threw him out.

Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; naye alipomwona alisema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu? Yohana 9:35

Jesus heard that they had thrown him out, and finding him, he said, "Do you believe in the Son of God?"

Naye akajibu akasema, Ni nani, Bwana, nipate kumwamini? Yohana 9:36

He answered, "Who is he, Lord, that I may believe in him?"

Yesu akamwambia, Umemwona, naye anayesema nawe ndiye. Yohana 9:37

Jesus said to him, "You have both seen him, and it is he who speaks with you."

Akasema, Naamini, Bwana. Akamsujudia. Yohana 9:38

He said, "Lord, I believe!" and he worshiped him.

Yesu akasema, Mimi nimekuja ulimwenguni humu kwa hukumu, ili wao wasioona waone, nao wanaoona wawe vipofu. Yohana 9:39

Jesus said, "I came into this world for judgment, that those who don't see may see; and that those who see may become blind."

Baadhi ya Mafarisayo waliokuwapo pamoja naye wakasikia hayo, wakamwambia, Je! Sisi nasi tu vipofu? Yohana 9:40

Those of the Pharisees who were with him heard these things, and said to him, "Are we also blind?"

Yesu akawaambia, Kama mngekuwa vipofu, msingekuwa na dhambi; lakini sasa mwasema, Twaona; basi dhambi yenu inakaa. Yohana 9:41

Jesus said to them, "If you were blind, you would have no sin; but now you say, 'We see.' Therefore your sin remains.