Yohana 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 10 (Swahili) John 10 (English)

Yesu aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang'anyi. Yohana 10:1

"Most assuredly, I tell you, one who doesn't enter by the door into the sheep fold, but climbs up some other way, the same is a thief and a robber.

Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. Yohana 10:2

But one who enters in by the door is the shepherd of the sheep.

Bawabu humfungulia huyo, na kondoo humsikia sauti yake; naye huwaita kondoo wake kwa majina yao, na kuwapeleka nje. Yohana 10:3

The gatekeeper opens the gate for him, and the sheep listen to his voice. He calls his own sheep by name, and leads them out.

Naye awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. Yohana 10:4

Whenever he brings out his own sheep, he goes before them, and the sheep follow him, for they know his voice.

Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni. Yohana 10:5

They will by no means follow a stranger, but will flee from him; for they don't know the voice of strangers."

Mithali hiyo Yesu aliwaambia, lakini wao hawakuelewa na mambo hayo aliyowaambia. Yohana 10:6

Jesus spoke this parable to them, but they didn't understand what he was telling them.

Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo. Yohana 10:7

Jesus therefore said to them again, "Most assuredly, I tell you, I am the sheep's door.

Wote walionitangulia ni wevi na wanyang'anyi; lakini kondoo hawakuwasikia. Yohana 10:8

All who came before me are thieves and robbers, but the sheep didn't listen to them.

Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. Yohana 10:9

I am the door. If anyone enters in by me, he will be saved, and will go in and go out, and will find pasture.

Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele. Yohana 10:10

The thief only comes to steal, kill, and destroy. I came that they may have life, and may have it abundantly.

Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo. Yohana 10:11

I am the good shepherd. The good shepherd lays down his life for the sheep.

Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya. Yohana 10:12

He who is a hired hand, and not a shepherd, who doesn't own the sheep, sees the wolf coming, leaves the sheep, and flees. The wolf snatches the sheep, and scatters them.

Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake. Yohana 10:13

The hired hand flees because he is a hired hand, and doesn't care for the sheep.

Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi; Yohana 10:14

I am the good shepherd. I know my own, and I'm known by my own;

kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo. Yohana 10:15

even as the Father knows me, and I know the Father. I lay down my life for the sheep.

Na kondoo wengine ninao, ambao si wa zizi hili; na hao nao imenipasa kuwaleta; na sauti yangu wataisikia; kisha kutakuwako kundi moja na mchungaji mmoja. Yohana 10:16

I have other sheep, which are not of this fold. I must bring them also, and they will hear my voice. They will become one flock with one shepherd.

Ndiposa Baba anipenda, kwa sababu nautoa uhai wangu ili niutwae tena. Yohana 10:17

Therefore the Father loves me, because I lay down my life, that I may take it again.

Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nalilipokea kwa Baba yangu. Yohana 10:18

No one takes it away from me, but I lay it down by myself. I have power to lay it down, and I have power to take it again. I received this commandment from my Father."

Kukaingia tena matengano kati ya Wayahudi, kwa ajili ya maneno hayo. Yohana 10:19

Therefore a division arose again among the Jews because of these words.

Wengi wao wakasema, Ana pepo huyu, tena ana wazimu; mbona mnamsikiliza? Yohana 10:20

Many of them said, "He has a demon, and is insane! Why do you listen to him?"

Wengine wakasema, Maneno hayo siyo ya mtu mwenye pepo. Je! Pepo aweza kuwafumbua macho vipofu? Yohana 10:21

Others said, "These are not the sayings of one possessed by a demon. It isn't possible for a demon to open the eyes of the blind, is it?"

Basi huko Yerusalemu ilikuwa Sikukuu ya Kutabaruku; ni wakati wa baridi. Yohana 10:22

It was the Feast of the Dedication{The "Feast of the Dedication" is the Greek name for "Chanukkah," a celebration of the rededication of the Temple.} at Jerusalem.

Naye Yesu alikuwa akitembea hekaluni, katika ukumbi wa Sulemani. Yohana 10:23

It was winter, and Jesus was walking in the temple, in Solomon's porch.

Basi Wayahudi walimzunguka, wakamwambia, Hata lini utatuhangaisha nafsi zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi. Yohana 10:24

The Jews therefore came around him and said to him, "How long will you hold us in suspense? If you are the Christ, tell us plainly."

Yesu akawajibu, Naliwaambia, lakini ninyi hamsadiki. Kazi hizi ninazozifanya kwa jina la Baba yangu ndizo zinazonishuhudia. Yohana 10:25

Jesus answered them, "I told you, and you don't believe. The works that I do in my Father's name, these testify about me.

Lakini ninyi hamsadiki, kwa sababu hammo miongoni mwa kondoo wangu. Yohana 10:26

But you don't believe, because you are not of my sheep, as I told you.

Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Yohana 10:27

My sheep hear my voice, and I know them, and they follow me.

Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. Yohana 10:28

I give eternal life to them. They will never perish, and no one will snatch them out of my hand.

Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Yohana 10:29

My Father, who has given them to me, is greater than all. No one is able to snatch them out of my Father's hand.

Mimi na Baba tu umoja. Yohana 10:30

I and the Father are one."

Basi Wayahudi wakaokota mawe tena ili wampige. Yohana 10:31

Therefore Jews took up stones again to stone him.

Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonyesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe? Yohana 10:32

Jesus answered them, "I have shown you many good works from my Father. For which of those works do you stone me?"

Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu. Yohana 10:33

The Jews answered him, "We don't stone you for a good work, but for blasphemy: because you, being a man, make yourself God."

Yesu akawajibu, Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? Yohana 10:34

Jesus answered them, "Isn't it written in your law, 'I said, you are gods?'

Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka); Yohana 10:35

If he called them gods, to whom the word of God came (and the Scripture can't be broken),

je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu? Yohana 10:36

Do you say of him whom the Father sanctified and sent into the world, 'You blaspheme,' because I said, 'I am the Son of God?'

Kama sizitendi kazi za Baba yangu, msiniamini; Yohana 10:37

If I don't do the works of my Father, don't believe me.

lakini nikizitenda, ijapokuwa hamniamini mimi, ziaminini zile kazi; mpate kujua na kufahamu ya kuwa Baba yu ndani yangu, nami ni ndani ya Baba. Yohana 10:38

But if I do them, though you don't believe me, believe the works; that you may know and believe that the Father is in me, and I in the Father."

Wakatafuta tena kumkamata; lakini akatoka mikononi mwao. Yohana 10:39

They sought again to seize him, and he went out of their hand.

Akaenda zake tena ng'ambo ya Yordani, mpaka mahali pale alipokuwapo Yohana akibatiza hapo kwanza, akakaa huko. Yohana 10:40

He went away again beyond the Jordan into the place where John was baptizing at first, and there he stayed.

Na watu wengi wakamwendea, wakasema, Yohana kweli hakufanya ishara yo yote, lakini yote aliyoyasema Yohana katika habari zake huyu yalikuwa kweli. Yohana 10:41

Many came to him. They said, "John indeed did no sign, but everything that John said about this man is true."

Nao wengi wakamwamini huko. Yohana 10:42

Many believed in him there.