Yohana 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
Yohana 19 (Swahili) John 19 (English)

Basi ndipo Pilato alipomtwaa Yesu, akampiga mijeledi. Yohana 19:1

So Pilate then took Jesus, and flogged him.

Nao askari wakasokota taji ya miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau. Yohana 19:2

The soldiers twisted thorns into a crown, and put it on his head, and dressed him in a purple garment.

Wakawa wakimwendea, wakisema, Salamu! Mfalme wa Wayahudi! Wakampiga makofi. Yohana 19:3

They kept saying, "Hail, King of the Jews!" and they kept slapping him.

Kisha Pilato akatokea tena nje, akawaambia, Mtu huyu namleta nje kwenu, mpate kufahamu ya kuwa mimi sioni hatia yo yote kwake. Yohana 19:4

Then Pilate went out again, and said to them, "Behold, I bring him out to you, that you may know that I find no basis for a charge against him."

Ndipo Yesu alipotoka nje, naye amevaa ile taji ya miiba, na lile vazi la zambarau. Pilato akawaambia, Tazama, mtu huyu! Yohana 19:5

Jesus therefore came out, wearing the crown of thorns and the purple garment. Pilate said to them, "Behold, the man!"

Basi wale wakuu wa makuhani na watumishi wao walipomwona, walipiga kelele wakisema, Msulibishe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Mtwaeni ninyi basi, mkamsulibishe; kwa maana mimi sioni hatia kwake. Yohana 19:6

When therefore the chief priests and the officers saw him, they shouted, saying, "Crucify! Crucify!" Pilate said to them, "Take him yourselves, and crucify him, for I find no basis for a charge against him."

Wayahudi wakamjibu, Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo amestahili kufa, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu. Yohana 19:7

The Jews answered him, "We have a law, and by our law he ought to die, because he made himself the Son of God."

Basi Pilato aliposikia neno hilo, akazidi kuogopa. Yohana 19:8

When therefore Pilate heard this saying, he was more afraid.

Akaingia tena ndani ya ile Praitorio, akamwambia Yesu, Wewe umetokapi? Lakini Yesu hakumpa jibu lo lote. Yohana 19:9

He entered into the Praetorium again, and said to Jesus, "Where are you from?" But Jesus gave him no answer.

Basi Pilato akamwambia, Husemi nami? Hujui ya kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua, nami nina mamlaka ya kukusulibisha? Yohana 19:10

Pilate therefore said to him, "Aren't you speaking to me? Don't you know that I have power to release you, and have power to crucify you?"

Yesu akamjibu, Wewe hungekuwa na mamlaka yo yote juu yangu, kama usingepewa kutoka juu; kwa hiyo yeye aliyenitia mikononi mwako yuna dhambi iliyo kubwa zaidi. Yohana 19:11

Jesus answered, "You would have no power at all against me, unless it were given to you from above. Therefore he who delivered me to you has greater sin."

Na tangu hapo Pilato akatafuta kumfungua; lakini Wayahudi wakapiga makelele wakisema, Ukimfungua huyu, wewe si rafiki yake Kaisari; kila mtu ajifanyaye kuwa mfalme humfitini Kaisari. Yohana 19:12

At this, Pilate was seeking to release him, but the Jews cried out, saying, "If you release this man, you aren't Caesar's friend! Everyone who makes himself a king speaks against Caesar!"

Basi Pilato, aliposikia maneno hayo, akamleta Yesu nje, akaketi juu ya kiti cha hukumu, mahali paitwapo Sakafu ya Mawe, au kwa Kiebrania, Gabatha. Yohana 19:13

When Pilate therefore heard these words, he brought Jesus out, and sat down on the judgment seat at a place called "The Pavement," but in Hebrew, "Gabbatha."

Nayo ilikuwa Maandalio ya pasaka, yapata saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, Mfalme wenu! Yohana 19:14

Now it was the Preparation Day of the Passover, at about the sixth hour.{noon} He said to the Jews, "Behold, your King!"

Basi wale wakapiga kelele, Mwondoshe! Mwondoshe! Msulibishe! Pilato akawaambia, Je! Nimsulibishe mfalme wenu! Wakuu wa makuhani wakamjibu, Sisi hatuna mfalme ila Kaisari. Yohana 19:15

They cried out, "Away with him! Away with him! Crucify him!" Pilate said to them, "Shall I crucify your King?" The chief priests answered, "We have no king but Caesar!"

Basi ndipo alipomtia mikononi mwao ili asulibiwe; nao wakampokea Yesu. Yohana 19:16

So then he delivered him to them to be crucified. So they took Jesus and led him away.

Akatoka, hali akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha. Yohana 19:17

He went out, bearing his cross, to the place called "The Place of a Skull," which is called in Hebrew, "Golgotha,"

Wakamsulibisha huko, na wengine wawili pamoja naye, mmoja huku na mmoja huku, na Yesu katikati. Yohana 19:18

where they crucified him, and with him two others, on either side one, and Jesus in the middle.

Naye Pilato akaandika anwani, akaiweka juu ya msalaba, imeandikwa, YESU MNAZARETI, MFALME WA WAYAHUDI. Yohana 19:19

Pilate wrote a title also, and put it on the cross. There was written, "JESUS OF NAZARETH, THE KING OF THE JEWS."

Basi anwani hiyo waliisoma wengi katika Wayahudi; maana mahali pale aliposulibiwa Yesu palikuwa karibu na mji; nayo iliandikwa kwa Kiebrania, na Kirumi, na Kiyunani. Yohana 19:20

Therefore many of the Jews read this title, for the place where Jesus was crucified was near the city; and it was written in Hebrew, in Latin, and in Greek.

Basi wakuu wa makuhani na Wayahudi wakamwambia Pilato, Usiandike, Mfalme wa Wayahudi; bali ya kwamba yule alisema, Mimi ni mfalme wa Wayahudi. Yohana 19:21

The chief priests of the Jews therefore said to Pilate, "Don't write, 'The King of the Jews,' but, 'he said, I am King of the Jews.'"

Pilato akajibu, Niliyoandika nimeyaandika. Yohana 19:22

Pilate answered, "What I have written, I have written."

Nao askari walipomsulibisha Yesu, waliyatwaa mavazi yake, wakafanya mafungu manne, kwa kila askari fungu lake; na kanzu nayo. Basi kanzu ile haikushonwa, ilikuwa imefumwa yote pia tangu juu. Yohana 19:23

Then the soldiers, when they had crucified Jesus, took his garments and made four parts, to every soldier a part; and also the coat. Now the coat was without seam, woven from the top throughout.

Basi wakaambiana, Tusiipasue, lakini tuipigie kura, iwe ya nani. Ili litimie andiko lile linenalo, Waligawanya nguo zangu, Na vazi langu wakalipigia kura. Basi ndivyo walivyofanya wale askari. Yohana 19:24

Then they said to one another, "Let's not tear it, but cast lots for it to decide whose it will be," that the Scripture might be fulfilled, which says, "They parted my garments among them. For my cloak they cast lots." Therefore the soldiers did these things.

Na penye msalaba wake Yesu walikuwa wamesimama mamaye, na umbu la mamaye, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene. Yohana 19:25

But there were standing by the cross of Jesus his mother, and his mother's sister, Mary the wife of Clopas, and Mary Magdalene.

Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. Yohana 19:26

Therefore when Jesus saw his mother, and the disciple whom he loved standing there, he said to his mother, "Woman, behold your son!"

Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake. Yohana 19:27

Then he said to the disciple, "Behold, your mother!" From that hour, the disciple took her to his own home.

Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu. Yohana 19:28

After this, Jesus, seeing{NU, TR read "knowing" instead of "seeing"} that all things were now finished, that the Scripture might be fulfilled, said, "I am thirsty."

Kulikuwako huko chombo kimejaa siki; basi wakatia sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakampelekea kinywani. Yohana 19:29

Now a vessel full of vinegar was set there; so they put a sponge full of the vinegar on hyssop, and held it at his mouth.

Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake. Yohana 19:30

When Jesus therefore had received the vinegar, he said, "It is finished." He bowed his head, and gave up his spirit.

Basi Wayahudi, kwa sababu ni Maandalio, miili isikae juu ya misalaba siku ya sabato, (maana sabato ile ilikuwa siku kubwa), walimwomba Pilato miguu yao ivunjwe, wakaondolewe. Yohana 19:31

Therefore the Jews, because it was the Preparation Day, so that the bodies wouldn't remain on the cross on the Sabbath (for that Sabbath was a special one), asked of Pilate that their legs might be broken, and that they might be taken away.

Basi askari wakaenda, wakamvunja miguu wa kwanza, na wa pili, aliyesulibiwa pamoja naye. Yohana 19:32

Therefore the soldiers came, and broke the legs of the first, and of the other who was crucified with him;

Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; Yohana 19:33

but when they came to Jesus, and saw that he was already dead, they didn't break his legs.

lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji. Yohana 19:34

However one of the soldiers pierced his side with a spear, and immediately blood and water came out.

Naye aliyeona ameshuhudia, na ushuhuda wake ni kweli; naye anajua ya kuwa anasema kweli ili ninyi nanyi mpate kusadiki. Yohana 19:35

He who has seen has testified, and his testimony is true. He knows that he tells the truth, that you may believe.

Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa. Yohana 19:36

For these things happened, that the Scripture might be fulfilled, "A bone of him will not be broken."

Na tena andiko lingine lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma. Yohana 19:37

Again another Scripture says, "They will look on him whom they pierced."

Hata baada ya hayo Yusufu wa Arimathaya, naye ni mwanafunzi wa Yesu, (lakini kwa siri, kwa hofu ya Wayahudi), alimwomba Pilato ruhusa ili auondoe mwili wake Yesu. Na Pilato akampa ruhusa. Basi akaenda, akauondoa mwili wake. Yohana 19:38

After these things, Joseph of Arimathaea, being a disciple of Jesus, but secretly for fear of the Jews, asked of Pilate that he might take away Jesus' body. Pilate gave him permission. He came therefore and took away his body.

Akaenda Nikodemo naye, (yule aliyemwendea usiku hapo kwanza), akaleta machanganyiko ya manemane na uudi, yapata ratli mia. Yohana 19:39

Nicodemus, who at first came to Jesus by night, also came bringing a mixture of myrrh and aloes, about a hundred pounds.{100 Roman pounds of 12 ounces each, or about 72 pounds, or 33 Kilograms.}

Basi wakautwaa mwili wake Yesu, wakaufunga sanda ya kitani pamoja na yale manukato, kama ilivyo desturi ya Wayahudi katika kuzika. Yohana 19:40

So they took Jesus' body, and bound it in linen cloths with the spices, as the custom of the Jews is to bury.

Na pale pale aliposulibiwa palikuwa na bustani; na ndani ya bustani mna kaburi jipya, ambalo hajatiwa bado mtu ye yote ndani yake. Yohana 19:41

Now in the place where he was crucified there was a garden. In the garden a new tomb in which no man had ever yet been laid.

Humo basi, kwa sababu ya Maandalio ya Wayahudi, wakamweka Yesu; maana lile kaburi lilikuwa karibu.

Yohana 19:42

Then because of the Jews' Preparation Day (for the tomb was near at hand) they laid Jesus there.