2 Samweli 20 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 20 (Swahili) 2nd Samuel 20 (English)

Basi ilitukia ya kwamba kulikuwapo mtu asiyefaa, jina lake akiitwa Sheba, mwana wa Bikri, Mbenyamini; naye akapiga tarumbeta, akasema, Sisi hatuna sehemu katika Daudi, wala hatuna urithi katika mwana wa Yese; nendeni kila mtu hemani kwake, enyi Israeli. 2 Samweli 20:1

There happened to be there a base fellow, whose name was Sheba, the son of Bichri, a Benjamite: and he blew the trumpet, and said, We have no portion in David, neither have we inheritance in the son of Jesse: every man to his tents, Israel.

Basi wakapanda watu wote wa Israeli kutoka kumfuata Daudi, wakamfuata Sheba, mwana wa Bikri; lakini watu wa Yuda wakaambatana na mfalme wao, toka Yordani hata kufika Yerusalemu. 2 Samweli 20:2

So all the men of Israel went up from following David, and followed Sheba the son of Bichri; but the men of Judah joined with their king, from the Jordan even to Jerusalem.

Basi Daudi akaja Yerusalemu nyumbani kwake; kisha mfalme akawatwaa wale wanawake kumi, masuria, aliowaacha kuitunza nyumba, akawatia nyumbani mwa kulindwa, akawalisha, ila asiingie kwao. Basi wakafungwa hata siku ya kufa kwao, huku wakiishi hali ya ujane. 2 Samweli 20:3

David came to his house at Jerusalem; and the king took the ten women his concubines, whom he had left to keep the house, and put them in custody, and provided them with sustenance, but didn't go in to them. So they were shut up to the day of their death, living in widowhood.

Ndipo mfalme akamwambia Amasa, Uwakusanye pamoja kwangu kwa siku tatu watu wa Yuda, na uwepo wewe hapa. 2 Samweli 20:4

Then said the king to Amasa, Call me the men of Judah together within three days, and be here present.

Amasa akaenda kuwakusanya Yuda; lakini akakawia zaidi ya huo muda aliowekewa. 2 Samweli 20:5

So Amasa went to call [the men of] Judah together; but he stayed longer than the set time which he had appointed him.

Basi Daudi akamwambia Abishai, Sasa Sheba, mwana wa Bikri, atatudhuru, kuliko Absalomu; twaa wewe watumishi wa bwana wako, ukamfuatie, asiingie katika miji yenye boma, na kujiponya machoni petu. 2 Samweli 20:6

David said to Abishai, Now will Sheba the son of Bichri do us more harm than did Absalom: take your lord's servants, and pursue after him, lest he get him fortified cities, and escape out of our sight.

Ndipo wakatoka nyuma yake watu wa Yoabu, na Wakerethi na Wapelethi, na mashujaa wote; wakatoka Yerusalemu, ili kumfuatia Sheba, mwana wa Bikri. 2 Samweli 20:7

There went out after him Joab's men, and the Cherethites and the Pelethites, and all the mighty men; and they went out of Jerusalem, to pursue after Sheba the son of Bichri.

Basi walipokuwako kwenye lile jiwe kubwa lililoko Gibeoni, Amasa akaja kuwalaki. Naye Yoabu alikuwa amefungwa mavazi yake ya vita aliyoyavaa, na juu yake alikuwa na mshipi, na upanga uliotiwa viunoni mwake ndani ya ala yake; naye alipokuwa akiendelea, ukaanguka. 2 Samweli 20:8

When they were at the great stone which is in Gibeon, Amasa came to meet them. Joab was girded with his apparel of war that he had put on, and thereon was a sash with a sword fastened on his loins in the sheath of it; and as he went forth it fell out.

Naye Yoabu akamwambia Amasa, Amani kwako, ndugu yangu. Kisha Yoabu akamshika Amasa ndevu kwa mkono wake wa kuume ili ambusu. 2 Samweli 20:9

Joab said to Amasa, Is it well with you, my brother? Joab took Amasa by the beard with his right hand to kiss him.

Wala Amasa hakuangalia huo upanga uliomo mkononi mwa Yoabu; basi akampiga nao wa tumbo, akamwaga matumbo yake chini, asimpige mara ya pili; naye akafa. Kisha Yoabu na Abishai, nduguye, wakamfuata Sheba, mwana wa Bikri. 2 Samweli 20:10

But Amasa took no heed to the sword that was in Joab's hand: so he struck him therewith in the body, and shed out his bowels to the ground, and didn't strike him again; and he died. Joab and Abishai his brother pursued after Sheba the son of Bichri.

Akasimama karibu naye mmojawapo wa vijana wa Yoabu, huyo akasema, Ampendaye Yoabu, na aliye wa Daudi, na amfuate Yoabu. 2 Samweli 20:11

There stood by him one of Joab's young men, and said, He who favors Joab, and he who is for David, let him follow Joab.

Lakini Amasa alikuwa anagaagaa katika damu yake katikati ya njia kuu. Basi yule mtu alipowaona watu wote wamesimama, akamwondoa Amasa toka njia kuu akamtia kondeni, akamfunika nguo, hapo alipoona ya kuwa kila mtu aliyefika kwake amesimama. 2 Samweli 20:12

Amasa lay wallowing in his blood in the midst of the highway. When the man saw that all the people stood still, he carried Amasa out of the highway into the field, and cast a garment over him, when he saw that everyone who came by him stood still.

Na alipoondolewa katika njia kuu, watu wote wakapita, wakamwandama Yoabu ili kumfuatia Sheba, mwana wa Bikri. 2 Samweli 20:13

When he was removed out of the highway, all the people went on after Joab, to pursue after Sheba the son of Bichri.

Naye akapita kati ya kabila zote za Israeli mpaka Abeli, na kwa Bethmaaka na Wabikri wote; nao wakakusanyika, wakaenda pia kumwandama. 2 Samweli 20:14

He went through all the tribes of Israel to Abel, and to Beth Maacah, and all the Berites: and they were gathered together, and went also after him.

Na hao wakaja wakamhusuru katika Abeli wa Bethmaaka, wakafanya chuguu mbele ya mji, nayo ikasimama kuielekea ngome; na watu wote waliokuwa pamoja na Yoabu wakavunja-vunja ukuta, wapate kuubomoa. 2 Samweli 20:15

They came and besieged him in Abel of Beth Maacah, and they cast up a mound against the city, and it stood against the rampart; and all the people who were with Joab battered the wall, to throw it down.

Ndipo akalia mwanamke mmoja mwenye akili toka mjini, Sikieni, sikieni; mwambieni na Yoabu, aje hapa karibu, niseme naye. 2 Samweli 20:16

Then cried a wise woman out of the city, "Hear, hear! Please say to Joab, 'Come near here, that I may speak with you.'"

Basi akamkaribia; na yule mwanamke akasema, Ndiwe Yoabu? Akajibu, Ndimi. Ndipo akamwambia Sikia maneno ya mjakazi wako. Akajibu, Mimi nasikia. 2 Samweli 20:17

He came near to her; and the woman said, Are you Joab? He answered, I am. Then she said to him, Hear the words of your handmaid. He answered, I do hear.

Kisha akanena, akisema, Watu hunena zamani za kale, wakisema, Wasikose kuuliza huko Abeli; ndivyo walivyomaliza shauri. 2 Samweli 20:18

Then she spoke, saying, They were wont to speak in old time, saying, They shall surely ask [counsel] at Abel: and so they ended [the matter].

Mimi ni wa hao wenye amani, walio waaminifu katika Israeli; wewe unatafuta kuuharibu mji, na mama wa Israeli; mbona wataka kuumeza urithi wa Bwana? 2 Samweli 20:19

I am of those who are peaceable and faithful in Israel: you seek to destroy a city and a mother in Israel: why will you swallow up the inheritance of Yahweh?

Yoabu akajibu, akasema, Isiwe, isiwe kwangu, niumeze wala kuuharibu. 2 Samweli 20:20

Joab answered, Far be it, far be it from me, that I should swallow up or destroy.

Neno hili silo hivyo; lakini mtu mmoja wa milima ya Efraimu, Sheba, mwana wa Bikri, jina lake, ameinua mkono wake juu ya mfalme, naam, Daudi, basi mtoeni yeye tu, nami nitaondoka katika mji huu. Basi yule mwanamke akamwambia Yoabu, Tazama, kichwa chake utatupiwa juu ya ukuta. 2 Samweli 20:21

The matter is not so: but a man of the hill-country of Ephraim, Sheba the son of Bichri by name, has lifted up his hand against the king, even against David; deliver him only, and I will depart from the city. The woman said to Joab, Behold, his head shall be thrown to you over the wall.

Ndipo yule mwanamke akawaendea watu wote katika akili zake. Nao wakamkata kichwa Sheba, mwana wa Bikri, wakamtupia Yoabu huko nje. Ndipo akapiga tarumbeta, nao wakatawanyika kutoka mjini kila mtu hemani kwake. Naye Yoabu akarudi mpaka Yerusalemu kwa mfalme. 2 Samweli 20:22

Then the woman went to all the people in her wisdom. They cut off the head of Sheba the son of Bichri, and threw it out to Joab. He blew the trumpet, and they were dispersed from the city, every man to his tent. Joab returned to Jerusalem to the king.

Basi Yoabu alikuwa juu ya jeshi lote la Israeli; na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa juu ya Wakerethi, na juu ya Wapelethi; 2 Samweli 20:23

Now Joab was over all the host of Israel; and Benaiah the son of Jehoiada was over the Cherethites and over the Pelethites;

na Adoramu alikuwa juu ya shokoa; na Yehoshafati, mwana wa Ahiludi, alikuwa mkumbushi; 2 Samweli 20:24

and Adoram was over the men subject to forced labor; and Jehoshaphat the son of Ahilud was the recorder;

na Shausha mwandishi; na Sadoki na Abiathari walikuwa makuhani. 2 Samweli 20:25

and Sheva was scribe; and Zadok and Abiathar were priests;

Tena na Ira, Myairi, alikuwa kuhani kwa Daudi. 2 Samweli 20:26

and also Ira the Jairite was chief minister to David.