2 Samweli 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 10 (Swahili) 2nd Samuel 10 (English)

Ikawa baadaye, mfalme wa wana wa Amori akafa, akamiliki Hanuni, mwanawe, mahali pake. 2 Samweli 10:1

It happened after this, that the king of the children of Ammon died, and Hanun his son reigned in his place.

Naye Daudi akasema, Nitamtendea wema Hanuni, mwana wa Nahasi, kama babaye alivyonitendea wema mimi. Basi Daudi akatuma kwa mkono wa watumishi wake, ili kumtuliza kwa habari za babaye. Wakaja watumishi wa Daudi katika nchi ya wana wa Amoni. 2 Samweli 10:2

David said, I will show kindness to Hanun the son of Nahash, as his father shown kindness to me. So David sent by his servants to comfort him concerning his father. David's servants came into the land of the children of Ammon.

Lakini wakuu wa wana wa Amoni wakamwambia Hanuni, bwana wao, Je! Waona ya kuwa Daudi amemheshimu babayo kwa kutuma kwako wafariji? Je! Daudi hakuwapeleka watumishi wake kwako ili kuuangalia mji, na kuupeleleza, na kuuangamiza? 2 Samweli 10:3

But the princes of the children of Ammon said to Hanun their lord, Do you think that David honors your father, in that he has sent comforters to you? Hasn't David sent his servants to you to search the city, and to spy it out, and to overthrow it?

Basi Hanuni akawatwaa hao watumishi wa Daudi, akawanyoa nusu ya ndevu zao, akawakatia nguo zao katikati, hata matakoni, akawatoa waende zao. 2 Samweli 10:4

So Hanun took David's servants, and shaved off the one half of their beards, and cut off their garments in the middle, even to their buttocks, and sent them away.

Watu walipomwambia Daudi habari hizo, akatuma watu kuwalaki; kwa sababu watu hao walikuwa wametahayarika sana. Mfalme akasema, Ngojeni Yeriko, hata mtakapoota ndevu zenu, ndipo mrudi. 2 Samweli 10:5

When they told it to David, he sent to meet them; for the men were greatly ashamed. The king said, Wait at Jericho until your beards be grown, and then return.

Na wana wa Amoni walipoona ya kuwa wamekuwa machukizo kwa Daudi, wana wa Amoni wakatuma na kuwaajiri Washami wa Bethrehobu, na Washami wa Soba, askari ishirini elfu, na mfalme wa Maaka mwenye watu elfu, na watu wa Tobu watu kumi na mbili elfu. 2 Samweli 10:6

When the children of Ammon saw that they were become odious to David, the children of Ammon sent and hired the Syrians of Beth Rehob, and the Syrians of Zobah, twenty thousand footmen, and the king of Maacah with one thousand men, and the men of Tob twelve thousand men.

Naye Daudi aliposikia akamtuma Yoabu, na jeshi lote la mashujaa. 2 Samweli 10:7

When David heard of it, he sent Joab, and all the host of the mighty men.

Wana wa Amoni wakatoka, wakapanga vita mahali pa kuingilia lango; na Washami wa Soba, na wa Rehobu, na watu wa Tobu, na wa Maaka, walikuwa peke yao uwandani. 2 Samweli 10:8

The children of Ammon came out, and put the battle in array at the entrance of the gate: and the Syrians of Zobah and of Rehob, and the men of Tob and Maacah, were by themselves in the field.

Basi Yoabu alipoona ya kwamba uso wa vita umekuwa juu yake mbele na nyuma, akachagua baadhi ya wateule wote wa Israeli, akawapanga juu ya Washami; 2 Samweli 10:9

Now when Joab saw that the battle was set against him before and behind, he chose of all the choice men of Israel, and put them in array against the Syrians:

akawatia nguvu watu waliosalia mkononi mwa Abishai, nduguye, akawapanga juu ya wana wa Amoni. 2 Samweli 10:10

The rest of the people he committed into the hand of Abishai his brother; and he put them in array against the children of Ammon.

Akasema, Wakiwa Washami hodari mno kwangu, ndipo wewe utanisaidia, lakini wana wa Amoni wakiwa ni hodari mno kwako, ndipo mimi nitakuja nikusaidie wewe. 2 Samweli 10:11

He said, If the Syrians be too strong for me, then you shall help me; but if the children of Ammon be too strong for you, then I will come and help you.

Uwe hodari, tukajitie moyo mkuu, kwa ajili ya watu wetu, na kwa ajili ya miji ya Mungu wetu; naye Bwana afanye yaliyo mema machoni pake. 2 Samweli 10:12

Be of good courage, and let us play the man for our people, and for the cities of our God: and Yahweh do that which seems him good.

Basi Yoabu na watu waliokuwa pamoja naye wakakaribia kupigana na Washami; nao wakakimbia mbele yake. 2 Samweli 10:13

So Joab and the people who were with him drew near to the battle against the Syrians: and they fled before him.

Na wana wa Amoni walipoona ya kwamba Washami wamekimbia, wakakimbia nao mbele ya Abishai, wakaingia mjini. Ndipo Yoabu akarudi kutoka kwa wana wa Amoni, akaja Yerusalemu. 2 Samweli 10:14

When the children of Ammon saw that the Syrians were fled, they likewise fled before Abishai, and entered into the city. Then Joab returned from the children of Ammon, and came to Jerusalem.

Na Washami walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, wakakusanyika. 2 Samweli 10:15

When the Syrians saw that they were put to the worse before Israel, they gathered themselves together.

Naye Hadadezeri akatuma na kuwaleta Washami waliokuwako ng'ambo ya Mto; nao wakaja Helamu, naye Shobaki, jemadari wa jeshi la Hadadezeri, akawaongoza. 2 Samweli 10:16

Hadarezer sent, and brought out the Syrians who were beyond the River: and they came to Helam, with Shobach the captain of the host of Hadarezer at their head.

Alipoambiwa Daudi, akakusanya Israeli wote, akavuka Yordani, akaja Helamu. Nao Washami wakajipanga kinyume cha Daudi, wakapigana naye. 2 Samweli 10:17

It was told David; and he gathered all Israel together, and passed over the Jordan, and came to Helam. The Syrians set themselves in array against David, and fought with him.

Wakakimbia Washami mbele ya Israeli; naye Daudi akawaua katika Washami, watu wa magari mia saba, na wapanda farasi arobaini elfu, naye akampiga huyo Shobaki, jemadari wa jeshi lao, hata akafa huko. 2 Samweli 10:18

The Syrians fled before Israel; and David killed of the Syrians [the men of] seven hundred chariots, and forty thousand horsemen, and struck Shobach the captain of their host, so that he died there.

Na wafalme wote waliomtumikia Hadadezeri walipojiona kuwa wameshindwa mbele ya Israeli, walifanya amani na Israeli, wakawatumikia. Basi Washami wakaogopa kuwasaidia wana wa Amoni tena.

2 Samweli 10:19

When all the kings who were servants to Hadarezer saw that they were put to the worse before Israel, they made peace with Israel, and served them. So the Syrians feared to help the children of Ammon any more.