2 Samweli 14 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 14 (Swahili) 2nd Samuel 14 (English)

Basi Yoabu, mwana wa Seruya, akatambua ya kuwa moyo wa mfalme unamwelekea Absalomu. 2 Samweli 14:1

Now Joab the son of Zeruiah perceived that the king's heart was toward Absalom.

Yoabu akatuma watu waende Tekoa, akaleta kutoka huko mwanamke mwenye akili, akamwambia, Nakusihi, ujifanye kama unakaa matanga, ukavae nguo za kufiwa, nakusihi, wala usijitie mafuta, ila ukafanane na mwanamke aliyeomboleza siku nyingi kwa ajili yake aliyefariki; 2 Samweli 14:2

Joab sent to Tekoa, and fetched there a wise woman, and said to her, please act like a mourner, and put on mourning clothing, Please, and don't anoint yourself with oil, but be as a woman who has a long time mourned for the dead:

kisha uingie kwa mfalme ukamwambie maneno haya. Hivyo Yoabu akamtia maneno kinywani. 2 Samweli 14:3

and go in to the king, and speak on this manner to him. So Joab put the words in her mouth.

Naye yule mwanamke wa Tekoa aliponena na mfalme, akaanguka kifulifuli chini, akamsujudia, akasema, Nisaidie, Ee mfalme. 2 Samweli 14:4

When the woman of Tekoa spoke to the king, she fell on her face to the ground, and did obeisance, and said, Help, O king.

Mfalme akamwuliza, Una nini? Naye akajibu, Hakika ni mjane mimi, niliyefiwa na mume wangu. 2 Samweli 14:5

The king said to her, What ails you? She answered, Of a truth I am a widow, and my husband is dead.

Nami mjakazi wako nalikuwa na wana wawili, na hao wawili wakashindana uwandani, wala hapakuwa na mtu wa kuwaamua, lakini mmoja akampiga mwenzake, akamwua. 2 Samweli 14:6

Your handmaid had two sons, and they two strove together in the field, and there was none to part them, but the one struck the other, and killed him.

Na tazama, jamaa yote wameniinukia mimi mjakazi wako, wakasema, Mtoe yule aliyempiga nduguye, ili tupate kumwua yeye kwa maisha ya nduguye aliyemwua, hata na kumfisha mrithi pia; ndivyo watakavyolizima kaa langu lililobaki, wasimwachie mume wangu jina wala masalio usoni pa nchi. 2 Samweli 14:7

Behold, the whole family is risen against your handmaid, and they say, Deliver him who struck his brother, that we may kill him for the life of his brother whom he killed, and so destroy the heir also. Thus will they quench my coal which is left, and will leave to my husband neither name nor remainder on the surface of the earth.

Mfalme akamwambia huyo mwanamke, Nenda nyumbani kwako, nami nitakufanyia agizo. 2 Samweli 14:8

The king said to the woman, Go to your house, and I will give charge concerning you.

Ndipo huyo mwanamke wa Tekoa akamwambia mfalme, Na uwe juu yangu, Ee bwana wangu mfalme, na juu ya nyumba ya baba yangu uovu huu; wala kwa mfalme na kwa kiti chake cha enzi pasiwepo hatia. 2 Samweli 14:9

The woman of Tekoa said to the king, My lord, O king, the iniquity be on me, and on my father's house; and the king and his throne be guiltless.

Mfalme akasema, Ye yote atakaye kuambia neno, mlete kwangu, naye hatakugusa tena. 2 Samweli 14:10

The king said, Whoever says anything to you, bring him to me, and he shall not touch you any more.

Ndipo akajibu, Nakusihi, mfalme na amkumbuke Bwana, Mungu wako, ili mlipiza kisasi cha damu asizidi kuharibu, wasije kumharibu mwanangu. Naye akasema, Aishivyo Bwana, hautaanguka chini hata unywele mmoja wa mwanao. 2 Samweli 14:11

Then said she, Please let the king remember Yahweh your God, that the avenger of blood destroy not any more, lest they destroy my son. He said, As Yahweh lives, there shall not one hair of your son fall to the earth.

Mwanamke akasema, Mwache mjakazi wako, nakusihi, niseme neno moja kwa bwana wangu mfalme. Akasema, Haya nena. 2 Samweli 14:12

Then the woman said, Please let your handmaid speak a word to my lord the king. He said, Say on.

Mwanamke akasema, Kwa nini basi wewe umewafikiria mambo kama hayo watu wa Mungu? Kwani kwa kunena neno hili mfalme ni kama mwenye hatia, kwa kuwa mfalme hamleti kwao tena yule mfukuzwa wake. 2 Samweli 14:13

The woman said, Why then have you devised such a thing against the people of God? for in speaking this word the king is as one who is guilty, in that the king does not bring home again his banished one.

Kwa kuwa hatuna budi kufa, nasi tu kama maji yaliyomwagika chini, yasiyowezekana kuzoleka tena; wala Mungu haondoi maisha ila hufikiri shauri, kwamba yeye aliyefukuzwa asiwe mkimbizi kwake. 2 Samweli 14:14

For we must needs die, and are as water split on the ground, which can't be gathered up again; neither does God take away life, but devises means, that he who is banished not be an outcast from him.

Hata sasa nilivyokuja mimi kunena neno hili na bwana wangu mfalme, ni kwa sababu watu wamenitisha; nami, mjakazi wako, nikasema, Mimi nitanena sasa kwa mfalme; labda itakuwa mfalme atanifanyia haja yangu mimi mtumwa wake. 2 Samweli 14:15

Now therefore seeing that I have come to speak this word to my lord the king, it is because the people have made me afraid: and your handmaid said, I will now speak to the king; it may be that the king will perform the request of his servant.

Kwa kuwa mfalme atasikia, ili amwokoe mtumwa wake mkononi mwa yule mtu atakaye kuniharibu mimi na mwanangu pia katika urithi wa Mungu. 2 Samweli 14:16

For the king will hear, to deliver his servant out of the hand of the man who would destroy me and my son together out of the inheritance of God.

Ndipo mimi mjakazi wako nikasema, Neno la bwana wangu mfalme na liwe la kustarehesha; kwa kuwa kama malaika wa Mungu ndivyo alivyo bwana wangu mfalme, kuyapambanua yaliyo mema na yaliyo mabaya; naye Bwana, Mungu wako na awe pamoja nawe. 2 Samweli 14:17

Then your handmaid said, Please let the word of my lord the king be comfortable; for as an angel of God, so is my lord the king to discern good and bad: and Yahweh your God be with you.

Ndipo mfalme akajibu, akamwambia yule mwanamke, usinifiche, nakusihi, neno lo lote nitakalokuuliza. Na mwanamke akasema, Na anene sasa bwana wangu mfalme. 2 Samweli 14:18

Then the king answered the woman, Please don't hide anything from me that I shall ask you. The woman said, Let my lord the king now speak.

Mfalme akasema, Je! Si mkono wa Yoabu ulio pamoja nawe katika haya yote? Mwanamke akajibu, akasema, Kama iishivyo roho yako, bwana wangu, mfalme, hapana mtu awezaye kugeuka kwa kuume, au kwa kushoto, kukana neno lo lote alilolisema bwana wangu mfalme; kwani mtumwa wako Yoabu ndiye aliyeniamuru, na kuyaweka maneno haya yote kinywani mwa mjakazi wako; 2 Samweli 14:19

The king said, Is the hand of Joab with you in all this? The woman answered, As your soul lives, my lord the king, none can turn to the right hand or to the left from anything that my lord the king has spoken; for your servant Joab, he bade me, and he put all these words in the mouth of your handmaid;

mtumwa wako Yoabu ameyatenda haya ili kubadili uso wa jambo hili; na bwana wangu anayo akili, kama akili ya malaika wa Mungu, hata ajue mambo yote ya duniani. 2 Samweli 14:20

to change the face of the matter has your servant Joab done this thing: and my lord is wise, according to the wisdom of an angel of God, to know all things that are in the earth.

Basi mfalme akamwambia Yoabu, Angalia sasa, nimekata shauri hili; nenda, ukamrudishe tena yule kijana Absalomu. 2 Samweli 14:21

The king said to Joab, Behold now, I have done this thing: go therefore, bring the young man Absalom back.

Naye Yoabu akaanguka kifulifuli hata nchi, akasujudu, akambariki mfalme, Yoabu akasema, Leo mimi mtumwa wako najua ya kwamba nimepata neema machoni pako, bwana wangu mfalme, kwa kuwa mfalme amemfanyia mtumwa wake haja yake. 2 Samweli 14:22

Joab fell to the ground on his face, and did obeisance, and blessed the king: and Joab said, Today your servant knows that I have found favor in your sight, my lord, king, in that the king has performed the request of his servant.

Basi Yoabu akaondoka, akaenda Geshuri, akamleta Absalomu Yerusalemu. 2 Samweli 14:23

So Joab arose and went to Geshur, and brought Absalom to Jerusalem.

Naye mfalme akasema, Ageukie nyumbani kwake, asinione uso wangu. Basi Absalomu akarejea nyumbani kwake, asimwone uso mfalme. 2 Samweli 14:24

The king said, Let him turn to his own house, but let him not see my face. So Absalom turned to his own house, and didn't see the king's face.

Basi katika Israeli wote hapakuwa na mtu hata mmoja mwenye kusifiwa kwa uzuri wake kama huyo Absalomu; tangu nyayo za miguu yake hata utosi wa kichwa chake hapakuwa na ila kwake. 2 Samweli 14:25

Now in all Israel there was none to be so much praised as Absalom for his beauty: from the sole of his foot even to the crown of his head there was no blemish in him.

Naye aliponyoa kichwa, (basi mwisho wa kila mwaka hunyoa; na kwa sababu nywele zilikuwa nzito kwake, kwa hiyo akanyoa;) hupima nywele za kichwa chake shekeli mia mbili kwa uzani wa mfalme. 2 Samweli 14:26

When he cut the hair of his head (now it was at every year's end that he cut it; because it was heavy on him, therefore he cut it); he weighed the hair of his head at two hundred shekels, after the king's weight.

Kisha wakazaliwa kwake Absalomu wana watatu na binti mmoja, ambaye jina lake aliitwa Tamari; naye alikuwa mwanamke mzuri wa uso. 2 Samweli 14:27

To Absalom there were born three sons, and one daughter, whose name was Tamar: she was a woman of a beautiful face.

Absalomu akakaa miaka miwili mizima katika Yerusalemu; asimwone uso mfalme. 2 Samweli 14:28

Absalom lived two full years in Jerusalem; and he didn't see the king's face.

Ndipo Absalomu akatuma kumwita Yoabu, ampeleke kwa mfalme, lakini yeye akakataa kumjia; akatuma tena mara ya pili, lakini akakataa kuja. 2 Samweli 14:29

Then Absalom sent for Joab, to send him to the king; but he would not come to him: and he sent again a second time, but he would not come.

Kwa hiyo akawaambia watumishi wake, Tazameni, shamba la Yoabu liko karibu na shamba langu, naye ana shayiri huko; nendeni mkalitie moto. Basi watumishi wa Absalomu wakalitia moto lile shamba. 2 Samweli 14:30

Therefore he said to his servants, Behold, Joab's field is near mine, and he has barley there; go and set it on fire. Absalom's servants set the field on fire.

Ndipo akaondoka Yoabu, akamwendea Absalomu nyumbani kwake, akamwambia, Kwa nini watumishi wako wamelitia moto shamba langu? 2 Samweli 14:31

Then Joab arose, and came to Absalom to his house, and said to him, Why have your servants set my field on fire?

Absalomu akamjibu Yoabu, Angalia, nilituma kwako, kusema, Njoo kwangu, ili nikupeleke kwa mfalme kunena, Mbona nimekuja kutoka Geshuri? Ingekuwa heri kwangu kama ningekuwako huko hata sasa; basi sasa na nimtazame uso mfalme; na ukiwapo uovu kwangu, na aniue. 2 Samweli 14:32

Absalom answered Joab, Behold, I sent to you, saying, Come here, that I may send you to the king, to say, Why am I come from Geshur? it were better for me to be there still. Now therefore let me see the king's face; and if there be iniquity in me, let him kill me.

Basi Yoabu akamwendea mfalme, akamwambia hayo, naye alipomwita Absalomu, yeye akaja kwa mfalme, akainama kifulifuli hata nchi mbele ya mfalme; naye mfalme akambusu Absalomu.

2 Samweli 14:33

So Joab came to the king, and told him; and when he had called for Absalom, he came to the king, and bowed himself on his face to the ground before the king: and the king kissed Absalom.