2 Samweli 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 9 (Swahili) 2nd Samuel 9 (English)

Kisha Daudi akasema, Je! Amesalia mtu mmoja katika nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema kwa ajili ya Yonathani? 2 Samweli 9:1

David said, Is there yet any who is left of the house of Saul, that I may show him kindness for Jonathan's sake?

Palikuwa na mtumishi mmoja wa nyumba ya Sauli, jina lake Siba, basi wakamwita aende kwa Daudi; na mfalme akamwuliza, Wewe ndiwe Siba? Naye akasema Mimi, mtumwa wako ndiye. 2 Samweli 9:2

There was of the house of Saul a servant whose name was Ziba, and they called him to David; and the king said to him, Are you Ziba? He said, Your servant is he.

Mfalme akasema, Je! Hakuna hata sasa mtu ye yote wa nyumba ya Sauli, nipate kumtendea mema ya Mungu? Siba akamwambia mfalme, Yonathani anaye mwana hata sasa, aliye na kilema cha mguu. 2 Samweli 9:3

The king said, Is there not yet any of the house of Saul, that I may show the kindness of God to him? Ziba said to the king, Jonathan has yet a son, who is lame of his feet.

Mfalme akamwambia, Yuko wapi? Siba akamwambia mfalme, Tazama, yumo katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari. 2 Samweli 9:4

The king said to him, Where is he? Ziba said to the king, Behold, he is in the house of Machir the son of Ammiel, in Lo Debar.

Basi mfalme Daudi akatuma watu, akamwondoa katika nyumba ya Makiri, mwana wa Amieli, katika Lo-debari. 2 Samweli 9:5

Then king David sent, and fetched him out of the house of Machir the son of Ammiel, from Lo Debar.

Basi Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli akaenda kwa Daudi, akaanguka kifudifudi, akasujudu. Daudi akasema, Mefiboshethi! Naye akaitika, Mimi hapa, mtumwa wako! 2 Samweli 9:6

Mephibosheth, the son of Jonathan, the son of Saul, came to David, and fell on his face, and did obeisance. David said, Mephibosheth. He answered, Behold, your servant!

Daudi akamwambia, Usiogope, maana bila shaka nitakutendea mema; kwa ajili ya Yonathani, baba yako, nami nitakurudishia mashamba yote ya Sauli, baba yako; nawe utakula chakula mezani pangu daima. 2 Samweli 9:7

David said to him, "Don't be afraid of him; for I will surely show you kindness for Jonathan your father's sake, and will restore you all the land of Saul your father; and you shall eat bread at my table continually."

Akasujudu, akasema, Mimi mtumwa wako ni nini, hata ukamwangalia mbwa mfu kama mimi? 2 Samweli 9:8

He did obeisance, and said, "What is your servant, that you should look on such a dead dog as I am?"

Ndipo mfalme akamwita Siba, mtumwa wa Sauli, akamwambia, Mali yote yaliyokuwa ya Sauli na ya nyumba yake nimempa mwana wa bwana wako. 2 Samweli 9:9

Then the king called to Ziba, Saul's servant, and said to him, "All that pertained to Saul and to all his house have I given to your master's son.

Nawe utamlimia nchi hiyo, wewe, na wanao, na watumwa wako; nawe utamletea mwana wa bwana wako matunda yake, apate chakula ale; lakini Mefiboshethi, mwana wa bwana wako, atakula chakula mezani pangu sikuzote. Basi huyo Siba alikuwa na wana kumi na watano na watumwa ishirini. 2 Samweli 9:10

You shall till the land for him, you, and your sons, and your servants; and you shall bring in [the fruits], that your master's son may have bread to eat: but Mephibosheth your master's son shall eat bread always at my table." Now Ziba had fifteen sons and twenty servants.

Ndipo Siba akamwambia mfalme, Mimi, mtumwa wako, nitatenda hayo yote kama bwana wangu, mfalme, alivyoniamuru. Na kwa habari za Mefiboshethi, mfalme alisema, Atakula mezani pangu, kama mmojawapo wa wana wa mfalme. 2 Samweli 9:11

Then said Ziba to the king, According to all that my lord the king commands his servant, so shall your servant do. As for Mephibosheth, [said the king], he shall eat at my table, as one of the king's sons.

Huyo Mefiboshethi alikuwa na mwana mdogo, jina lake akiitwa Mika. Na watu wote waliokaa nyumbani mwa Siba walikuwa watumwa wa Mefiboshethi. 2 Samweli 9:12

Mephibosheth had a young son, whose name was Mica. All that lived in the house of Ziba were servants to Mephibosheth.

Basi Mefiboshethi akakaa Yerusalemu; maana alikuwa akila chakula sikuzote mezani pa mfalme; naye alikuwa na kilema cha miguu yote miwili. 2 Samweli 9:13

So Mephibosheth lived in Jerusalem; for he ate continually at the king's table. He was lame in both his feet.