2 Samweli 15 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 15 (Swahili) 2nd Samuel 15 (English)

Ikawa baada ya hayo, Absalomu akajiwekea tayari gari na farasi, na watu hamsini wa kupiga mbio mbele yake. 2 Samweli 15:1

It happened after this, that Absalom prepared him a chariot and horses, and fifty men to run before him.

Tena Absalomu huondoka asubuhi na mapema, na kusimama kando ya njia ya lango; kisha ikawa, mtu ye yote aliyekuwa na neno, lililokuwa halina budi kufika kwa mfalme ili kuhukumiwa, Absalomu humwita mtu huyo kwake, na kumwuliza, Wewe u mtu wa mji gani? Naye akasema, Mtumwa wako ni mtu wa kabila fulani ya Israeli. 2 Samweli 15:2

Absalom rose up early, and stood beside the way of the gate: and it was so, that when any man had a suit which should come to the king for judgment, then Absalom called to him, and said, Of what city are you? He said, Your servant is of one of the tribes of Israel.

Naye Absalomu humwambia, Tazama, maneno yako ni mema yenye haki; lakini hapana mtu aliyeagizwa na mfalme kukusikiliza. 2 Samweli 15:3

Absalom said to him, Behold, your matters are good and right; but there is no man deputized of the king to hear you.

Tena Absalomu husema, Laiti mimi ningewekwa kuwa mwamuzi katika nchi hii, ili kila mtu mwenye neno au daawa aje kwangu, nimpatie haki yake! 2 Samweli 15:4

Absalom said moreover, Oh that I were made judge in the land, that every man who has any suit or cause might come to me, and I would do him justice!

Tena ikawa hapo alipokaribia mtu ye yote kumsujudia, hunyosha mkono wake, na kumshika, na kumbusu. 2 Samweli 15:5

It was so, that when any man came near to do him obeisance, he put forth his hand, and took hold of him, and kissed him.

Hivyo ndivyo Absalomu alivyowatendea Israeli wote, waliomwendea mfalme ili wapate hukumu; na hivyo Absalomu akawadanganya watu wa Israeli. 2 Samweli 15:6

In this manner Absalom did to all Israel who came to the king for judgment: so Absalom stole the hearts of the men of Israel.

Hata ikawa mwisho wa miaka minne, Absalomu akamwambia mfalme Tafadhali uniache niende nikaondoe nadhiri yangu, niliyomwekea Bwana huko Hebroni. 2 Samweli 15:7

It happened at the end of forty years, that Absalom said to the king, please let me go and pay my vow, which I have vowed to Yahweh, in Hebron.

Maana mimi mtumishi wako naliweka nadhiri hapo nilipokuwa nikikaa Geshuri katika Shamu, nikasema, Kama Bwana akinirudisha Yerusalemu kweli, ndipo nitamtumikia Bwana. 2 Samweli 15:8

For your servant vowed a vow while I abode at Geshur in Syria, saying, If Yahweh shall indeed bring me again to Jerusalem, then I will serve Yahweh.

Naye mfalme akamwambia, Enenda na amani. Basi akaondoka, akaenda Hebroni. 2 Samweli 15:9

The king said to him, Go in peace. So he arose, and went to Hebron.

Lakini Absalomu akapeleka wapelelezi katika kabila zote za Israeli kusema, Mara mtakaposikia sauti ya tarumbeta, ndipo mtakaposema Absalomu anamilikl huko Hebroni. 2 Samweli 15:10

But Absalom sent spies throughout all the tribes of Israel, saying, As soon as you hear the sound of the trumpet, then you shall say, Absalom is king in Hebron.

Na watu mia mbili walioalikwa wakatoka Yerusalemu pamoja na Absalomu, wakaenda katika ujinga wao wasijue neno lo lote. 2 Samweli 15:11

With Absalom went two hundred men out of Jerusalem, who were invited, and went in their simplicity; and they didn't know anything.

Absalomu naye akatuma kumwita Ahithofeli Mgiloni, mshauri wake Daudi, kutoka katika mji wake, yaani, Gilo, alipokuwa akitoa dhabihu. Fitina yao ikawa na nguvu; maana watu waliokuwa pamoja na Absalomu wakazidi kuwa wengi. 2 Samweli 15:12

Absalom sent for Ahithophel the Gilonite, David's counselor, from his city, even from Giloh, while he was offering the sacrifices. The conspiracy was strong; for the people increased continually with Absalom.

Mjumbe akamfikilia Daudi, akasema, Mioyo ya watu wa Israeli inashikamana na Absalomu. 2 Samweli 15:13

There came a messenger to David, saying, The hearts of the men of Israel are after Absalom.

Basi Daudi akawaambia watumishi wake wote waliokuwa pamoja naye Yerusalemu, Ondokeni, tukakimbie kwa kuwa tusipokimbia hapana mtu miongoni mwetu atakayeokoka mikononi mwa Absalomu; haya! Fanyeni haraka, tuondoke, asitupate kwa upesi, na kutuletea maovu, na kuupiga mji huu kwa makali ya upanga. 2 Samweli 15:14

David said to all his servants who were with him at Jerusalem, Arise, and let us flee; for else none of us shall escape from Absalom: make speed to depart, lest he overtake us quickly, and bring down evil on us, and strike the city with the edge of the sword.

Hao watumishi wa mfalme wakamwambia mfalme, Angalia, sisi watumishi wako tu tayari kutenda lo lote atakalolichagua bwana wetu mfalme. 2 Samweli 15:15

The king's servants said to the king, Behold, your servants are ready to do whatever my lord the king shall choose.

Basi mfalme akatoka na watu wa nyumbani mwake wote wakafuatana naye. Mfalme akaacha wanawake kumi, masuria, ili kuitunza nyumba. 2 Samweli 15:16

The king went forth, and all his household after him. The king left ten women, who were concubines, to keep the house.

Mfalme akatoka, na watu wote wakamfuata; wakakaa kidogo katika Beth-merhaki. 2 Samweli 15:17

The king went forth, and all the people after him; and they stayed in Beth Merhak.

Watumishi wake wote wakapita karibu naye; na Wakerethi wote, na Wapelethi wote, na Wagiti wote, watu mia sita walioandamana naye kutoka Gathi, wakapita mbele ya mfalme. 2 Samweli 15:18

All his servants passed on beside him; and all the Cherethites, and all the Pelethites, and all the Gittites, six hundred men who came after him from Gath, passed on before the king.

Ndipo mfalme akamwambia Itai, Mgiti, Mbona wewe unakwenda pamoja nasi? Rudi, ukakae na mfalme; maana wewe u mgeni, tena u mtu uliyefukuzwa mahali pako mwenyewe. 2 Samweli 15:19

Then said the king to Ittai the Gittite, Why go you also with us? return, and abide with the king: for you are a foreigner, and also an exile; [return] to your own place.

Kwa kuwa umekuja jana tu kwa nini nikusumbue leo, na kukuzungusha huko na huko pamoja nasi nami hapa naenda niwezapo kwenda? Rudi wewe, ukawarudishe na ndugu zako; rehema na kweli ziwe pamoja nawe. 2 Samweli 15:20

Whereas you came but yesterday, should I this day make you go up and down with us, seeing I go where I may? return you, and take back your brothers; mercy and truth be with you.

Naye Itai akamjibu mfalme akasema, Kama aishivyo Bwana, na bwana wangu mfalme aishivyo, hakika yake kila mahali atakapokuwapo mfalme, bwana wangu, ikiwa ni kwa kufa au ikiwa ni kwa kuishi, ndipo atakapokuwapo na mtumwa wako. 2 Samweli 15:21

Ittai answered the king, and said, As Yahweh lives, and as my lord the king lives, surely in what place my lord the king shall be, whether for death or for life, even there also will your servant be.

Basi Daudi akamwambia Itai, Haya, enenda ukavuke. Akavuka Itai, Mgiti na watu wake wote, na watoto wadogo wote waliokuwa pamoja naye. 2 Samweli 15:22

David said to Ittai, Go and pass over. Ittai the Gittite passed over, and all his men, and all the little ones who were with him.

Na nchi yote ikalia kwa sauti kuu, nao watu wote wakavuka, mfalme mwenyewe naye akavuka kile kijito Kidroni, na hao watu wote wakavuka, wakielekea njia ya nyika. 2 Samweli 15:23

All the country wept with a loud voice, and all the people passed over: the king also himself passed over the brook Kidron, and all the people passed over, toward the way of the wilderness.

Na tazama, Sadoki naye akaja, na Walawi wote pamoja naye, huku wakilichukua sanduku la agano la Mungu; kisha wakalitua hilo sanduku la Mungu; Abiathari naye akapanda juu, hata watu wote walipokwisha kuutoka mji. 2 Samweli 15:24

Behold, Zadok also [came], and all the Levites with him, bearing the ark of the covenant of God; and they set down the ark of God; and Abiathar went up, until all the people had done passing out of the city.

Naye mfalme akamwambia Sadoki, Rudisha sanduku la Mungu mjini; nikipata kibali machoni pa Bwana atanirudisha, na kunionyesha tena sanduku hili, na maskani yake; 2 Samweli 15:25

The king said to Zadok, Carry back the ark of God into the city: if I shall find favor in the eyes of Yahweh, he will bring me again, and show me both it, and his habitation:

lakini akisema kama hivi, Mimi si radhi nawe kabisa; basi, mimi hapa, na anitendee kama aonavyo kuwa vyema. 2 Samweli 15:26

but if he say thus, I have no delight in you; behold, here am I, let him do to me as seems good to him.

Kisha mfalme akamwambia Sadoki, kuhani, Angalia, rudini mjini kwa amani, na wana wenu wawili pamoja nanyi,Ahimaasi,mwana wako, na Yonathani,mwana wa Abiathari. 2 Samweli 15:27

The king said also to Zadok the priest, "Aren't you a seer? Return into the city in peace, and your two sons with you, Ahimaaz your son, and Jonathan the son of Abiathar.

Angalia, mimi nitangoja penye vivuko vya jangwani, hata litakaponifikilia neno la kunipasha habari kutoka kwenu. 2 Samweli 15:28

Behold, I will stay at the fords of the wilderness, until word comes from you to inform me."

Basi Sadoki na Abiathari wakalichukua sanduku la Mungu, wakalirudisha Yerusalemu; wakakaa huko. 2 Samweli 15:29

Zadok therefore and Abiathar carried the ark of God again to Jerusalem: and they abode there.

Daudi akapanda akishika njia ya kuupandia mlima wa Mizeituni, akilia alipokuwa akipanda; naye alikuwa amejifunika kichwa chake, akaenda hana viatu; na watu wote waliokuwa pamoja naye wakajifunika vichwa vyao, kila mmoja wao, wakapanda juu, wakilia walipopanda. 2 Samweli 15:30

David went up by the ascent of the [Mount of] Olives, and wept as he went up; and he had his head covered, and went barefoot: and all the people who were with him covered every man his head, and they went up, weeping as they went up.

Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee Bwana, nakusihi, uligeuze shauri la Ahithofeli liwe ubatili. 2 Samweli 15:31

One told David, saying, Ahithophel is among the conspirators with Absalom. David said, Yahweh, please turn the counsel of Ahithophel into foolishness.

Ikawa, Daudi alipofika juu, hapo Mungu alipoabudiwa, tazama, Hushai, Mwarki, akaja kumlaki na joho lake limeraruliwa, tena ana udongo kichwani mwake. 2 Samweli 15:32

It happened that when David had come to the top [of the ascent], where God was worshiped, behold, Hushai the Archite came to meet him with his coat torn, and earth on his head.

Daudi akamwambia, Ukienda mbele pamoja nami, utakuwa mzigo kwangu; 2 Samweli 15:33

David said to him, If you pass on with me, then you will be a burden to me:

lakini ukirudi mjini, na kumwambia Absalomu, Nitakuwa mtumishi wako, Ee mfalme; kama vile nilivyokuwa mtumishi wa baba yako tokea zamani, ndivyo nitakavyokuwa mtumishi wako sasa; ndipo utayavunja mashauri ya Ahithofeli kwa ajili yangu. 2 Samweli 15:34

but if you return to the city, and tell Absalom, I will be your servant, O king; as I have been your father's servant in time past, so will I now be your servant; then will you defeat for me the counsel of Ahithophel.

Je! Hawako Sadoki na Abiathari, makuhani, pamoja nawe huko? Basi itakuwa, kila neno utakalolisikia katika jumba la mfalme, utawaambia Sadoki na Abiathari, makuhani. 2 Samweli 15:35

Don't you have Zadok and Abiathar the priests there with you? therefore it shall be, that whatever thing you shall hear out of the king's house, you shall tell it to Zadok and Abiathar the priests.

Angalia, wanao huko pamoja nao wana wao wawili, Ahimaasi, mwana wa Sadoki, na Yonathani, mwana wa Abiathari; nanyi kwa mikono yao mtanipelekea habari ya kila neno mtakalolisikia. 2 Samweli 15:36

Behold, they have there with them their two sons, Ahimaaz, Zadok's son, and Jonathan, Abiathar's son; and by them you shall send to me everything that you shall hear.

Basi Hushai, rafiki wa Daudi, akaingia ndani ya mji; naye Absalomu akafika akaingia Yerusalemu. 2 Samweli 15:37

So Hushai, David's friend, came into the city; and Absalom came into Jerusalem.