2 Samweli 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 13 (Swahili) 2nd Samuel 13 (English)

Ikawa baada ya hayo, Absalomu, mwana wa Daudi, alikuwa na umbu mzuri, jina lake akiitwa Tamari, naye Amnoni, mwana wa Daudi, akampenda. 2 Samweli 13:1

It happened after this, that Absalom the son of David had a beautiful sister, whose name was Tamar; and Amnon the son of David loved her.

Akasononeka Amnoni, hata akaugua, kwa ajili ya umbu lake Tamari, maana huyu msichana alikuwa mwanamwali, Amnoni akaona ni vigumu kumtendea neno lo lote. 2 Samweli 13:2

Amnon was so vexed that he fell sick because of his sister Tamar; for she was a virgin; and it seemed hard to Amnon to do anything to her.

Lakini Amnoni alikuwa na rafiki, jina lake Yonadabu, mwana wa Shama, nduguye Daudi; naye Yonadabu alikuwa mtu mwerevu sana. 2 Samweli 13:3

But Amnon had a friend, whose name was Jonadab, the son of Shimeah, David's brother; and Jonadab was a very subtle man.

Naye akamwambia, Kwa nini, Ee mwana wa mfalme, unakonda hivi siku kwa siku? Hutaki kuniambia? Amnoni akamwambia, Nampenda Tamari, umbu la ndugu yangu, Absalomu. 2 Samweli 13:4

He said to him, Why, son of the king, are you thus lean from day to day? Won't you tell me? Amnon said to him, I love Tamar, my brother Absalom's sister.

Yonadabu akamwambia, Lala kitandani mwako ujifanye mgonjwa na babako atakapokuja kukutazama, umwambie, Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, anipe mkate nile, akaandae chakula machoni pangu nikione, nikakile mkononi mwake. 2 Samweli 13:5

Jonadab said to him, Lay you down on your bed, and feign yourself sick: and when your father comes to see you, tell him, Please let my sister Tamar come and give me bread to eat, and dress the food in my sight, that I may see it, and eat it from her hand.

Basi Amnoni akalala, akajifanya mgonjwa; na mfalme alipokuja kumtazama, Amnoni akamwambia mfalme Mwache ndugu yangu, Tamari, aje, nakusihi, aniandalie mikate miwili machoni pangu, nipate kula mkononi mwake. 2 Samweli 13:6

So Amnon lay down, and feigned himself sick: and when the king was come to see him, Amnon said to the king, Please let her sister Tamar come, and make me a couple of cakes in my sight, that I may eat from her hand.

Basi Daudi akatuma mjumbe aende nyumbani kwa Tamari, akasema, Nenda sasa nyumbani kwa Amnoni, ndugu yako, ukamwandalie chakula. 2 Samweli 13:7

Then David sent home to Tamar, saying, Go now to your brother Amnon's house, and dress him food.

Akaenda Tamari nyumbani kwa nduguye Amnoni; naye alikuwa amelala. Akachukua unga, akaukanda, akaiandaa mikate machoni pake, akaioka mikate. 2 Samweli 13:8

So Tamar went to her brother Amnon's house; and he was laid down. She took dough, and kneaded it, and made cakes in his sight, and did bake the cakes.

Akalitwaa kaango, akaisongeza mbele yake; lakini alikataa kula. Naye Amnoni akasema, Toeni watu wote kwangu. Wakatoka kila mtu kwake. 2 Samweli 13:9

She took the pan, and poured them out before him; but he refused to eat. Amnon said, Have out all men from me. They went out every man from him.

Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani. 2 Samweli 13:10

Amnon said to Tamar, Bring the food into the chamber, that I may eat from your hand. Tamar took the cakes which she had made, and brought them into the chamber to Amnon her brother.

Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu. 2 Samweli 13:11

When she had brought them near to him to eat, he took hold of her, and said to her, Come, lie with me, my sister.

Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu. 2 Samweli 13:12

She answered him, No, my brother, do not force me; for no such thing ought to be done in Israel. Don't you do this folly.

Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa. 2 Samweli 13:13

I, where shall I carry my shame? and as for you, you will be as one of the fools in Israel. Now therefore, please speak to the king; for he will not withhold me from you.

Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. 2 Samweli 13:14

However he would not listen to her voice; but being stronger than she, he forced her, and lay with her.

Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako. 2 Samweli 13:15

Then Amnon hated her with exceeding great hatred; for the hatred with which he hated her was greater than the love with which he had loved her. Amnon said to her, Arise, be gone.

Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza. 2 Samweli 13:16

She said to him, Not so, because this great wrong in putting me forth is [worse] than the other that you did to me. But he would not listen to her.

Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema, Mtoe sasa mwanamke huyu kwangu, ukafunge mlango nyuma yake. 2 Samweli 13:17

Then he called his servant who ministered to him, and said, Put now this woman out from me, and bolt the door after her.

Naye alikuwa amevaa kanzu ndefu; kwa kuwa kwa nguo hizo huvikwa binti za mfalme waliokuwa wanawali. Ndipo mtumishi wake akamleta nje, akafunga mlango nyuma yake. 2 Samweli 13:18

She had a garment of various colors on her; for with such robes were the king's daughters who were virgins dressed. Then his servant brought her out, and bolted the door after her.

Naye Tamari akatia majivu kichwani mwake, akairarua hiyo kanzu ndefu yake aliyoivaa, akaweka mkono kichwani akaenda zake huku akilia kwa sauti. 2 Samweli 13:19

Tamar put ashes on her head, and tore her garment of various colors that was on her; and she laid her hand on her head, and went her way, crying aloud as she went.

Huyo Absalomu nduguye akamwambia, je! Amekuwa nawe Amnoni nduguyo? Ila sasa tulia, dada; ni nduguyo; usilitie moyoni jambo hili. Basi Tamari akakaa hali ya ukiwa nyumbani mwa nduguye Absalomu. 2 Samweli 13:20

Absalom her brother said to her, Has Amnon your brother been with you? but now hold your peace, my sister: he is your brother; don't take this thing to heart. So Tamar remained desolate in her brother Absalom's house.

Na mfalme Daudi alipoyasikia maneno hayo yote, alikasirika sana. 2 Samweli 13:21

But when king David heard of all these things, he was very angry.

Ila Absalomu hakusema na Amnoni wala kwa heri wala kwa shari; kwa maana Absalomu alimchukia Amnoni kwa kumtenza nguvu umbu lake Tamari. 2 Samweli 13:22

Absalom spoke to Amnon neither good nor bad; for Absalom hated Amnon, because he had forced his sister Tamar.

Ikawa baada ya miaka miwili mizima, Absalomu alikuwa na wenye kukata manyoya ya kondoo huko Baal-hasori uliopo upande wa Efraimu; naye Absalomu akawaalika wana wote wa mfalme. 2 Samweli 13:23

It happened after two full years, that Absalom had sheep-shearers in Baal Hazor, which is beside Ephraim: and Absalom invited all the king's sons.

Absalomu akamjia mfalme, akasema, Tazama sasa, mimi mtumwa wako ninao wakata manyoya ya kondoo; basi mfalme na aende, nakusihi, na watumishi wake pamoja nami mtumwa wako. 2 Samweli 13:24

Absalom came to the king, and said, See now, your servant has sheep-shearers; let the king, I pray you, and his servants go with your servant.

Mfalme akamwambia Absalomu, Sivyo, mwanangu, tusiende sote, tusije tukakulemea. Akamsihi sana; asikubali kwenda, ila akambariki. 2 Samweli 13:25

The king said to Absalom, No, my son, let us not all go, lest we be burdensome to you. He pressed him: however he would not go, but blessed him.

Ndipo akasema Absalomu, Kwamba huji, nakusihi, mwache ndugu yangu Amnoni aende nasi. 2 Samweli 13:26

Then said Absalom, If not, please let my brother Amnon go with us. The king said to him, Why should he go with you?

Mfalme akamwambia, Kwa nini aende nawe? Lakini Absalomu akamsihi sana, naye akamwacha Amnoni na wana wote wa mfalme waende naye. 2 Samweli 13:27

But Absalom pressed him, and he let Amnon and all the king's sons go with him.

Kisha Absalomu akawaamuru watumishi wake, akasema, Angalieni basi, moyo wake Amnoni utakapofurahiwa kwa mvinyo; nami nitakapowaambia, Mpigeni Amnoni, ndipo mwueni, msiogope; si mimi niliyewaamuru? Iweni hodari, iweni na ujasiri. 2 Samweli 13:28

Absalom commanded his servants, saying, Mark you now, when Amnon's heart is merry with wine; and when I tell you, Smite Amnon, then kill him; don't be afraid; haven't I commanded you? be courageous, and be valiant.

Basi watumishi wa Absalomu wakamfanyia Amnoni kama alivyoamuru Absalomu. Ndipo wakaondoka wana wote wa mfalme, wakapanda kila mtu nyumbu wake, wakakimbia. 2 Samweli 13:29

The servants of Absalom did to Amnon as Absalom had commanded. Then all the king's sons arose, and every man got him up on his mule, and fled.

Ikawa, walipokuwa njiani, habari zikamwasilia Daudi, kusema, Absalomu amewaua wana wote wa mfalme, wala hata mmoja wao hakusalia. 2 Samweli 13:30

It happened, while they were in the way, that the news came to David, saying, Absalom has slain all the king's sons, and there is not one of them left.

Ndipo mfalme akainuka, akararua nguo zake, akalala chini; nao watumishi wake wote wakasimama karibu naye, wenye nguo zao zimeraruliwa. 2 Samweli 13:31

Then the king arose, and tore his garments, and lay on the earth; and all his servants stood by with their clothes torn.

Akajibu Yonadabu, mwana wa Shama, nduguye Daudi, akasema, Asidhani bwana wangu ya kwamba wamewaua vijana wote, wana wa mfalme; maana ndiye Amnoni peke yake aliyekufa; yakini haya yamekusudiwa kwa kinywa chake Absalomu tangu siku ile alipotenzwa nguvu umbu lake, Tamari. 2 Samweli 13:32

Jonadab, the son of Shimeah, David's brother, answered, Don't let my lord suppose that they have killed all the young men the king's sons; for Amnon only is dead; for by the appointment of Absalom this has been determined from the day that he forced his sister Tamar.

Basi sasa bwana wangu mfalme asilitie neno hili moyoni, kudhani ya kwamba wana wote wa mfalme wamekufa maana ni Amnoni peke yake aliyekufa. 2 Samweli 13:33

Now therefore don't let my lord the king take the thing to his heart, to think that all the king's sons are dead; for Amnon only is dead.

Lakini Absalomu akakimbia. Na kijana yule aliyekuwa mlinzi akainua macho yake, akaona, na tazama, kuna watu wengi wanakuja kwa njia ya upande wa kilima nyuma yake. 2 Samweli 13:34

But Absalom fled. The young man who kept the watch lifted up his eyes, and looked, and, behold, there came much people by the way of the hill-side behind him.

Ndipo Yonadabu akamwambia mfalme, Tazama, wana wa mfalme wamekuja; kama mimi mtumwa wako nilivyosema, ndivyo ilivyo. 2 Samweli 13:35

Jonadab said to the king, Behold, the king's sons are come: as your servant said, so it is.

Ikawa alipokwisha kusema, tazama, wana wa mfalme walikuja, nao wakapaza sauti zao wakalia; mfalme naye akalia, na watumishi wake wote, kilio kikubwa mno. 2 Samweli 13:36

It happened, as soon as he had made an end of speaking, that behold, the king's sons came, and lifted up their voice, and wept: and the king also and all his servants wept very sore.

Lakini Absalomu akakimbia, akamwendea Talmai, mwana wa Amihuri, mfalme wa Geshuri. Naye Daudi akamlilia mwanawe kila siku. 2 Samweli 13:37

But Absalom fled, and went to Talmai the son of Ammihur, king of Geshur. [David] mourned for his son every day.

Basi Absalomu akakimbia, akaenda Geshuri, akakaa huko muda wa miaka mitatu. 2 Samweli 13:38

So Absalom fled, and went to Geshur, and was there three years.

Mfalme Daudi akatamani kutoka kumwendea Absalomu kwa kuwa ametulizwa kwa habari ya Amnoni, kwa maana amekufa.

2 Samweli 13:39

[the soul of] king David longed to go forth to Absalom: for he was comforted concerning Amnon, seeing he was dead.